JK aiona CCM ni nyoka mzee!!!!!!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aiona CCM ni nyoka mzee!!!!!!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.  CCM kufumuliwa


  Imeandikwa na Jasmin Shamwepu, Dodoma; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:59

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinaonekana kugundua kilipojikwaa na sasa kimedhamiria kukabiliana na kizingiti hicho, ili kurejea kwenye mstari na kujihakikishia ushindi zaidi miaka ijayo.

  Pamoja na kubaini kiini hicho, chama hicho tawala kimesema hakina budi kujipanga na kujifanyia mageuzi makubwa kama ambavyo nyoka hujibadilisha anapozeeka.

  “Chama hiki kimekuwa madarakani kwa muda mrefu na hivyo kusababisha baadhi ya watu kukichoka na kutaka mabadiliko tu hata kama kimefanya mazuri,” alisema Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete jana.

  Kikwete alikuwa akihutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya CCM yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

  “Tutafanya kama nyoka, ambaye kila mara hujivua ngozi yake na kurudi kuwa mpya … nasi katika CCM tutafanya hivyo,” alisema Rais.

  Alisema chama hicho katika mabadiliko makubwa kinachotarajia kuyafanya, kitahakikisha kinarejesha mvuto hususan kwa vijana na kuwataka wanachama wakiwamo viongozi, kukubaliana na hatua hiyo.

  Alisema lazima chama kihuishwe ili kukiongeza mvuto mbele ya watu. Muundo utazamwe kama unakidhi haja, viongozi watendaji nao watazamwe kama wanakidhi haja na kama si mzigo unaokipaka matope chama hicho.

  “Wale tunaoweza kuachana nao sasa tuachane nao kwa maslahi mapana ya chama chetu.

  “Lengo letu kuu ni kutambua nguvu zetu na udhaifu wetu uko wapi na makosa gani tulifanya katika uchaguzi uliopita.

  Lengo letu ni kuimarisha nguvu zetu na kurekebisha kasoro zetu na kusahihisha makosa yetu.

  “Katika tathmini hiyo pia tuangalie nguvu za wapinzani wetu zilikuwa kwenye maeneo gani na udhaifu wao ulikuwa wapi na kisha tutumie udhaifu huo kwa manufaa yetu,” alisema.

  Sambamba na hatua hiyo, aliagiza kufanyika kwa tathmini kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa na kusema ni wazi kuwa katika mchakato wa uchaguzi mwaka jana kulikuwa na kununiana katika kura ya maoni.

  “Hali ya kununiana ilijitokeza katika kura hizo, hivyo sasa ni muhimu kusameheana na kuwa wamoja ili kujenga chama imara kitakachohakikisha ushindi zaidi mwaka 2010 … tuanze maandalizi sasa,” alisema.

  Kikwete alisema tathmini hizo zinatakiwa kufanywa kwa utulivu na kuepusha jazba kama zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi mwaka jana.

  Alisema makosa yaliyofanyika katika uchaguzi huo, yaliwanufaisha wapinzani hata kujiongezea viti vya ubunge na udiwani, kwani hata baadhi ya wana-CCM kwa hasira waliamua kuwapigia wapinzani na wengi hawakujitokeza kabisa.

  “Katika maeneo mengi tuliyoshindwa au hata kufanya vibaya katika uchaguzi, mgawanyiko wakati wa kura za maoni ulichangia sana.

  Baadhi ya wana-CCM waliacha kupiga kura au hata kudiriki kupigia kura wagombea wa upinzani kwa sababu ya hasira,” alisema.

  Aliwasihi wana-CCM kuendelea kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho na pia kujiandikisha kupiga kura “kwani wapiga kura ni waliojiandikisha na si vinginevyo,” alisema.

  Aliwataka pia wanachama wa CCM kuachana na malumbano huku wakitakiwa kujua kwamba chama chao ni chama kikongwe ambacho kimeongoza nchi kwa miaka 34 na kuwaletea maendeleo wananchi.

  Alisema pamoja na kuwapo changamoto ndani ya chama hicho, ni kawaida ya chama chochote duniani na hakuna kiongozi ambaye anaweza kumaliza changamoto zake katika uongozi. “

  Jamani Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa zaidi ya miaka 20 hakumaliza changamoto zote akaja Mzee Ruksa hakumaliza na Mzee Mkapa naye hakumaliza, itakuwa mimi?

  Lakini nataka nikuhakikishieni kuwa nitajitahidi kupunguza changamoto hizo zinazokikabili chama,” alisema Kikwete.

  Aidha, alisema ili kuhakikisha nguvu za chama zinaimarika, chama hicho kitakuwa tayari
  kuachana na wanachama ambao wanaonekana kuwa wasumbufu na hawakubaliani na uamuzi wa chama hicho tawala.

  Alisema kwa sasa chama kina mikakati ya kujiimarisha ili kurejesha majimbo yote na kata zote ambazo zimechukuliwa na vyama vya upinzani.

  Kikwete alisema pamoja na kelele nyingi za baadhi ya wanasiasa bado hawana uwezo wa kushika madaraka makubwa katika nchi, kwani viongozi wengi wanafanya kazi zao kwa jazba.

  Alisema wapo baadhi ya wanachama wananuniana kutokana na makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika vipindi hivyo.

  Alisisitiza chama kujiimarisha kiuchumi akisema hali ya kifedha ya chama hicho si imara na kinategemea zaidi ruzuku inayotokana na ushindi kwa upande wa wabunge na madiwani.

  Kwa ajili hiyo, vyanzo vya asili vya chama kupata fedha za kujiendesha vimesahaulika, kwani miaka yote ada na michango ya wanachama vilikuwa ndizo nguzo na vyanzo vikuu vya mapato ya chama.

  “Hatuwezi kuacha jukumu la kugharimia uendeshaji wa chama chetu mikononi mwa wafadhili matajiri. Tunahatarisha uhuru wa chama chetu,” alionya na kuongeza:

  “Bahati mbaya safari hii ruzuku hiyo imepungua kwa sababu ya nguvu ya vyama vya upinzani kuongezeka.

  Uchaguzi ujao nguvu ya upinzani ikiongezeka zaidi tutakuwa na hali mbaya.”

  Alisisitiza pia uundwaji wa Katiba mpya akisema ni jambo lisiloepukika na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu mchakato utakapoanza na kujiepusha na jazba.

  ”Niwaombe, kuwa wakati huo ukifika wana-CCM na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni na katika kupiga kura ya maoni itakayoidhinisha Katiba hiyo.

  Katiba ni mali ya wananchi, hivyo tunataka tuwashirikishe kwa ukamilifu katika hatua zote muhimu,” alisema.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Pamoja na kubaini kiini hichochama hicho tawala kimesema hakina budi kujipanga na kujifanyia mageuzi makubwa kama ambavyo nyoka hujibadilisha anapozeeka
   
  "Chama hiki kimekuwa madarakani kwa muda mrefu na hivyo kusababisha baadhi ya watu kukichoka na kutaka mabadiliko tu hata kama kimefanya mazuri," alisema Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete jana
   
  Kikwete alikuwa akihutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya CCM yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.   
   
  "Tutafanya kama nyoka, ambaye kila mara hujivua ngozi yake na kurudi kuwa mpya … nasi katika CCM tutafanya hivyo," alisema Rais
   
  Alisema chama hicho katika mabadiliko makubwa kinachotarajia kuyafanyakitahakikisha kinarejesha mvuto hususan kwa vijana na kuwataka wanachama wakiwamo viongozikukubaliana na hatua hiyo
  Sidhani kwa CCM ambao safu zao zote za uongozi ndani na nje ya serikali wamejipanga wazee inaweza kuwa na mvuto kwa vijana........na pengine hili JK analifahamu na ndiyo maana amekifananisha chama chake na nyoka........................................kwenye maandiko matakatifu..........................nyoka hana nia nzuri na mwanaadamu bali kumghilbu aingie motoni.........na hizi ni ghiliba za CCM kujaribu kuwadanganya vijana ambao kwa ulimwengu wa leo hawadanganyiki.........amwulize Ben Ali na Hosni Mubaraka...................
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  CCM ni NYOKA ni SHETANI!vitabu vyote vya mungu biblia,quran vina mlaani NYOKA?Swali watanzania bado wanahitaji kuishi na SHETANI mnyonya damu?
   
 4. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  [QUOTE
  ”Niwaombe, kuwa wakati huo ukifika wana-CCM na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni na katika kupiga kura ya maoni itakayoidhinisha Katiba hiyo.

  Katiba ni mali ya wananchi, hivyo tunataka tuwashirikishe kwa ukamilifu katika hatua zote muhimu,” alisema.


  [/QUOTE]

  Hivi tumekwisha kubaliana kwamba kura ya maoni ndio utakuwa utaratibu wa kuidhinisha katiba? Mbona huyu jamaa anaonekana kuyatoa maamuzi ya jinsi mambo yatakavyokwenda hata kabla ya wabunge na wadau kukubaliana.. nafikiri uwezo wake wa kufikiri umefikia kikomo baada ya 5 star lunch nyingi sana hapo ikulu...JK wake up BADO WATU hawajakubalina ni utaratibu gani utumike...
   
 5. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Na kutoa mfano wa nyoka hauleti picha nzuri maana nyoka siku zote anaendana na ulaghai, ushirikina na kutoa simu ya kuua binadamu na viumbe wengine.. mfano huo labda ni wa mambo yatakayokuja wakumba watu wengi kwa maana ya kwamba anawalaghai, atawapelekea kwa sheik Yahya na unajimu wa nyota na mwisho wa siku wasikokubaliana nae watapelekwa kwenye court of star chamber kama ya Musolini wa Italia na Hitler wa Ujerumani...hayo ndio maana ya nyoka anayeogopewa hata nda ndege wa polini...
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kukifananisha chama CCM na NYOKA huku ni kukimaliza kabisa na hapa tuaona zaidi ya mambo ya ushirikina na machafu zaidi.
  Maneno huumba na kubomoa, subiri uone.
  Nyoka sehemu yeyote ni mnyama mbaya sana wala hahitaji kutolewa mifano katika mambo mhimu ya taifa au chama.
  Hap tunaona Yahaya anafanya kazi tena sana wala sio siri, maana jamaa amejaa mambo ya kutabiri tu na uongo
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hahaaha! Siyo nyoka mzee, bali ni joka zee.
   
 8. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,056
  Likes Received: 3,978
  Trophy Points: 280
  ningekuwa mie nisingefananisha chama changu na nyoka maana hata nyoka awe mpya bado huwa hatari na ana sumu kali anayoweza leta mathara nayo kwa binadamu! Nathani aliyemuandikia hii speech anamatatizo ya kufikiria!
   
 9. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  kwani mlikuwa hamjui kuwa siku nying ccm ni nyoka amnaye ana vichwa saba , nyoka mwenye vichwa saba huwa Habadiliki ngozi yake uzidi kokomaa sio nyoka wote wanabadilisha ngozi kuna aina nyingi za nyoka ambazo hazibadiliki ndio kama CCM, hawaangalii nyakati, naona mkuu ameshutuka yaliyomtokea Mubaraka wa Misri ndio kaona aongee hivi leo, hata hivyo kila kukicha viongozi wa ngazi za juu waliostaafu ameonya chama hiki kikongwe kwa muda mrefu, hawa watu wanaishi kwa kuonyeshana vidole, unafiki, kila kukicha wazee wanatoa onyo, onyo hizi wasipoangalia na kuzitumia mkuu chama kitamfia mikononi
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Badala ya kufikiria kutoa huduma kwa Jamii au wananchi yeye anafikiria uchaguzi ujao kushinda, kweli viongozi hakuna sasa taifa litajengwa lini? Pumbavu Kikwete:twitch:
   
 11. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Nyoka ni nyoka tu hata akijivua gamba na kuwa na gamba jipya sumu yake haibadiliki. Sasa sijui CCM inataka kuwa mjusi au gamba jipya kwa sumu ileile?
   
 12. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyoka ni nyoka hata akijivua ganda Kama ni sumu iko pale pale akikung'ata unakufa tu.
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa ccm ni nyoka(joka) lenye sumu kali.
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  kabisa mkubwa ccm ni nyoka tena wa hatari sana :roll:
   
 15. K

  Kwiifoenda Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna jambo moja hatupaswi kulipuuza katika hotuba ya rais kwa chama! Nalo ni suala la katiba mpya! Nampongeza kikwete kwa hili na vyovyote vile itakavyokuwa, na hata njia itakayotumika, sisi wananchi ndio msingi wa Katiba mpya! Lazima nikiri tuna bahati sana, kwamba kama tutakuwa makini na tukachanga karata zetu vizuri na wasomi wakaacha unafiki, tunaweza kupata katiba mpya nzuri bila kumwaga damu zaidi kama wenzetu wa kenya, zimbabwe, tunisia, misri n.k! Mimi nitamkumbuka kikwete kwa mambo mawili, moja ni uhuru wa vyombo vya habari na pili ni kuridhia kuandika katiba mpya! Ni mambo ya kishujaa mno kwa historia ya dunia! Tukipata katiba mpya itakayoweka misingi mizuri na maadili ya taifa basi kikwete atakuwa kwenye vitabu vya historia ya Tanzania!
   
 16. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  That was a bad analogy to be used in a superstitious society such as Tanzania.. But for the first time CCM has recognised that it is in dire need of radical reforms. It is a welcome development. Lets wait and see whether anything happens.
   
Loading...