JK ahofia CCM na UvCCM kumfia mikononi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ahofia CCM na UvCCM kumfia mikononi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, May 21, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,068
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakati akiwahutubia wanachama wa UVCCM katika mkutano wao uliofanyika mkoani Iringa hivi karibuni na kupelekea Mwenyekiti wa UVCCM Ndg Yusupf Masauni kujiuzulu kwa tuhuma za kugushi nyaraka kuhusu umri wake, JK aliwakemea wanachama wa UVCCM wa sasa kwa kile alichokiita njama za kumalizana; na kuwatahadhrisha kuwa tabia na mienendo yao itaiua taasisi ya UVCCM.

  Jk alifikia hatua ya kuwakumbusha enzi zao katika Umoja huo walipokuwa wakidumisha hali ya amani, upendo, mshikamano na umoja. Na kuwataja wanachama wenzie wa enzi hizo akina Seif Khatibu Anna Makinda n.k ambao kwa madai yake ni marafiki wakubwa hadi sasa.

  Cha kushangaza Jk mwenyewe na wote aliwataja ndio wanaoongoza CCM na Serikali ya Tanzania kama alivyokuwa Baba wa Taifa wakati wako ni vijana katika Umoja huo. Lakini alichofanya Baba wa Taifa kama baba katika familia alifanikiwa kukuza TUNU adimu sana za amani, upendo, mshikamano na umoja; ambazo JK anazitamani ziwepo sasa.

  Jk amesahau msemo wa wingereza "Like Father like son". Enzi za uongozi wa Baba wa Taifa watanzania wote wakubwa na wadogo ikiwemo vijana walikuwa wakipata malezi mema kutoka kwa waasisi wa Taifa kwa misingi ya usawa ndio zikajengeka TUNU za amani, upendo, mshikamano na umoja. Lakini baada ya Tanzania kuchukuliwa na akina JK waliokuwa UMOJA wa Vijana wa wakati huo, wamefanikiwa sana kujenga matabaka, ubinafsi, matumizi mabaya ya madaraka kujinufaisha, kulindana na kubebana kwa misingi ya ukabila, udini, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi. Wakati wanafunzi wa NYERERE wakiyatenda haya watoto na vijana wanaona na kujifunza.

  Mfano mzuri ni kura za maoni za Urais mwaka 2005, JK na washirika wake walipowachafua wagombea wengine akiwemo Ndg Salim Ahmed kwa kumuita ni Mwarabu, Hizbu na majina mengine ya aina hiyo. Kwa vijana wengi ndio ilikuwa mara ya kwanza kushuhudia watu wazima wakitumia vyombo vya habari kutukanan hadharani, na kibaya zaidi kwa kuwatumia watoto wadogo na vijana ambao wengi wao wameajiriwa katika vyomb vya habari vilivyokuwa vikitumika kutukanana, kuuza magazeti yeliyosheheni matuzi ya nguoni kwa wagombe wengine n.k.

  Yote haya yalifanywa na watu na makundi yaliyopangwa na JK mwenyewe na washirika wake, sasa anashanga nini UVCCM ya leo kutumia staili hiyo ya kumalizana. Angalau UVCCM ya sasa imetuthibitishia jambo moja kuwa hata ndani ya Kamti Kuu ya CCM uozo umejaa. Tuwapongeze kwa kshindwa kuvumilia hali hiyo. Sasa JK Ndg S A Salim ulimtukania nini? Ni urais tu, ndio ulikufanya kuvunja utamaduni wa watanzania wa kuheshimiana na kustahiana?

  JK hana sifa za kushangaa yote yanayotendeka kwa kuwa ni yeye aliyeasisi "MTANDAO" ndani ya CCM na siasa za makundi ambayo kazi yake kubwa na kumalizana ili kugombea madaraka; na madaraka akayapata kwa kutumia mbinu hizo chafu. Leo anawashangaa nini vijana na watoto wakiiga, au alifiikiri hawakuona na kujifunza wakati anawatumia kuwamaliza wagombea wake?

  Jk and team waliokuwa Umoja wa Vijana wa TANU na baadaye CCM wakati waasisi wa Taifa hili walipojenga Taifa lenye amani, upendo, mshikamano, na umoja wanapaswa kuwapatia watanzania majibu nini kimetokea hadi TUNU kupotea wakati nchi ibado inaongozwa na Chama na watu wanaoaminika kuwa wanafuniz wa Baba wa Taifa badala ya kuanza kulalama.

  JK KUMBUKA BABA WA TAIFA ALIWAHI KUULIZA WATU WANAKIMBILIA NINI IKULU, KUNA BIASHARA GANI?
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Asipo jiuzuru mwenyewe lazima ccm itamfika mikononi mwake tena kwa kifo kibasa ambacho kinaweza kuleta machafuko.
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM itamfia mikononi tu...tusubiri muda ufike!!
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Imfie mara ngapi? kuna msemo mmoja by Octavian Butler unasema hivi nanukuu, "When no influence is strong enough to unify people, they divide, They struggle, one against one, group against group", Sasa tizama CCM ya leo nadhani utakubaliana na msemo huo hapo kuwa CCM ishakufa hakuna tena wa kuiongoza wala kuitawala kwani hakuna mwenye influence ndani ya CCM.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  This is what I'm talking about!.. Tujiulize kwa nini JK ana wasiwasi?..Upinzani ndani ni moja ya njia za kupata Ushindi. Nawasifu sana vijana hawa kwa kuanzisha Mapinduzi ndani ya chama kuliko hao CCJ wanaotaka kukimbia chama kuleta mabadiliko.
   
 6. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,327
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  vijana wa uvccm wanastahili pongezi za dhati
   
Loading...