JK Agoma Kusaini Sheria Mpya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Agoma Kusaini Sheria Mpya!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Apr 15, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  K agoma kusaini sheria mpya

  *NI YA KAMPUNI ZA SIMU KUJISAJILI SOKO LA HISA DAR

  Ramadhan Semtawa

  BAADA ya kusaini Sheria ya gharama za uchaguzi ambayo imegubikwa na utata, Rais Jakaya Kikwete ameshtuka na amegoma kusaini sheria inayobana makampuni ya elektroniki ikiwemo ya simu na posta kujisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

  Habari za uhakikika zimelidokeza gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete alikataa kusaini sheria hiyo akitaka Muswada wake ufanyiwe marekibisho katika kifungu cha 26 ambacho pamoja na mambo mengine, kinabana makampuni ya simu kujisajili DSE kwa lazima.

  Kifungu hicho tayari kilipingwa na kampuni za simu nchini wakati mjadala huo ukijadiliwa kwenye mkutano wa 18 wa bunge mjini Dodoma, ambako walitaka kilegezwe.

  Said Arfi ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani katika mambo ya mawasiliano, sayansi na teknolojia akisoma maoni ya kamati, alipinga vifungu mbalimbali vya muswada huo, kikiwemo kifungu cha 26.


  Kwa habari zaidi soma Mwananchi.
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Safari hii ameisoma kwanza nini? Maana ana tabia ya kujiingiza kichwa kichwa.
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280

  Hana lolote huyo..atie sign kama kawaida yao...au issue haina maslahi ki-uchumi kwake na washkaji zake nn?...sipendi kuamini kuwa eti yeye au wasaidizi wake wamestukia vimeo kwenye sheria ndio amegoma kutia sign....hakuna watu smart kiasi hicho nyuma yake..yeye kimeo na wasaidizi vimeo mbayaaaa....NI MAONI TUU
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nahisi hata hajaisoma ila alikuwa busy kuandaa safari ya Marekani!!!? Halafu itakuwaje awabane waingie DSE kwa lazima ili wagawane faida na watanzania wakati si lengo la RA na other shareholders kuwapa wazalendo ahueni??? Fungueni macho jamani!!!! Ni lazima alinde interest za swahiba kwanza!! Sisi walalahoi tutamsaidiaje? Hajawa serious na haitatokea awe serious, labda akiamua kupumzika angalao mwezi mmoja nyumbani apitie masuala muhimu kwa Taifa hili. Pity!
   
Loading...