JK agoma kusaini sheria mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK agoma kusaini sheria mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  JK agoma kusaini sheria mpya
  *NI YA KAMPUNI ZA SIMU KUJISAJILI SOKO LA HISA DAR

  Ramadhan Semtawa

  BAADA ya kusaini Sheria ya gharama za uchaguzi ambayo imegubikwa na utata, Rais Jakaya Kikwete ameshtuka na amegoma kusaini sheria inayobana makampuni ya elektroniki ikiwemo ya simu na posta kujisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

  Habari za uhakikika zimelidokeza gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete alikataa kusaini sheria hiyo akitaka Muswada wake ufanyiwe marekibisho katika kifungu cha 26 ambacho pamoja na mambo mengine, kinabana makampuni ya simu kujisajili DSE kwa lazima.

  Kifungu hicho tayari kilipingwa na kampuni za simu nchini wakati mjadala huo ukijadiliwa kwenye mkutano wa 18 wa bunge mjini Dodoma, ambako walitaka kilegezwe.

  Said Arfi ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani katika mambo ya mawasiliano, sayansi na teknolojia akisoma maoni ya kamati, alipinga vifungu mbalimbali vya muswada huo, kikiwemo kifungu cha 26.

  Upinzani huo wa kambi ya upinzani na kampuni za simu, unaelezwa na chanzo hicho cha habari kwamba ulikuwa na nguvu ya hoja ambazo zimemshwawishi Rais Kikwete kugoma kufanya kazi yake ya kikatiba ya kusaini sheria hiyo ili ianze kufanyakazi.

  Hata hivyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Peter Msolla alipoulizwa kuhusu hatua hiyo ya Rais, alijibu kwa kifupi: "Sijapata taarifa hizo, lakini pia Rais halazimishwi kusaini au kutosaini muswada wa sheria."

  Chanzo cha habari kilifafanua kwamba, Rais ameona ni vema serikali iweke mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kuwekeza hisa DSE na si kulazimisha kama kifungu cha muswada huo kilivyokuwa kikisisitiza.

  "Rais amekataa kusaini sheria hiyo na itarudishwa bungeni ili ifanyiwe marekebisho. Serikali imeleta mapendekezo ya kubadili section (kifungu) ya 26, its a blow to bunge and Msolla (Ni pigo kwa Bunge na Msolla)," kiliweka bayana chanzo hicho cha kuaminika.

  “Kwa mujibu wa taarifa hizo huru, inachopaswa kufanya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji na si kuwalizimisha,” kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho huru kilisisitiza kwamba: "Economically you don't force to list but you provide incentive to list (Kiuchumi, huwezi kulazimisha kusajili bali unaweka mazingira ya kuvutia watu wajisajili".

  Sheria hiyo, pamoja na mambo mengine ulikuwa ukitoa nafasi pia kwa kampuni za simu kutumia miundombinu ya pamoja katika kupitishia na kutoa huduma za mawasiliano.

  Lengo la mpango huo lilikuwa ni kupunguza athari za wingi wa minara hivyo kuweza hata kusababisha mwingiliano wa masafa na hivyo kuleta athari kwa binadamu.

  Kampuni kubwa za simu nchini ni Vodacom, TTCL, Zain, Tigo na Zantel huku kampuni nyingine zikichupuka kwa kasi kama vile, Benson Informatics (BoL), Six Telecoms. Pia kuna kampuni zingine zinahusu huduma za kiposta.

  Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete, amesaini sheria mbalimbali nyeti ikiwemo ile ya Kudhibiti wanaoeneza virusi vya Ukimwi kwa nguvu, Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007, Kuzuia Fedha chafu ya mwaka 2007 na Kitengo cha Kuzuia Fedha chafu (FIU).

  Hata hivyo, kati ya sheria zote hizo, Sheria ya gharama za uchaguzi imemuweka katika wakati mgumu baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa, kuibua tuhuma akisema kifungu kinachohusu idadi ya wapambe wa uchaguzi kilichomekwa nje ya bunge na Rais akasaini bila kujua.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19226
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  amestuka kidogo,
   
 3. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimepata taarifa kuwa JK ilikuwa akafungue kiwanda kimoja huko Kibaha ambacho kinaunganisha magari mwezi uliopita - kumbe wangemwingiza mkenge akastuka hakwenda. Utapeli wa wawekezaji bomu uchunguzwe kabla ya kumhusisha Mkuu wa nchi.
   
Loading...