Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,109
- 53,626
Siasa ina mashujaa wake. Wanaohimili mikikimikiki ya kila wiki na mambo yao yanatiki. Mbunge John John Mnyika wa Kibamba kwa tiketi ya CHADEMA ni kati ya wanasiasa mashujaa hapa Tanzania. Mnyika hana bei,ni mwanaCHADEMA hasa.
Mnyika aliandamwa kwa lawama na kubanwa kipropaganda. Mnyika alisemwa amekasirika kwenda Lowassa CHADEMA,akawa kimya. Akasemwa anaumwa hata kuchanganyikiwa,akawa kimya. Akasemwa hamkubali Katibu wake Mkuu mpya,Dr. Mashinji,akawa kimya. Akaandikwa na kusemwa kuwa anajiandaa kuhama chama chake,akawa kimya.
Hata hapa Dodoma,alitajwatajwa kama mmoja wa watakaofanyiwa usajili tarehe 23 mwezi huu. Mnyika hajali wala kutikisika. Anaendelea kutekeleza majukumu yake muhimu ya chama chake kwa kusonga mbele kuelekea kwenye kilele. Mnyika si wa kawaida. Hajajibu wala kuyumbishwa na yaliyosemwa. Hana bei. Ni shujaa.
Amenikumbusha mbinu za kuishi Seminarini. Seminari aliyosoma Mnyika imempika. Imempa uhodari mahiri. Ukimya nao ni jibu mujarabu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Na akatoka na A's 9 ambapo hakuna mwana CCM nchi hii amewahi kuipata.
Hivi Lizaboni ulipata ngapi?