Jiunge na program ya Mafunzo ya Maarifa ya Kazi

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Wapendwa naamini hamjambo kabisa.
Napenda kuwajulisha kuwa tangu nimewajuza kuhusu program ya Maarifa ya Kazi, wale waliojitokeza na kuanza kupata huduma hii wanaendelea vizuri.
Kwa ujumla huduma hii inatolewa kwa njia ya masafa. Unajifunz hapo ulipo na unafanya kazi zako hapo ulipo. Hakuna haja ya kutumia mda wako kusafiri, kuachana na familia yako, kusitisha shughuli zako zingine n.k
Kwa ufupi ni kwamba mafunzo yenyewe yanakuwezesha kufanya yafuatayo:-
1. Kuzalisha chakula cha mifugo aina mbali mbali maarufu kama hydroponics Green Fodder
2. Kuandaa bustani za mbogamboga nyumbani kwako pasipo kuwa na shamba.
3. Kuandaa viua wadudu kwa njia ya asili.
4. Kuandaa mbolea za maji zisizokuwa na madhara kwenye mimea na mifugo.

Mafunzo hayo yatafungua fursa nyingi kwa vijana walioko katika eneo lako sambamba na kukufungulia fursa nyingine wewe mwenyewe utakayekuwa umejifunza.
Nakaribisha swali lolote lile kwa yule ambaye atakuwa amesoma na hajanielewa.
Pia nichukue fursa hii kuwashukuru wataalam wa mifugo toka Mwabuki walionitembelea shambani kuja kuangalia namna program inavyoendelea. Naamini zipo taasisi nyingine zinazoweza kushirikiana nami katika shughuli hii ila hawajapata nafasi ya kujua nini kinaendelea.
Watanzania tumekuwa tukishangaa ni kwa nini mayai toka Uganda yanauzwa kwetu kwa bei ya chini tofauti na ya kwetu. Siri ndo hiyo, wao walianza mapema kutumia teknolojia hii katika malisho ya kuku na wanyama wengine.
Niko tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi za kiserikali, zisizo za kiserikali na watu binafsi kuhakikisha jamii ya watanzania inatokana na mawazo mgando ya kuendelea na ufugaji wa kizamani.
Wale members mlionitafuta na kunishirikisha katika hili nawashukuruni sana, tuendeleeni kuwajuza na wengine.
'JF zaidi ni zaidi ya Chuo
upload_2017-6-1_12-16-45.jpeg


Kwa kuwa mda mwingi nakuwa field, nawaombeni mnitafute kwa simu, namba zipo hapo kwenye fomu iliyoambatanishwa hapo. Kumbuka kilimo na ufugaji ni shughuli inayohitaji kuwa serious zaidi ya kitu chochote.
 
Je ninafanyaje ili niweze kujiunga katika hayo mafunzo?
Nikupongeze kwa kuona umuhimu wa program hii. '
Kuna fomu ya kujaza ili ujiunge na hii program, fomu hiyo tunakutumia kwenye e-mail yako.
 
Okay! Ngoja nitafakari kwanza, nikiwa na swali nitarudi...
Unakaribishwa,
Wapo waliojiunga na wanaendelea vyema huko walipo. Japo ni wachache lakini inatia moyo kwa sababu wale ambao tayari walikuwa kwenye changamoto ya malisho ya mifugo ndo walikuwa wa kwanza kukubali kujiunga na program hiyo.
 
Ngoja na mie niku PM unipe ushauri, mipapai yangu kila ikitoa maua yanaliwa na vidudu kama sisimizi halafu yananyauka!!!
 
Ngoja na mie niku PM unipe ushauri, mipapai yangu kila ikitoa maua yanaliwa na vidudu kama sisimizi halafu yananyauka!!!
KUNA UWEZEKANO KUNA MAJI MENGI HAPO SHAMBANI KWAKO ...
PILI .. JARIBU KUNYUNYIZIA JUISI YA NDULELE KWA MCHANGANYIKO NITAKAOKUELEKEZA HAPO BAADAE.
 
Back
Top Bottom