jitokezeni tumchangie-MPENDAZOE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jitokezeni tumchangie-MPENDAZOE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Feb 25, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Wamchangia Mpendazoe kuendesha kesi yake Send to a friend Thursday, 24 February 2011 21:22 0diggsdigg

  James Magai
  ALIYEKUWA mgombea ubunge katika Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, Fredy Mpendazoe, sasa amepata uhakika wa kesi yake, kusikilizwa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, baada ya wananchi kumchangia fedha za kuendesha kesi.
  Mpendazoe ambaye amefungua kesi mahakamani, akipinga matokeo ya ubunge katika jimbo hilo, Desemba mwaka jana aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba msamaha au punguzo la kiwango cha fedha za kuwezesha usikilizwaji wa kesi yake.

  Februari 15, mwaka huu, mahakama hiyo, mbele ya Jaji Profesa Ibrahim Juma ilitupilia mbali maombi yake hayo kutokana na dosari za kisheria zilizobainika katika hati yake ya kiapo.


  Hata hivyo jana wakili wake Peter Kibatala aliliambia Mwananchi kwamba sasa mteja wake yuko tayari kutoa Sh15 milioni kwa ajili ya dhamana ya kusikiliza kesi hiyo.

  Wakili Kibatala alisema mteja wake amepata kiasi hicho, baada ya wanachama wa chama chake na wananchi mbalimbali kumchangia.

  “Baada ya maombi yetu ya msahama wa dhamana ya kesi hiyo, kubainika kuwa na dosari za kisheria tulikusudia kuwasilisha maombi mapya, lakini wananchi wenye mapenzi mema walijitolea kumchangia mteja wangu na kufaniwa kupata pesa hizo.

  “Kwa hiyo, sasa tumeamua kutoa fedha hizo ili kuharakisha usikilizwaji wa kesi yetu, na tuko tayari kuiomba mahakama ituruhusu tutoe fedha hizo ili itupangie tarehe ya kesi yetu kuanza kusikilizwa,” alisema waakili Kibatala.

  Kuwa wa mujibu sheria ya uchaguzi, kila mlalamikaji anapaswa kutoa Sh5 milioni kwa kila mlalamikiwa kwenye kesi moja, kama dhamana kwa ajili ya kuendesha kesi hiyo.

  Alisema kwa kuwa kwenye kesi hiyo, kuna walalamikiwa watatu, yaani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliyeshinda ubunge katika jimbo hilo, Dk Makongoro Mahanga na msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Mpendazoe alipaswa kutoa Sh15milioni.

  Sheria hiyo, pia inatoa nafasi kwa mlalamikaji kupeleka maombi ya kusamehewa kabisa fedha hizo au kupunguziwa kiwango hicho, kulingana na sababu atakazozitoa na kutegemeana na mazingira ya uendeshaji wa kesi hiyo.


  Katika maombi ya awali, awali Mpendazoe alidai hana uwezo wa kulipa kiasi hicho, kilichowekwa kisheria kwa sababu alitoka kwenye kampeni ndefu za uchaguzi ambazo pia alifadhiliwa na wapenzi wake na kwamba sasa hali ya uchumi siyo nzuri kiuchumi.

  Katika uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alimtangaza mgombea wa CCM, Dk Mahanga kuwa mshindi baada ya kupata kura 43,555 na Mpendazoe kura 38,150.
   
 2. k

  kukubata Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunatoa kiasi gani?
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  chochote ulicho nacho toa utasaidia
   
 4. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kwani ile kesi aliyoshinda marehemu Advocate Julius Ndyanabo ya kuruhusu kuweka dhamana ya tzs 500 badala ya 5ml katika kupinga kesi za ubunge iliishia wapi?? Maana hii nchi kwa sasa siielewi kabisa mambo yanavyoenda.
   
 5. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,299
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  acheni kujisumbua huyo mtu ameshapoteza muelekeo achaneni naye!
   
 6. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,299
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  chochote unamaanisha nini yakhe! mzima weye? haya mpe ulichonacho basi! si una huruma weye?
   
 7. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,299
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  dah1 hali mbaya naona watu wengi wameshachanganyikiwa sasa wewe ndio kabisaa! mtu umechoka laini unataka kujimaliza kwa starehe za mwenzako? ama kweli wajinga bado wengi nchi hii. kazi tunayo!
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Fedha za ruzuku za CHADEMA zinafanya kazi gani au ni kwa ajili ya posho za maandamano ? CCM wao wameisha sema pesa za kesi watalipa kutoka kwenye mfuko wa chama
   
 9. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Please, we are people power. Tunataka kumchangia. atufanyeje. Give account or any other means.
   
 10. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,299
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  acha u..la! utaibiwa wewe!
   
 11. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ccm na mahakimu damu damu cjui itakuaje hukumu inaweza tolewa 2015!!! God forbid!!!
   
Loading...