Jitenge kidogo, utagundua mengi sana

Jitenge kidogo, utagundua mengi sana

Binadamu amekuwa kiumbe katili katika ulimwengu huu kuliko wanyama wa mwituni. Binadamu tunaogopana tena kwa tahadhari kubwa sana.Kuwa karibu na mnyama yoyote ni salama zaidi kuliko ukaribu na mwanadamu hasa ngozi nyeusi.
 
Hii ni kwa wale ambao hawawezi kufanya kitu chochote bila kushirikisha marafiki.

Umezungukwa na kundi la watu kiasi kwamba huna maamuzi yako binafsi.

Ukipata pesa unawashirikisha, ukipata mchumba unawashirikisha, unajenga unawashirikisha, unataka kuanzisha biashara unawashirikisha.

Mwenyewe unadhani wanafurahia mafanikio yako kumbe baadhi yao wanatamani usifanikiwe kuwazidi wao.

Na ndio maana kuna baadhi ya watu usipowashirikisha mambo unafanikiwa,lakini ukiwashirikisha tu hufanikiwi.

Ni wakati wako sasa Jitenge nao kidogo na kuwa busy na shughuli zako uone watakavyokasirika maana hawatajua nini kinaendelea juu yako.

Hii ni kwa sababu unawaambia kila kitu, mfano ukigombana na mke wako, mme wako, au wachumba zenu.

Kumbe wanatamani muendelee kugombana tu, au uendelee kufeli tu kwenye mambo yako.

Hebu jaribu kukaa kimya kidogo kwa manufaa yako mwenyewe na mambo yako yatanyooka mwenyewe utashangaa.
Waamuzi 16:5

Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
 
Back
Top Bottom