Jitahidi mwanao asisome masomo ya Sanaa


Ushaur mzur, ila jaribu kufikiria na mfumo wetu wa elimu unasupport inshu za sayansi?

Usifikir hakuna asiyependa mwanae asome sayansi lkn je shule zetu hiz za kata zina miundombinu mizur ya kumfanya mwanafunzi asome sayansi? Kuna watu walikuwa wanapenda kuwa madokta lkn ndoto zao zilikwamishwa kwan hapo anaposoma unakuta hakuna mwalimu hta mmoja wa sayansi, shule ambazo zina miundombinu ya kutosha kma walimu, maabara, vitabu ya sayansi vya kujifunzia na kufundishia ndio ambazo n private school na zina toza ada kubwa ili uweze kuipata io elimu

#Tutafakar
 
A level nilichaguliwa kusoma PCB nikachagua Arts , sioni tatizo mpaka sasa. Maisha hayapangwi kwa somo unalosoma darasani mkuu, haiko hivyo.
 
nasikia Mafuruki na yule Mo Ibrahim ni wanasayansi. inawezekana wanasayansi huridhika na ajira na mishahara yao ambayo relatively ni mizuri . ila ninaamini ukichukulia wastani wa kipato cha graduate wa art na sayansi, wa sayansi yuko mbali sana.
 
marijuana

Nilitaka ku-comment lakini naona umeshamaliza Mkuu, mfumo wetu wa elimu una maambukizi na tayari umeshaathiri mazao mengi mno, kama thread ya mdau inavyojipambanua!
 
Last edited by a moderator:
ndiyo maana nimesema jitahidi. we fanya bidii zote mwisho wa siku matokeo yake yataamua.
 

I see unapotosha watu sana. Mtoto halazimishwi kusoma masomo ya science au art ni uwezo wake ndiyo utaamua. Mimi mwenyewe ni shahidi, nilipokuwa O level nilichukua masomo ya science, lakini yalinishinda kabisa, hadi nilipoamua kubadili na kusoma art hadi A level. Nimejikuta kwenye mafanikio makubwa hadi nimefika chuo kikuu. Kwa sasa nimepata kazi nzuri kwa masomo ya art.
Nakumbuka nikiwa O level kuna rafiki yangu alikuwa mkali sana wa mathematics, lakini alikuwa anafeli hadi Kiswahili achilia mbali english, history na masomo mengine ya art, wakati sisi ndiyo yalikuwa yanatutoa. Haya siyo mambo ya kulazimisha. Zungumza na walimu waliosoma psychology watakuelewesha.
 
mimi pamoja na kusoma sayansi nataka kujiajiri na soon ntajiajiri fulltime. hatuwezi pinga kwamba nchi yetu ambayo middle class ni wachache kujiajiri ni kugumu na ajira inaplay part kubwa sana.
 
Ila mkuu education sio tu for employment sake...but kwa kuwa umechukua kigezo cha employment apo poa
 
Bwana mdogo umetoa ushauri wa bure bila malipo, kazi kwetu
 
Ila mkuu education sio tu for employment sake...but kwa kuwa umechukua kigezo cha employment apo poa
huoni hata kujiajiri mtu wa sayansi atakuwa na chance kubwa?
 
Hii ni dunia ya habari(information age),sio dunia ya viwanda(industrial age).

Hivyo kumsomesha mtot kw target y ajira ni makosa makubwa sana. Mtoa mada na wengineo weny fikra km zako,waandaen wenenu kusimama wenyew kw kuwapatia maarifa.

Habar za ajira kipind hiki zinazid kufa,na zitapotea kw kiwango kikubw sana miaka kadhaa ijayo. Huko ndiko dunian inakoenda. Kumsomesha mwanao na stiry za ajira,salary,pensio(security)ni makosa makubwa sana. Tabia za kichumi zinabadilika sana,tusipokuw makini tutaitukana serikali hadi tunaingia mavumbini.

Mtot apewe elimu,akomae aje afanye chchte kimkomboe. Mwenye elimu huwa hafi njaa,regardless amesomea kitu gani. Zingatia hilo mtoa mada.
 
Ila mkuu education sio tu for employment sake...but kwa kuwa umechukua kigezo cha employment apo poa
Umeona hapo.

Na ndio maana siku zote ukichunguza mtu aliesoma(wengi wao) haamini kama kuna maisha bila ya kazi(KUJIAJIRI).

Kwa kweli wanakuwa waoga sana, mtu yuko tayari aendelee kupata mshahara mdogo lakini aendelee kufanya kazi
 
Mtoa mada nathubutu kukuita mbumbumbu kwa hoja kwamba ili jamii iendelee inahitaji fani zote ziwe na wasomi waliobobea. Hivi tusipokuwa na wana historia kuna uhai kama taifa.

Hivi tukikosa wasomi wa lugha jamii itakuwaje ya majuha ya lugha? Hivi tukikosa wanasheria tutakuwa jamii gani? Unaonekana bado hujayajua maisha aidha upo high school.

Nakushauri kakojoe ukalale ukukua tutakuja kudadili nawe
 
huoni hata kujiajiri mtu wa sayansi atakuwa na chance kubwa?

Kujiajiri ni kote kote mkuu..au unazungumkia ajira gani...kama post yako imelenga kutarget soko la ajira la bongo sawa..ila kwa mimi naamini elimu sio tu kupata ajira bali ni njia ya kuongeza utambuzi na pia education inaweza kuwa leisure kama utaspecialize kwenye kitu ambacho unapenda
 
kiongozi N.korea aliwahi ulizwa mnawezaje kujitegemea? akasema moja ya sababu ni kuulimit humanity sciences to 30% ya wanFunzi vyuoni. kwa hiyo wakazlisha wanasayansi kwa wingi. sayansi ndiyo nguzo ya maendeleo kwa nchi yoyote.
 
Janga la ajira halitaisha nchi hii kwa fikra hizi. Mie sijasoma arts lakini nimejiajiri nje kabisa ya taaluma. Na ninajuta sana kuikosa taaluma ya uhasibu na uchumi.
 
kiongozi N.korea aliwahi ulizwa mnawezaje kujitegemea? akasema moja ya sababu ni kuulimit humanity sciences to 30% ya wanFunzi vyuoni. kwa hiyo wakazlisha wanasayansi kwa wingi. sayansi ndiyo nguzo ya maendeleo kwa nchi yoyote.

Hapo umeongea kuongeza % which I agree but hoja kwamba let us get rid of arts haina mashiko kabisa you must concur ndio maana NKorea haina uhusiano mzuri diplomatically na mataifa ya dunia. Huoni hapo tatizo
 
Mimi nafikiri sina cha nyongeza.

Umemaliza kila kitu.

Asieweza kukuelewa hapo kamwe hatoweza kukuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…