Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,250
- 79,799
JISAMEHE ILI MAISHA YAENDELEE!
Anaandika, Robert Heriel
Wazazi walikukazania usome lakini ukapuuza, ukafeli sasa unaona Maisha ni magumu, unawaelewa ukiwa umechelewa, Usijilaumu; imetosha sasa! Jisamehe uendelee na Maisha mengine. Ikiwezekana kawaombe wazazi wako Msamaha.
Ulikatazwa usicheze na wanaume, ukashauriwa vya kutosha lakini haukusikia, Matokeo yake ukazalishwa na kutelekezwa, imetosha sasa, Usijilaumu. Kiri kabisa ulikosea ili Nafsi yako iwe na Amani. Kukiri kosa ni hatua muhimu katika kujisamehe.
Ulikatazwa usiendekeze Umalaya na uasherati, ukakaidi sasa umekumbwa na magonjwa ya zinaa kama Ukimwi. Ni kweli inaumiza na pengine umekata tamaa. Imetosha kujilaumu. Umekiri vyakutosha. Sasa jisamehe.
Uliambiwa unywe pombe Kwa kiasi, lakini ukakaidi, ukawaona Watu hamnazo, ukasema kama ni Kufa kila MTU atakufa ukasahau kuwa vipo vifo vinavyokuja Kwa mateso makubwa, vipo vifo vinavyokuja polepole huku vikikukazia macho ya kikatili na kukudhalilisha, sasa una magonjwa hatari yasiyotibika yaliyotokana na ukaidi wako.
Usijilaumu tena. Umejifunza sasa Kwa Njia ngumu. Jisamehe na pengine nashukuru Mungu umekuwa mfano mzuri Kwa Watu wakaidi na watu watajifunza kupitia wewe. Na wale wakaidi watajifunza Kwa Njia ngumu.
Kila Mwanadamu anamakosa, lakini kukosea sio mwisho wa Maisha,
Nini chakufanya Baada ya kukosea kwenye Maisha;
1. Kubali na Kiri kuwa umekosea. Kisha Jisamehe
2. Wakati unajisamehe usijefikiri kuwa Watu watakusamehe isipokuwa watatumia Makosa yako kama fimbo ya kukuchapia sio wewe tuu Bali hata Watoto na kizazi chako
Mfano, Unaweza kuwa ulikuwa umekosea uchaguzi wa Maisha ukaamua kuwa Malaya na Mkaa Uchi labda ni Kutokana na ushamba au ulimbukeni au balehe tuu. Lakini baadaye ukaona umekosea ukabadilika na kuwa MTU Mwema.
Elewa kuwa wapo Watu ambao watakutambua Kwa zile tabia Mbaya zako, watakuita yaleyale majina ya tabia zako na hata Watoto wako watawatambua kama Watoto wa Malaya.
Elewa kuwa wanadamu wabaya hufurahia pale unapotenda mabaya, wanapenda kukuita Kwa majina mabaya, na hupendelea mabaya yakupate.
3. Kuwa ushuhuda Kwa Watu kuwa ulikuwa MTU Mbaya lakini sasa umebadilika na hautaki Watu wawe kama wewe. Usichukie Watu wakikuita Kwa majina mabaya ya mwanzoni. Hiyo itamaanisha bado wewe ni Mbaya. Vile wakuitavyo ndivyo ulivyokuwa, huyu wa sasa hawamtambui.
Kujisamehe ni kutafuta Amani yako ya moyoni. Wewe ndiye ulikosea na wewe ndiye madhara uliyeyapata Kwa 100% hivyo ni jukumu lako kujisahihisha.
Kujisamehe ni kuruhusu ukamilifu Kwa sababu ukamilifu unaletwa na Makosa yaliyosahihishwa. Na ili ujisahihishe ni lazima ukubali ulikosea, Ukiri na ujisahihishe.
Sio useme Mimi nilikosea mbona na wengine wanakosea. Huko ni kujipa Haki Wakati haustahili Haki. Haki ya MTU aliyekosea na kukubali Makosa yake, na Madhara ya aliyoyafanya, kisha kujisamehe.
Taikon anawasihi Vijana, Kipindi hiki ndio kipindi chenye Makosa mengi zaidi, hivyo ni muhimu kujisamehe zaidi ili kuepuka Depression.
Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam