Fbn
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 15,749
- 37,422
Samson alikuwa jirani yangu, tulisali kanisa moja. Wakati huo Nikiwa form one Samson alalishamaliza form six. Alikosa nafasi ya kujiunga na chuo hivyo ndugu zake walimsaidia kupata ajira Benk Kuu.
Enzi hizo nikikutana na Samson aliniuliza unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa? Nilimwambia mimi ninataka kuwa mtawa wa kanisa Katoliki. Siku moja alinikalisha akanieleza kama uifikirie dunia, hivi ni kweli uko tayari kuyatoa maisha yako hata mama yako akiugua ushidwe kumuuguza?
Samson alikuwa mcheshi na mpole, alinipenda sana lakini kwa tofauti ya umri wetu alichuja sana maneno ya kuniambia.
Nikiwa form three nilipata habari kuwa Samson alikunywa sumu na kujiua. Kisa kikiwa nafasi yake ya kwenda kusomeshwa na bank kupewa mtoto wa kigogo.
RIP Samson.
ulisemwa alibebwa akushindwa kubeba nafasi ya moyo wake