Zoezi hili ni gum kama hatutaiunga mkono serikali.
Arusha kuna kitu kinaitwa Culture heritage, kimejaza wahindi wanachonga vinyago vya kuuza kwa watalii na kusafirisha nje ya nje kibaya zaidi wanavidrill/ kupekecha na kutumia kusafirishia tanzanite kwenda india na kwingineko.
Wamakonde wasingeweza kuajiriwa?
Kuna madudu mengi ya wageni huku, wamejaa wakenya wanafanya kazi za hotel management,,,watz hawawezi?
Kuna wazungu wanajifanya wanajenga mahotel lakini tayari yanalaza watu na kutumia kama camp site, halipi chochote serikalini na wanawanyima wageni wenye hotel wanaolipa kodi.
Nashauri serikali ifungue web itakayotumika kupokea taarifa ya wageni haramu au namba za simu