Jipu la ulevi Rombo sasa kutumbuliwa

matubara

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
226
89
Kwa mwendo huu wa JPM hakuna shaka kuwa ulevi Rombo sasa unachungulia kaburi. Huku vijana hawachezi pool asubuhi bali wanaanza kunywa pombe asubuhi. Kila duka rombo ni LAZIMA kuwe na pombe hata kama ni duka la viatu au vitabu. Hakuna cha baa wala grosari kwani vijana wanabeba pombe za kwenye makaratasi almaarufu viroba mifukoni mwao. Watoto wa sekondari ndio usiseme. Dc wetu amepambana na ulevi ila naona amezidiwa.
 
Upo sahihi Mkuu, ulevi wa pombe ya viroba wilaya hiyo ya rombo hilo ni jipu Sugu.
 
Sasa kama watu wanabeba pombe za makaratasi unadhani huyo DC atawapatia wapi na umesema hamna bar?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom