Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 62,099
- 127,838
Habari za wakati huu.
Nianze kwa kusema binadamu tumeumbwa tofauti. Kila mtu ana vitu anavyovipenda na vitu asivyovipenda.
Inawezekana ana sababu za kijamii/kiafya/kiimani au bas tu amejikuta hapendi.
Mfano mimi nina rafiki yangu ukimuandikia sms kwa herufi kubwa hasomi, hata akijitahidi kusoma hakujibu, yaani ni kwamba anazichukia hakuna mfano.
Mimi binafsi sipendi muziki wa taarabu....yani sijui ni kwa nini yan sipendi hata kumsikia mtu anaimba karibu yangu.
Unapoingia kwenye mahusiano na mtu unaweza kugundua kuna vitu fulani mtu wako anavifanya wewe havikupendezi, jitahidi umwambie mapema kwamba vitu hivyo we hupendi.
Mfano kuna wanaume hawapendi wapenzi wao wavae suruali, wengine hawapendi simu na sms za usiku,wengine hawapendi pombe na kuna wanawake hawapendi baadhi ya mavazi na wasingependa wapenzi/waume zao wavae,kuna watu hawapendi baadhi ya vyakula...n.k
Usipomueleza huyu mtu mapema kuhusu vitu kama hivi japo ni vidogo sana inaweza kuleta shida baadae.
mfano mwanzoni mwa ndoa mkeo anakupikia vyakula fulani we huvipendi lakini we unajibalaguza unakula kwa kupenda hasa....hii sio sawa jitahidi kuwa wazi ili mjadili namna ya kufanya.
Usipoyasema mapema ukajitia kuvumilia.....sisi ni binadamu tunafika mahali uvumilivu unatuishia unajikuta unaanza kuonyesha hali halisi....mwenzio atahisi umemchoka au umepata mchepuko na unamtafutia visa kwa vitu ambavyo havikuwa vikikukera toka mwanzo wa mahusiano yenu...kumbe maskini ya Mungu ulikuwa unapata shida lakini unaogopa kusema kwa sababu utatibua penzi changa.
Tujitahidi kuwa wawazi.
Ni hayo tu nimejisikia kushea na ninyi leo hii. Na hii haiishii kwa wapenzi au ndoa tu. Inaapply kwa ndugu jamaa na marafiki pia.