Jionii baada ya ordination

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Baada ya chakula cha jioni Yesu akaenda matembezi. Andrew akaenda kumtafuta Yesu,na alipomuona akasema,''Bwana,ndugu zangu wanashindwa kuelewa kuhusu ufalme. Hatuoni kama tunao uwezo wa kuanza kazi mpaka utupe maagizo zaidi. Nimekuja kukuomba kuungana nasi katika bustani utusaidie kuelewa maana ya maneno yako.''
Alipofika katika bustani aliwakusanya mitume wake,kumzunguka na akawafundisha,akasema,''Mnapata taabu kuupokea ujumbe wangu kwa vile mnataka kujenga haya mafundisho mapya moja kwa moja juu ya yale ya zamani. Lazima muanze upya kama watoto wadogo na muwe tayari kuyaamini mafundisho yangu na kumuamini Mungu. Haya mafundisho mapya ya ufalme hayawezi kufanywa yalingane na yale ambayo yapo. Mna mawazo ambayo siyo sahihi kuhusu Mwana wa Mtu na kazi yake duniani. Lakini msifanye kosa la kufikiri kwamba nimekuja kuiweka kando sheria na manabii;sikuja kuiondoa isipokuwa kuitimiza,kuikuza na kuiangaza.Nimekuja siyo kuiondoa sheria,bali kuandika amri hizi mpya katika ubao wa mioyo yenu.
''Nataka kutoka kwenu haki ambayo itaishinda haki ya wale ambao wanatafuta kupendwa na Baba kwa zaka,sala na kufunga. Kama mnataka kuingia katika ufalme,lazima haki yenu iwe na upendo,huruma na kweli-mtake kwa dhati kufanya utashi wa Baba yangu aliye mbinguni.
Halafu Simon Peter akasema,''Bwana,kama una sheria mpya,tungependa kuisikia.Ifunue hiyo njia mpya kwetu.'' Yesu akamjibu Peter,''Mmesikia ikisemwa na wale wanaofundisha sheria'Usiue,yoyote anayeua anaweza kuhukumiwa',lakini mimi natazama mbele zaidi ya tendo kuifunua nia. Nasema kila anayemkasirikia ndugu yake yuko hatarini kutiwa hatiani. Yule mwenye chuki moyoni mwake,na anapanga mipango ya kisasi akilini mwake anaweza kuhukumiwa. Lazima muwahukumu wenzenu kwa matendo yao,lakini Baba wa mbinguni anahukumu kwa kufuata nia.Mmesikia waalimu wa sheria wanasema 'Usizini',lakini mimi nasema kila mwanaume anayemtazama mwanamke kwa ashiki ameshazini naye moyoni mwake. Ninyi mnaweza tu kuwahukumu watu kwa matendo yao,lakini Baba yangu anatazama katika mioyo ya watoto wake na kwa huruma anawahukumu kutokana na malengo yao na hamu zao.
Yesu alitaka kufundisha amri nyingine wakati James Zebedee alipomkatiza na kumuuliza,''Bwana,tuwafundishe nini watu kuhusu talaka? Tumruhusu mwanamke amtaliki mke wake kama Mose alivyoagiza?''Na Yesu aliposikia swali hili akasema,''Sikuja kutunga sheria[to legislate] ispokuwa kutoa mwangaza. Sikuja kurekebisha falme za dunia hii,bali kuanzisha ufalme wa mbinguni.Siyo utashi wa Baba yangu kwamba niingie katika kishawishi cha kufundisha sheria za serikali,biashara,au tabia za kijamii,ambazo ingawa zinaweza kufaa kwa leo,zikawa hazifai kwa jamii ya siku za baadaye. Nipo duniani kufariji akili tu,kuziokoa roho za watu. Lakini nitasema kuhusu hili swala la talaka,kwamba ingawa Mose aliafiki haya mambo,haikuwa hivyo katika siku za Adam au katika Bustani.
Baada ya mitume kuongea wao kwa wao kwa muda,Yesu akaendelea kusema,''Wakati wote lazima mtambue maoni ya aina mbili,ya tabia za kibinadamu,na ya kitakatifu,njia ya mwili na njia ya roho,makadirio ya mpito,na msimamo wa milele'' Na ingawa hawa kumi na mbili hawakuelewa yote aliyowafundisha,walisaidiwa sana na haya maagizo.
Halafu Yesu akasema,''Lakini mnaweza kukwama katika mafundisho yangu,kwa ajili ya tabia yenu ya kuupokea ujumbe wangu vile vile ulivyotamkwa. Lazima mkumbuke kwamba ninyi ni taarishi wangu,mnalazimika kuishi maisha yenu kama ambavyo mimi katika roho ninavyoishi maisha yangu. Ninyi ni wawakilishi wangu binafsi;lakini msifanye kosa la kutegemea watu wote wataishi kama ninyi kwa kila hali. Pia lazima mkumbuke kwamba wapo kondoo wengine ambao hawapo katika kundi hili,na mimi nawatafuta wao pia ili niwaonyeshe mfano wa kufanya utashi wa Mungu wakati wa kuishi maisha ya duniani.
''Halafu Nathaniel akauliza,''Bwana,tunatakiwa kuiacha hukumu?Sheria ya Mose inasema,'Jicho kwa jicho,na jino kwa jino. Sisi tuseme nini?' Na Yesu akajibu,''Mtalipiza wema kwa uovu. Taarishi wangu wasikinzane na watu,ila wawe wapole kwa wote. Kipimo kwa kipimo haitakuwa sheria yenu. Viongozi wa watu wanaweza kuwa na sheria hizo,lakini siyo hivyo katika ufalme. Na kama haya ni maneno magumu,hata sasa mnaweza kuondoka. Huruma wakati wote itawale hukumu zenu na upendo utawale mwenendo wenu. Kama mnafikiria masharti ya utume ni magumu,mnaweza kuirudia njia rahisi ya kuwa wafuasi.
Baada ya kuyasikia haya maneno ya kustusha,mitume wakaenda pembeni kujadiliana kwa muda,lakini wakarudi upesi,na Peter akasema,''Bwana,tunataka kwenda na wewe,hakuna hata mmoja wetu takayerudi nyuma. Tuko tayari kuilipa hiyo gharama zaidi itakayohitajika,tutakunywa kikombe,tunataka kuwa mitume,siyo wafuasi tu.''
Yesu aliposikia hivi akasema,'Muwe tayari, kwa hiyo,kuchukua majukumu yenu na kunifuata. Fanyeni matendo yenu mema kwa siri,mkitoa zaka,mkono wa kushoto usijue mkono wa kulia unafanya nini. Na mkisali,nendeni pembeni muwe peke yenu na msirudierudie maneno yasiyokuwa na maana. Kumbukeni wakati wote kwamba Baba anafahamu mnalohitaji hata kabla hamjamuomba. Na msiwe na tabia ya kufunga kwa sura ya huzuni kuonekana na watu. Kama mitume wangu niliowachagua,sasa mjiweke kando,kwa utumishi katika ufalme,kwa utumishi wenu wa kujitolea jiwekeeni utajiri mbinguni,kwa ajili utajiri wako ulipo,moyo wako utakuwepo hapo hapo.
''Taa ya mwili ni jicho;kwa hiyo,kama jicho lako lina ukarimu,mwili wako wote utajaa mwangaza. Lakini kama jicho lako lina uchoyo,mwili wote utajaa giza. Kama taa iliyoko ndani yako ikibadilika kuwa giza,giza hilo litakuwa kubwa sana!''
Halafu Thomas akamuuliza Yesu kama wanapaswa ''kuendelea kumiliki vitu kwa pamoja'' Bwana akasema,''Ndiyo,ndugu zangu,nataka muishi pamoja kama familia moja inayoelewana. Mmekabidhiwa kazi kubwa,na sitaki mchanganyikiwe. Mnajua imesemwa kwa usahihi,'Mtu hawezi kutumikia mabwana wawili. Hamwezi kumtumikia Mungu kwa nguvu zote,na wakati huo huo kuitumikia hela kwa nguvu zote.Kwa vile sasa mmejitoa kufanya kazi ya ufalme,msiwe na shaka kuhusu maisha yenu,au kuwa na shaka mtakula nini au kunywa,au kwa miili yenu mtavaa nini. Tayari mmeshajifunza kwamba mikono iliyo tayari na moyo wenye bidii havishindi njaa.Na sasa mnapojitayarisha kuutumikia ufalme kwa nguvu zenu zote,muwe na hakika kwamba Baba anayaelewa mahitaji yenu yote. Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu,na mkiupata mlango,vitu vyote mnavyohitaji mtaongezewa. Kwa hiyo msiwe na shaka kuhusu kesho. Matatizo ya siku moja yanatosha .
Yesu alipoona kwamba wapo tayari kukesha kuuliza maswali akawaambia,''Ndugu zangu,ninyi ni vyombo vya udongo,ni bora mpumzike ili muwe tayari kwa kazi ya kesho.'' Lakini usingizi ulikuwa umeondoka machoni mwao. Peter akamwomba Bwana'' kuongea nawe faragha siyo kwa vile nina siri nataka kuwaficha wengine isipokuwa kwa vile kuna mambo yanaisumbua roho yangu,na iwapo,itatokea,nikagombezwa,itakuwa rahisi zaidi kuvumilia nikiwa peke yangu,kuliko hapa mbele ya wote.'' Yesu akamwambia,''Njoo Peter,'' na kuongoza njia ndani ya nyumba. Peter aliporudi alikuwa amefurahi na pia amepata matumaini,,kwa hiyo James naye akaamua kwenda kuongea na Bwana. Hivyo hivyo,wote wakaenda mmoja baada ya mwingine kuongea na Bwana. Wote walikwenda isipokuwa wale mapacha amabo walikuwa wamelala.Andrew akasema,''Bwana,wale mapacha wamelala katika bustani,karibu na moto. Niwaamshe,niwaulize kama wanataka kuongea na wewe?'' Yesu akasema,''Wanafanya vyema,usiwasumbue.''
 
Please edit hii kazi ili iwe rahisi kusoma!
Weka paragraphs, na acha nafasi between paragraphs.
Tunapata shida kusoma. Otherwise it is a good thread, though sijajua imetoka injili gani!
 
Ni kitabu gani hiki unacho rejea wewe mwenzetu? Ni korani? Maana hii biblia sijapataiona. Au ni ufunuo wako utuambie.
 
Mkuu ubarikiwe kwa hii post, ila kama ungetutumbukizia hapa source ni kitabu gani tungeweza kuchangia kwa mtizamo sahihi. Ni vizuri zaidi kuitambua dhamira ya mwandishi kuliko kudhania.
 
halafu tafadhali useme pia ni toleo gani pia la biblia. kama kiswahili cha kisasa au...?
 
Back
Top Bottom