Jinsi ya kuzuia usiote ndoto za kishetani

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Watu wengi wanapolala huota ndoto. Baadhi ya ndoto ni za kawaida, nyingine zinatoka kwa Mungu, na nyingine hutokana na akili zetu wenyewe. Lakini pia zipo ndoto zinazotokana na shetani. Ndoto za kishetani huleta hofu, mateso na kumfanya mtu akate tamaa. Ndoto za kishetani hazifurahishi bali zinakera na kuumiza moyo. Hii hapa ni mifano ya ndoto za kishetani:
  • Kuota unakimbizwa na wanyama wakali kama nyoka, mbwa au simba.
  • Kuota unazama majini au unazuiliwa na nguvu za ajabu.
  • Kuota unafanya tendo la ndoa na mtu asiye mume au mke wako (ndoto za mapepo ya mahaba – incubus/succubus).
  • Kuota unaona mazishi, makaburi au watu waliokufa.
  • Kuota unapigwa, unachinjwa au kushikwa na nguvu zisizo za kawaida.
  • Kuota umefukuzwa shule au kazini bila sababu (ndoto za kurudishwa nyuma kimaendeleo).
  • Kuota unakula chakula kisichojulikana.
Ndoto za kishetani mara nyingi humuacha mtu akiwa na hofu, huzuni au kuchanganyikiwa anapoamka.

Hebu tujifunze sasa jinsi ya kuzizuia ndoto hizo za kishetani
(a) Hakikisha unaishi maisha matakatifu
Dhambi huwapa mapepo nafasi ya kuwaingia watu na kuwatesa ndotoni. Kwahiyo mtu anayeishi maisha ya ulevi, uasherati, chuki, uongo na dhambi nyingine kama hizo, anakuwa ameacha mlango wazi wa kushambuliwa na shetani na mapepo yake katika ndoto. Kwahiyo kama umekuwa ukiishi dhambini, ili uweze kuzuia ndoto za kishetani, tubu dhambi zako na uanze kuishi maisha ya utakatifu mbele za Mungu.

(b) Omba kabla ya kulala
Maombi ni silaha kubwa ya kiroho. Kabla hujalala, omba na kumkabidhi Mungu roho yako, akili yako na mwili wako. Omba damu ya Yesu ikufunike kwa imani unapolala.
Huu hapa mfano wa sala: “Ee Mungu ninalala sasa. Naomba unifunike kwa damu ya Yesu Kristo. Nazuia mapepo na nguvu za giza kuja kunisumbua ndotoni, kwa Jina la Yesu, amen.”

(c) Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku
Neno la Mungu ni nuru. Likiangazia akili yako, giza haliwezi kuendelea. Soma Zaburi, hasa Zaburi ya 91, 27, au 23 kabla ya kulala. Zaburi hizo zitakupa amani na kuzuia usiote ndoto mbaya.

(d) Imba nyimbo za sifa na kuabudu
Sifa za Mungu zinamfukuza shetani. Nyimbo za kumtukuza Mungu zikijaa ndani ya moyo wa mtu, hata katika ndoto atakuwa katika hali ya amani.

(e) Takasa mazingira unayolala
Mazingira unayolala yanaweza kukuletea usumbufu wa kiroho. Hivyo uwe makini na picha unazobandika ukutani, picha unazotazama kwenye mitandao, miziki na vitu vinavyovuta roho za giza nyumbani kwako. Omba na kutakasa chumba chako kwa jina la Yesu Kristo.

(f) Funga na kuomba
Ukiona ndoto za kishetani zinajirudia rudia, ongeza gia ya maombi - funga na kuomba. Maombi ya kufunga humfanya mwamini kuwa na nguvu za rohoni na kufunga milango yote ya giza.

Usizipuuze ndoto za kishetani. Ndoto hizo ni mojawapo ya mbinu za shetani za kukuletea hofu, kukurudisha nyuma kimaisha na kukutesa. Lakini kama tulivyoona, kwa jina la Yesu Kristo tunaweza kuzuia ndoto za kishetani. Tangu nilipozijua siri hizo za kuzuia kuota ndoto za kishetani, nimekuwa nikiota ndoto za mafanikio, sherehe na ushindi.

Ukiyazingatia hayo, hutababaishwa tena na ndoto mbaya unapolala, bali utakuwa ukiota ndoto za amani, furaha na baraka kutoka kwa Mungu. Ulale unono usiku wa leo, katika Jina la Yesu, amen.
 
Umefafanua vizuri, ila nina swali...
 
Yeah, ila sikumbuki sana content
Sawa. Ngoja basi nikukumbushe kwa ufupi maudhui ya kitabu cha Ayubu. Kwa sehemu kubwa kitabu hicho kinasimulia jinsi shetani alivyoruhusiwa kumtesa Ayubu kwa majaribu mbalimbali. Ayubu aliugua magonjwa mazito; akapoteza watoto wake, na hata mke wake alitumiwa na shetani kumkatisha tamaa Ayubu.

Sasa katika sura ya 7:13–14, sikia jinsi Ayubu anavyolalamika akisema: “Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituliza moyo, malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu; ndipo unitishapo kwa ndoto, na kunitia hofu kwa maono; hata nafsi yangu huchagua kunyongwa, na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya. Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.”

Hapo tunaona wazi kuwa hata usiku, Ayubu alipokuwa amelala, aliteseka kwa ndoto za vitisho na maono yanayoleta hofu. Sasa kwa kuwa Maandiko yanatuonyesha kwamba majaribu yote ya Ayubu yaliletwa na shetani kwa ruhusa ya Mungu (Ayubu 1:12, 2:6), basi ni wazi pia kwamba hizo ndoto za hofu zilitoka kwa shetani.

Ndoto alizoota Ayubu usiku hazikuwa ndoto za faraja kutoka kwa Mungu. Alipolala alitarajia kuugua kwake kungepungua, lakini ikawa kinyume kiasi cha kutamani kunyongwa na kufa! Hivyo ndivyo shetani anavyowafanyia watu wengi ndotoni.

Naamini umeelewa sasa jinsi nilivyojua kwamba ile list ni mifano ya ndoto zinazotoka kwa shetani. Nimejifunza kutoka katika kitabu cha Ayubu; kitabu chenye ushahidi au mfano mzuri wa ndoto za kishetani. Vilevile kwa kusikiliza shuhuda za watu waliokuwa na mapepo, nimejifunza pia jinsi shetani anavyoweza kuwaletea ndoto mbaya watu aliowateka. Kuna binti mmoja yeye alikuwa anaota mtu anamuijia na kisu na kutaka kumchinja. Mapepo aliyokuwa nayo yalipokemewa na kutoka, akawa huru mbali na ndoto hizo za hofu. Umenipata, mkuu?
 
Sawa. Ngoja basi nikukumbushe kwa ufupi maudhui ya kitabu cha Ayubu. Kwa sehemu kubwa kitabu hicho kinasimulia jinsi shetani alivyoruhusiwa kumtesa Ayubu kwa majaribu mbalimbali. Ayubu aliugua magonjwa mazito; akapoteza watoto wake, na hata mke wake alitumiwa na shetani kumkatisha tamaa Ayubu.

Sasa katika sura ya 7:13–14, sikia jinsi Ayubu anavyolalamika akisema: “Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituliza moyo, malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu; ndipo unitishapo kwa ndoto, na kunitia hofu kwa maono; hata nafsi yangu huchagua kunyongwa, na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya. Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.”

Hapo tunaona wazi kuwa hata usiku, Ayubu alipokuwa amelala, aliteseka kwa ndoto za vitisho na maono yanayoleta hofu. Sasa kwa kuwa Maandiko yanatuonyesha kwamba majaribu yote ya Ayubu yaliletwa na shetani kwa ruhusa ya Mungu (Ayubu 1:12, 2:6), basi ni wazi pia kwamba hizo ndoto za hofu zilitoka kwa shetani.

Ndoto alizoota Ayubu usiku hazikuwa ndoto za faraja kutoka kwa Mungu. Alipolala alitarajia kuugua kwake kungepungua, lakini ikawa kinyume kiasi cha kutamani kunyongwa na kufa! Hivyo ndivyo shetani anavyowafanyia watu wengi ndotoni.

Naamini umeelewa sasa jinsi nilivyojua kwamba ile list ni mifano ya ndoto zinazotoka kwa shetani. Nimejifunza kutoka katika kitabu cha Ayubu; kitabu chenye ushahidi au mfano mzuri wa ndoto za kishetani. Umenipata, mkuu?

Kwa hiyo ndoto zote ni maono ya Mungu? Tuanziie hapo
 
Inaonekana hujasoma paragraph ya kwanza ya mada yangu. Nimesema hivi: "Watu wengi wanapolala huota ndoto. Baadhi ya ndoto ni za kawaida, nyingine zinatoka kwa Mungu, na nyingine hutokana na akili zetu wenyewe. Lakini pia zipo ndoto zinazotokana na shetani. Ndoto za kishetani huleta hofu, mateso na kumfanya mtu akate tamaa. Ndoto za kishetani hazifurahishi bali zinakera na kuumiza moyo..."
 
Wauliza maswali wengi wao hua aidha
1. Sio wakristo
2. Hawasomi biblia
3. Atheists
4. Dark magics believers.

Mimi nimesoma rasha rash tu ila nimekuelewa and yes hata mimi niliwahi fundishwa hivyo na matokeo mazuri nikayaona lakini shida ya walio wengi waliozaliwa kwenye neema ya wokovu hua hawatilii maanani mambo kama hayo na wanaisha kukejeli na kudhihaki.

NB: Fellas GOD CAN NOT BE MOCKED.
 
We dada si uliagaga humu. ? Au sio wewe.? Usiku wote huu tuanze kuwaza ndoto tutakazoota jamani?. Khaah!..
 
Wauliza maswali wengi wao hua aidha
1. Sio wakristo
2. Hawasomi biblia
3. Atheists
4. Dark magics believers.

Mimi nimesoma rasha rash tu ila nimekuelewa and yes hata mimi niliwahi fundishwa hivyo na matokeo mazuri nikayaona lakini shida ya walio wengi waliozaliwa kwenye neema ya wokovu hua hawatilii maanani mambo kama hayo na wanaisha kukejeli na kudhihaki.

NB: Fellas GOD CAN NOT BE MOCKED.
Asante kwa kuchangia mada na kwa ushuhuda mzuri. Ubarikiwe sana
 
Ni kweli nimeota ndoto mpaka nazikwa.
Na sasa ndoto za kula usiku zinasumbua sana, nakutana mahali nawajua watu tunakula usiku kucha, nyama, samaki kila kitu.
Naamka nimeshiba Mbaya.
Hapo sina njaa tena siku 4-5.
Mungu saidia Kwa kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom