Kuoneshana upendo na kuishi kwa mapenzi
Hata kama utakuwa unampenda mwandani wako kiasi gani, iwapo hutalionesha pendo lako, mwenzio hatahisi kama unampenda. Hata kama unafurahishwa vipi na mwandani wako, kama huoneshi kufurahishwa, yeye hatahisi kama anafurahiwa.
Hakuna mume wala mke mkamilifu lakini wandani wanapooneshana mapenzi na furaha na kuishi kwa kufuata misingi ya Uislamu, siyo tu watapendana kwa mapenzi na heshima bali pia watapendwa na Allaah.
Magusano ya ziada huongeza zaidi uhusiano wenu wa ndoa na kukoleza huba ya kumfanya mwenza aongeze jitihada za kukuridhisha.
Aidha zawadi ndogo ndogo ambazo zinaonesha jinsi unavyomjali hizi ni chachu za pendo, na zinasambaza mawimbi ya mapenzi mwilini mwa kila mmoja.
Vilevile kula na kusali pamoja kwaimarisha mahusiano ya wanandoa. Usipuuze umuhimu wa chakula cha pamoja cha familia. Sufiyan ath-Thawri kasema; Nimesikia kuwa MwenyeziMungu na Malaika Wake huipa baraka familia inayokula pamoja.
Ni jambo la kupendeza kusali nyuma ya kiongozi wa familia na kufanya naye ibada pamoja. Hata hivyo mume-Imamu lazima azingatie mafundisho ya Mtume mwenyewe ambaye aliifanya swala ikidhi mahitaji na shida za jamaa iliyokuwa nyuma yake.
Mimi husimama kuswali kwa kisimamo kirefu lakini punde ninaposikia kilio cha mtoto naifupisha swala kwa kuchelea kuwa mama yake anaweza kudhikika. (Bukhari na Muslim).
Mbali na hayo, mambo mengine madogo sana kama haya yanaweza kukuleteeni kheri. Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kasema, hata kumlisha mkeo tonge la chakula mdomoni ni swadaka (Bukhari na Muslim).
Hii inaonesha aina ya ukarimu unaotakiwa kuwepo katika ndoa ya Muislam