Jinsi ya kuwa romantic

Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
3,422
Reaction score
5,597
Habari wana JF,

Kwa wale wataalamu wa hizi mambo,hivi ni mambo gani ambayo inabidi umfanyie mpenzi wako ili uweze kuwa romantic patner kwa jinsia zote.Kuna jamaa mmoja juzi kati alipigwa chini na moja ya binamu zangu baada ya kusemekana hayupo romantic,wamezaa mtoto mmoja na jamaa alishatoa mahari mwaka mmoja uliopita ila akawa anachelea kufunga harusi huku wakiishi mikoa tofauti na kuonana mara chache.Jamaa lecturer yuko mzumbe mbeya huku binamu yuko T.R.A HQ.

Kwa dondoo fupi,mchizi alikuwa akija DAR analeta vyakula tu na kujishughulisha zaidi na mambo ya kusahihisha test na kusoma research za wanafunzi wake huku akiwa less concerned na binamu+mtoto hali iliopelekea kushutumiwa kuwa ni less romantic na hatimaye kupigwa chini ghafla bin vuu.Jamaa amepagawa juu ya mkasa uliotokea ila hamna namna tena zaidi ya kugombania mtoto.

Swali:
Kwa wadada,je tunatakiwa tufanye mambo gani ili tuepukane na mkasa kama uliomkuta huyu jamaa hapo juu?

Kwa kaka zangu mliofanikiwa katika mahusiano pia ni mbinu zipi mzitumiazo kumfanya shemeji aone mpo romantic zaidi?
 
We kuwa na mapesa tu uone kama hautakua romantic.
 
Mupya ishapatikana hapo ghafla jamaa akaonekana sio romantic
 
Mupya ishapatikana hapo ghafla jamaa akaonekana sio romantic

Hata mimi nimehisi hivyo!

Ingawa kuna watu bana ni 'workaholics' mbaya! Yani yeye kila wakati anawaza kazi tu..especially Lecturers sijui kwa nini!

Anyway, jinsi ya kuwa romantic ni kujali hisia za mwenzio na kumfanyia kila kile upendacho kufanyiwa.

Lingine, ni kuwa wewe (being you) tangu mnapoonana...hii itasaidia kuepuka kujiundia picha tofauti na uhalisia!!!
 
Jamaa yako kashindwa kuthamini uwepo wa mwenzie, jamaa alikuepo kimwili tu akili ipo kwenye test na research zake, kazi ni muhimu but alitakiwa atumie muda kidunchu kuconcentrate na mbebs, then amuombe kuendelea na kazi inakua poa make kaonesha kuthamini ila tu kazi zimebana.
 
Nchi ikiwa na maendeleo automatically watu wake wanakua romantic stress za kimaisha pia hupelekea mtu kuwa harsh...

CHAGUA LOWASSA
VIVA UKAWA!!!

very correct labda nikazie Nyie wawili mkiwa na maendeleo no stress ndogondogo hata mapenzi yananoga
 
Meanwhile, Jaheim explained it better. Put that woman first.

​
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, kwa hiyo mtu akitekeleza kwa vitendo kauli mbiu "Hapa Kazi Tu" matokeo yake sio mazuri kwenye mambo ya mahusiano !!
 
lowassa atafanya kila kitu kuwa romantic
 
Mwanaume akiwa rich atakua romantic tuuu no way out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…