East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,209
Mkuu siku hizi upo wa kununua na hata ukitaka kwa jumla au rejareja unapata Pesa yako 2.
Uchawi hauuzwi ila waweza nunua majini yale yasiyokuwa na makao ambayo wenyewe waliokuwa wakiyamiliki walikufa wakakosa wa kuwarithisha au hawayataki tena n.k.Tunaita majini zururaji au majini koko.Ambayo hayana makao yanaishi kwenye miti,mabarabarani.makaburini n.k
kuna madalali wayatafutiayo pa kukaa ndio hao waitwao wauza uchawi.Wanachouza ni majini sio uchawi.Tatizo la hayo majini ni kuwa yamezoea kuishi hovyo mitaani yana tabia tukutu kama wale watoto wa mitaani waliokulia majalani.Ni mababe sana yaweza mara taka mtoto kumla, mara hili mara lile.Haya waweza nunua.Tahadhari ni kuwa yana masharti mengi wengi huwa yanawaliza baadaye na namna ya kuachana nao unakuta hawajui wanaishia tu kwenda kwenye vilinge kupungwa mashetani.
Narudia tena uchawi hauuzwi sokoni mtu anapewa.Ukikuta muuzaji ujue anauza majini.