Jinsi ya kuwa maskin milele

Punnisher

JF-Expert Member
Jul 28, 2014
1,169
1,376
1. Kamwe usiamke mapema, endelea kulala na kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.
2. Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako, wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha kaa chini na jifikirie umezitumiaje.
3. Kamwe usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave vipi pesa zako wakati unazo kidogo? Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema katika matumizi yako.
4. Kamwe usijiingize katika biashara ambazo huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na kiyoyozi.
5. Kamwe usifikiri kuanzisha biashara mpaka pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni kukuletea mtaji wa kuanzia biashara. Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama kina bakheresa walianza kuuza mgahawa, wewe ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika biashara zako.
6. Lalamika kuhusu kila kitu, isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na attitude yako. Ilaumu serikali ya Magufuli, zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha, zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya hawataki kukufanya uwe tajiri!
7. Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata. Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki nunua Verossa, watoto wa mjini wakukome.
8. Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua sumsung galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita halaf ongezea hela ukanunue sumsung galaxy S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu bhana.
8. Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari ya mtumba ambayo gharama zake za kulihudumia ni mara mbili ya mshahara unaoupata, au gari linalokaa muda mrefu gereji kuliko barabarani.
9. Wape wanao kila wanachokitaka kwa kuwa wewe ni mzazi bora, hawatakiwi kuhangaika wala kufundishwa utu na thamani ya pesa, usiwafundishe juu ya kutunza na kuheshimu fedha. Usiwafuatilie kabisa katika masomo yao.
Waache wakue wakiwa wavivu na waje kuwa masikini kuhakikisha kuwa hawawezi kukusaidia pale utakapozeeka.
10. Tembelea viwanja vyote vya bata, na uzuri wamiliki wa maeneo ya starehe wanatujali yaani wanafungua maeneo mapya kila siku, tembelea yote. Kula bata kula bata.
Na ukishakuhakikisha kwamba unatekeleza hayo yote, kaa chini na utafakari kuwa siku zote fainali nzuri huchezwa uzeeni!
Ponda raha kufa kwaja!
I DO NOT CARE!
 
Badilisha sigara mkuu, hii haikufai
 
ww acha nadharia zako zisizo na kichwa wala miguu.unaweza ukafanya yote yanayotakiwa kwa mtu kuwa tajiru na usiwe tajiri.asilimia 99 ya utajiri wa watu ni urithi kutoka kwa wazazi wao na asilimia 1 ni ubunifu na ugundunzi
 
Sasa Mkuu hao wazazi wao walipata wapi utajiri???
 
Usikubali kuajiriwa kwa mshahara mdogo.u dont work cheap ingawa we ni std7.jipendekeze kw matajir n wenye nazo ule bata tu na utese na magar yao kuwa mdudu wa taa kwa matajir kuwataftia madem n hakikisha unalala late night saa 10am afu unaamka saa 9 jion unamuuliza maza msos huku unapekua mahotpot ukishakula muombe mama ela ya sigara thn anza kupiga simu watu wa bata wako wapi.pia kumbuka ukipata ela usifanye kaz yyte ht ikitokea hakikisha pesa imeisha hd umeeka simu bondi bar ndo utoke ukatafute zingine.raha za dunia
 
Back
Top Bottom