Jinsi ya kuvunja urafiki bila UADUI

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
10,433
13,415
Kwenye maisha unapata marafiki mbalimbali wanaokupa experience nyingine, mashauri, upendo na hata msaada kiuchumi. Marafiki huwa ni zawadi toka kwa muumba ndo maana huwezi pata rafiki kwa kumnunulia bia lazima muwe na natural meet of mind.

Lakini jambo moja hatulijui, ni Je marafiki huja kufanya nini maishani? Marafiki hawaji hivi hivi huwa kuna msaada kwake au kwako na mara nyingi si wakipesa kukuvusha kwenye daraja kwenda safari yako, usipojua sasa kazi yake imeisha (kukusindikiza), unaweza jikuta unajenga awe adui yako MKUBWA kuliko unavyodhani.

Biblia yasema
Mithali. 18:24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Hapa inakuonya usiwe na marafiki wengi maana hao wakiamua kugeuka maadui zako hakika utaanguka .

JINSI YA KUWAPUNGUZA
- Usiwe mwepesi kuadmit kila mtu kuwa rafiki yako

- Tafakari Je marafiki ulionao wanaendana na lengo lako kuu kwenye maisha, unakunywa pombe na una ndoto ya kumiliki club kubwa nyingi halafu rafiki yako ni mlokole aliefungua kanisa lake, its ovious mnapita njia tofauti mshort list.

- Punguza mawasiliano Taratibu kama mnaongea mara 5 akipiga kuwa busy pokea moja tena ongea machache kwa kifupi ukipunguza ucheshi

- Usimpotezee kabisa unaweza mpigia kumsalimia halafu huongezi kitu cha maana.

- Kimbia hobby mnazoshare. Kama anapenda baa na we unapenda hama baa au kunywa mbali mfano mnakulaga monde Sinza nenda makumbusho akikuuliza sema niko Kigamboni kibada haji !

- Usimuelezee mafanikio yako ,msimulie failure tuu

UZOEFU
Kuna rafiki 2012 Alikuwa supervisor wangu Job, kuna siku alimtongoza demu wangu ambae anamjua mimi nkafanya upuuzi nkamfata nkammaindi na kumuonesha ushahidi plus kumtamkia navunja urafiki, asee jamaa alinisumbua kazini balaa nkawa namweleza tumevunja urafiki sijasema tunachukiana au maadui hakuwa anaelewa alivuruga ndoto zangu kwa kampuni ile kwa kuniongelea ovyo vikao vya management nkawa naambiwa.

Tangu hapo hii ndo mbinu yangu nikihakiki unakosa ambalo naona hufai kuwa rafiki nahakikisha hujui ni nini kimechange na sasa imeshadelete marafiki kibao ila wakinikuta kwenye shida wanansaidia kwa moyo, huenda ningempiga hii mbinu mshikaji leo ningekuwa CEO nchi za watu.

Poleni kwa maandishi mengi.
 
Ndio maana nina rafiki 1 tu toka tulipokua darasa la 4. Na tumetengena kwa miaka 2 hii.. For now sina rafiki n not searching.
Heri kuwa peke yako,Mi baba yangu alikuwa ana majamaa skuwahi muona na rafiki lakin nimekuwa nimeelewa
 
Kuna mmoja nilimchukulia kama ndugu yangu, kwakweli alikuwa anapitia mengi magu my. Kila Ijumaa alikuja kwangu tulikwenda mpaka J2.

Tatizo ni kama tulikuwa na mashindano, kila alichoniona nacho na yeye alinunua. Nilijua ni mambo ya kike.

Kumbe alikuwa anaongea kila kunachotokea kwangu. Kuna mtu aliniambia ni kama ninaishi nae alivyonijua nje ndani.

Sikumuuliza chochote yule dada, akipiga simu sipokei, alikwenda kuomba watu watukalishe kikao tupatanishwe lakini kwakweli moyo wangu ulishasema basi.
 
Sasa huyo snich ulikosea akipiga hupokei 3 unapokea moja afu unakuwa sio mcheshi kabisaaa ,anatakiwa sijue umempotezea nn akisema anakuja ijumaa unampiga kalenda ukimpiga 4 anajiongeza ,ila hawi adui yako anabaki kusema yuko strange
 
Niliyafanya taratibu sana, kwanza barua zake zilikuwa zinapitia kwangu, nilimuomba abadili anuani.
 
Niliyafanya taratibu sana, kwanza barua zake zilikuwa zinapitia kwangu, nilimuomba abadili anuani.
Hapo nimekusoma ,wanaweza kukujudge unaroho mbaya ooh umsamehe,nawezaisaidia nyoka kutoiua niirudishe polini sio kuishinayo.
 
Nope i have been hurt na so called friends . i have very soft spot in my heart . na nilikuwa mtu wa watu sana naona haifai tena coz nabak kuumia mm tu , life is unfair hakuna haja ya kuforce vitu .
Somo la life skills lilikupita kushoto.
 
Nope i have been hurt na so called friends . i have very soft spot in my heart . na nilikuwa mtu wa watu sana naona haifai tena coz nabak kuumia mm tu , life is unfair hakuna haja ya kuforce vitu .
That's the way it is!....tho few people are lucky to have loyal friends & family
Capture%2B_2019-08-28-17-50-17-1.jpeg
 
Back
Top Bottom