Jinsi ya kuunganisha simcard na akaunti CRDB

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
Nimejaribu kuunga laini yangu ya airtel lakini nikifika kwenye kuingiza tarehe inasema "umekosea kuingiza tarehe." Nimeshindwa kuelewa format ipi nitumie. Kadi imeandikwa 05/14. Msaada tafadhali.
 
Ingiza namba bila kuweka alama yyte katikati. Mfano tarehe ya ukomo wa kadi ni 02.10.2016 ww utaingiza 02102016
 
Mie nimekwamia kwenye passwd naingiza old pswd kisha new kisha na thibitisha lakini majibu inakua nimekosea.
 
hii kitu mpaka mimi nimechoka nimejaribu sana mwisho wa siku naambiwa REQUEST NOT CONFIRMED.
 
Samahani kwa kudandia hoja ya mwenzangu, mimi naomba mwenye kufahamu namna ya kujiondoa kwenye huduma hiyo anielekeze tafadhali.
 
Samahani kwa kudandia hoja ya mwenzangu, mimi naomba mwenye kufahamu namna ya kujiondoa kwenye huduma hiyo anielekeze tafadhali.

nadhani mpaka uwaone crdb wenyewe,maana kuna fomu maalum ambayo ulijaza pale benki ambayo kupitia maelezo hayo ya kwenye fomu ndiyo ukawezeshwa kujiunga ikiwa ni pamoja na kutumiwa sms toka kwao.mkuu wewe waone tu.
 
Ndugu watz wenzangu hapa jf, samahani sana, nami nina tatizo kuhusiana na hawa crdb, nilijaza form yao toka tarehe 25/06 kama sijakosea lakin bado hawaja ni enable online, hivi ni bofya *150*03# naambiwa 'tafadhali wasiliana na tawi lililo karibu kuweka record zako sahihi. Kinacho nipa utata ni kama mwezi unaisha toka niifungue hiyo akaunti, naomba unijuze ni nini kikwazo tafadhali. Naomba kujua pia ni benk nyingine zipi zinatoa huduma hiyo bila usumbufu. Asanteni
 
Back
Top Bottom