Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Wakuu habari ya leo. Nina imani afya zenu Ni njema kabisa. Mimi si mwanachama hai wa jukwaa hili, lakini leo nimeona nitoe mchango wangu kama njia ya kuboresha mahusiano.
Kuna tabia ambazo kwa namna moja ama nyingine zinachangia sana kuua mapenzi kati ya mke na mume. Sababu kubwa Ni kuwa ghafla mume humwona mkewe kama mgeni moyoni mwake. Baadhi ya tabia hizo zinaweza zisiwe za ajabu sana, lakini zina madhara makubwa moyoni mwa mume.
1. Kumlinganisha mumeo na mwanamume mwingine. Mfano unamwambia mbona wewe hauko kama flani? Usidhani itampa motivation. Badala yake utamfanya ajione hatoshi kuwa mwanamume. Kumbuka kuwa mumeo Ni yule yule ambaye ulimjua kabla hajakuoa.
Mara nyingi tamaa ya kuolewa huhadaa ufahamu, kiasi cha kutia upofu usiweze kuona udhaifu wa mwenzi wako. Hii hupelekea watu kuoana pasipo kujua kama kweli wanafanana. Kumbuka ndoa si kufaana bali Ni kufanana.
Unapomlinganisha mwanamume na mwanamume mwingine unaufunga moyo wake kwako. Moyoni atakuwa akiwaza, kwa nini basi kuolewa na mimi? Ina maana amemwona yule mwanamume kuwa bora kuliko mimi!!?
2. Kumtazama kwa dharau. Baadhi ya wanawake siku hizi wamekuwa na tabia ya kumtazama mwanamume kwa dharau, kunyonga midomo, kumtazama juu mpaka chini kwa dharau. Kitendo hiki unaufunga moyo wa mumeo. Ni kama kumwonyesha kuwa hana thamani tena kwako.
Kabla hajakuoa ulikuwa mwepesi wa kuomba msamaha hata pale anapokosea! Yes, anapokosea yeye, ulimweleza kwa lugha ya upole akakukasirikia, ukamwomba akusamehe. Lakini baada ya muda akarudi kukiri kwamba ni kweli ulichomwambia. Mwishowe mshindi ukawa ni wewe mwanamke. Sasa baada ya kuolewa unataka kila unachotamka kifuatwe kwa utii.
Umesahau msingi ulioujenga wakati wa uchumba. Mume anakuona kuwa mgeni kwake, si yule waliyerekebishana kwa upole, kwa nafasi. Asilimia kubwa ya wanaume hawawezi kukiri makosa moja kwa moja. Pia Pia mnapopishana mitazamo anatarajia mwanamke ajishushe, Kisha yeye atakuwa anafanyia marejeo hoja zake. Badala yake mke anamtazama mume kwa dharau, anampima chini mpaka juu. Hii inaujeruhi moyo wa mwanamume.
3. Kumwonyesha kuwa humhitaji sana kwenye maisha yako. Kabla ya kuolewa ulikuwa ukilia na kusaga meno kutaka uolewe. Baada ya kuolewa unaanza kumfanyia dharau mumeo, ukidai kwa Mfano, hukufukuzwa kwenu na kwamba asikubabaishe. Kila mkipishana kidogo tu, unajidai kumwonyesha kuwa hakuna jipya unalopata kwake.
Je, Ulipata kujiuliza Kabla ya kuolewa, ni kitu gani hasa unachohitaji kwake ambacho huna? Sio kwa habari ya sex tu. Je, ni nini ambacho ungependa akupe ili ujione umekamilika kuwa mwanamke? Au ndio ndoa za fasheni? Mfanye mume wako ajione mwanamume, hakika utauteka moyo wake.
4. Kubadili mfumo wa maisha. Kabla hajakuoa ulikuwa ukivaa mavazi fulani na kujipamba kwa namna fulani. Ni kwa mwonekano huu mumeo alijikuta ametekwa bakunja! Akanasa kwenye mtego, asione mwingine zaidi yako. Sasa baada ya kuolewa, unadhani umemaliza jukumu. Ghafla ukabadili utaratibu wa kujipamba.
Sasa tena hujipambi ili kumfurahisha mumeo, bali unajipambamba kuwafurahisha wanaokutazama huko barabarani. Ghafla mumeo hamwoni tena yule aliyekuwa akiichanganya akili yake. Anabaki kujishangaa ilikuwaje akakuoa wewe? Anahisi labda kuna uchawi ulitumika. Mumeo alikupenda ukiwa hujichubui, huweki makeup, yeye alipenda kukuona uko simple tu.
Baada ya kuolewa unaanza kukimbizana na wanawake wengine mtaani. Hakika utawavutia wakware wengine, lakini mumeo hatokuwa na furaha na wewe. Huishi tena kwa ajili ya mumeo, bali unatafuta sifa kwa mapapa wa mtaani. Hapo lazima utajiweka majaribuni na hakika utahatarisha ndoa yako.
5. Mawasiliano na wapenzi wako wa zamani. Hili nalo Ni jambo ambalo litamfanya mumeo asiwe na imani na wewe asilani. Kabla ya kuolewa uliua mawasiliano yote na wanaume wako wa kale, baada ya kuwekwa ndani ukaanza kufufua mahusiano. Jiulize, kama hao unaowasiliana nao, ambao huenda walioa kabla hata hujachumbiwa, wamekuwa wanakupenda hivyo, kwa nini walichagua wanawake wengine badala yako?
Ungetarajia wakuoe wewe basi! Walikuchezea, ulipofika wakati wa kuoa, wakaachana na wewe, wakaenda kutafuta wanawake ambao wangewafaa kuwa wake wa ndoa. Sasa wewe umeolewa unaendelea kuwa kipozeo kwao. Muheshimu mumeo aliyekutoa kwenu akakujengea heshima mbele ya jamii.
Hakuna mwanamume atakaye vumilia urafiki wa mkewe na mwanamume mwingine. Usijiweke kuwa easy target. Utakapoachika, hao hao wanaokudanganya watakaa mbali nawe kwa kukwepa aibu ya jamii. Mheshimu mumeo, mtunzie heshima yake kwa kuzuia tamaa. Ndicho kiapo cha ndoa.
6. Marafiki. Mke mwema hawezi kuwa na wanawake marafiki mashangingi, wasio na maadili ya familia. Kabla ya kuolewa ulijipambanua kama mwanamke mwenye hekima na ujuzi wa kuchagua marafiki. Baada ya kuolewa unaanzisha urafiki na wanawake wasio na mwelekeo. Hakika utatekwa na Ujinga wao. Lazima utafanya kile wanachokifanya wao.
7. Kujidanganya kuwa utambadili tabia. Wako baadhi ya wanawake kutokana na kiu ya kutaka kuolewa, watadharau mapungufu makubwa ya wachumba wao wakijidanganya kuwa watawarekebisha wakiingia ndani. Sio kweli hata kidogo. Hivi umewahi kujiuliza Ni katika umri gani mtoto anahesabika kushindikana kwa wazazi wake?
Maana yake huyo hawezi tena kubadilika kwa njia za kawaida. Sasa wewe ujitwike zigo la kumbadili tabia mtu mzima!! Ukweli ni kwamba yeye ndiye atakubadili wewe. Kama ulikuwa na tabia njema utajikuta umebadilika ili kuendana na hali. Hayupo mwanandoa anayeweza kumbadili mwenzake.
Zaidi unachoweza kufanya ni kumsaidia awe akijificha usigundue. Kwa hiyo unapochukua maamuzi ya kuolewa, pima tabia ya mwenza wako, kama unaona utaweza kuishi naye kwa Jinsi alivyo bila kuumia moyo, basi huko ndiko kuchukuliana mizigo. Huyo ni wako.
8. Haki sawa katika ndoa. Hii ni mada ngumu zaidi kiasi kwamba inahitaji kujitegemea kwenye thread. Ni ukweli usiopingika kuwa hili limekuwa jinamizi linalozalisha migogoro ya ndoa kila uchao. Wanawake wengine wamegeuka wanaharakati ndani ya ndoa zao. Nitaliongelea kwa urefu baadaye kidogo..........
10. Mara kwa mara kuongelea wanaume wengine. Wewe ni mke wa ndoa, halafu kila uwapo na mumeo maongezi yako ni kuhusu sifa fulani fulani za mwanamume mwingine. Mfano unafanya kazi ofisi fulani, basi kila mara unamzungumzia mfanyakazi mwenzio wa kiume, Jinsi anavyojituma, anavyovaa, ucheshi wake, alivyimchangamfu. Maongezi Kama haya utamfanya mumeo ajione hatoshi kwako na hatokuwa na furaha nawe.
11. Kugombea madaraka. Dunia ya sasa imeleta mapinduzi makubwa kwenye mahusiano. Ile family structure iliyozoeleka kwa kiasi kikubwa inafutika. Ni vema basi mwanamke ukajiuliza Unataka nini kwenye ndoa. Kama Unataka Mumeo akuthamini Kama mke, simama kwenye nafasi yako. Kitendo cha kuleta uanaharakati kwenye ndoa kitakupatia matokeo hasi. Kiasili mwanamume ameumbwa kiongozi wa familia, ndio maana anatoa mahari na kuoa. Mwanamke naye ameumbwa kuhitaji ulinzi wa mwanamume, yeye Ni msaidizi. Mpe mumeo nafasi ya kuongoza familia, ili uushinde moyo wake.
12. Mara zote kuangalia mapungufu kuliko Yale anayotimiza. Kama mke, ni muhimu kutambua kuwa mumeo Ni binadamu. Kuna majukumu atayatimiza, na mengine atashindwa kuyatimiza. Ni jambo LA kutia hamasa kwa mwanamume pale mke anapozingatia zaidi yale yaliyotimizwa na kuyasifia. Hii itamfanya mume apate nguvu ya kutimiza hata yale yaliyomuwia ugumu. Muoneshe imani yako kwake kuliko kukosoa tu yale yanayokosekana.
13. Mipasho. Wakaapo wawili kupishana kimtazamo lazima kutatokea. Ni Jinsi gani unalichukulia hili kunaweza kuathiri uhai wa ndoa yako. Kwa sababu ya ugomvi uliotokea, unakuta mwanamke anamwekea mumewe wimbo wa mipasho na huku akiuimba kwa kejeli. Hii inazidi kuongeza uchungu moyoni mwa mwanamume. Mfano unaweka wimbo wenye maneno kama "mume bwege, ukisusa wenzako wanakula, ukiona vya nini wenzio wanajiuliza watavipata lini" n.k. Hakika haya hayakusaidii lolote zaidi ya kuua moyo wa mumeo. Imetokea ambapo mke alikuwa anapika jikoni, mume kaketi sebuleni anaangalia TV. Ghafla ukanapigwa wimbo MWANAMUME MASHINE. Mke alitoka spidi jikoni kuja sebuleni kuitikia kibwagizo mwanamume mashine kwa furaha, huku akimkodolea jicho mumewe!!
James Graham alisema, LOVE IS BLIND, THEREFORE MARRIAGE IS AN INSTITUTION FOR THE BLIND. Mapenzi Ni upofu, hivyo ndoa Ni taasisi ya vipofu. Mara zote ona mazuri na si mabaya. Wakati wengine wanajiuliza kwa nini unaishi na mtu Kama yule, wewe unamshukuru Mungu kwa kukupatia mwenza bora kama huyu. Hakika hakuna mume atachomoka mkononi mwa mke.
gofo, Saint anne, Marianah

9~Kutoa siri zenu nje,mambo yenu ya ndani kutangaza nje,kwa ndugu,Jamaa,majirani
Mambo yenu muyamalize wenyewe kwa upendo na amani
☆mtu yoyote asijue mambo yenu