Jinsi ya kutunza uso | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kutunza uso

Discussion in 'JF Doctor' started by Michael Amon, Mar 30, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Uso ni sehemu ya kuonyesha uhalisia kwa mwanamke na unapotaka kujua ni jinsi gani mwanadada au mwanamke anapenda urembo basi utamwangalia usoni.


  Kwa mtazamo huo utaona yule mpenda urembo akiwa amepaka baadhi ya vipodozi usoni kwa mfano:- Poda, Lip-Stick, Wanja n.k na utagundua kwamba niliyekutana naye ni mmoja kati ya wanawake wanaopenda urembo.


  Leo imekuletea mada ya jinsi unavyoweza kusafisha uso wako na ili uelewe hilo fuata haya yafuatayo:-


  a)Penda kuosha uso wako kwa maji safi na salama na ili kujiepusha na mlipuko wa maradhi yatokanayo na maji.


  b)Kama uso wako wa mafuta basi tumia maji yenye uvugu vugu, ili kupunguza mafuta usoni mwako na ili kuuwezesha uso kuwa mkavu na kama unasura isiyo kavu, basi nakushauri utumie maji yoyote unayopenda kama ni vugu vugu au ya kawaida.


  c)Tumia sabubi yoyote nzuri uitumiayo kunawia uso wako siku zote, ili kuiboresha ngozi ya suo wako.


  d)Ila penda kutumia sabuni zisizo kali pindi usafishapo uso wako na itakuepusha na baadhi ya matatizo ambayo wanawake wengi huyapata kwa utumiaji wa sabuni kali.


  e)Tumia kitambaa safi na salama au taulo laini lililosafi na salama ili usipate matatizo ya michubuko usoni mwako, kitu kitakachopelekea kutokuwa na ngozi nzuri usoni.


  f)Usipende kutumia kilevi cha aina yoyote na kama ni mtumiaji usitumie kupita kiasi, kwani itapunguza uzuri wa sura yako kwani ulevi siku zote ni mbaya hupunguza baadhi ya vitamins mwilini mwa mwanadamu.


  g)Pia usipende kutumia sigara si nzuri kwa uboreshaji wa sura yako na afya yako kwa ujumla.


  h)Jitahidi usiwe mtu wa kutoka toka sana usiku ili upate muda mrefu wa kupumzika na uzidi kuboresha na kuirutubisha ngozi ya uso wako na kuifanya ipendeze daima.


  i)Pia unashauriwa kunywa maji, kula mboga za majani na matunda kwa wingi, na kwa kufanya hivyo utazidi kuonekana ni mwanamke mwenye sura safi, nyororo na iliyo na afya njema na yenye kuvutia daima machoni mwa jamii inayokuzunguka.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na wewe ni mmoja wa wapenda urembo ehhhh?
  Hongera.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ushauri.
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ndio. Napenda sana urembo na napenda sana kujitunza.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  U are welcome.
   
 6. salito

  salito JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhh..napita tu..
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  YM una undugu na boflo?
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Hapana. Kwa nini umeniuliza hilo swali mkuu?
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwasababu unapenda sana UREMBO. Vipodozi gani hua unatumia?
   
 10. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,119
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Hivi we si mwanaume?
  Mbona unasema wapenda kujitunza tupe siri ya mafanikio?
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Lol!
  Kwani Boflo anapenda sana urembo?
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Uache kuosha uso na 'jaribu' na sabuni za magadi. Afu punguza disco uwe unalala mapema eeh. Ndo siri ya urembo wa mkweo,hehehe!
   
 13. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sabuni gani inafaa kwa kuoshea uso ulo na ngozi yenye mafuta mengi?
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Sasa Lizzy, kama mimi mwanaume nikitumia vipodozi na wewe utatumia nini?
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo wanaume tunapokosea na ndio maana tunapigwa vibuti na mademu zetu kila kukicha. Nina nani aliyesema kuwa mwanaume hapaswi kujitunza? Unadhani kuna mwanamke ambaye anapenda mwanaume asiyejitunza?
   
 16. Primitive

  Primitive JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa iyo unatunza sura ili usipigwe chini na demu wako? madogo wa siku izi bana tabu tupu?
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Hapana. Najitunza kwa sababu napenda kufanya hivyo. Pili mimi sio dogo.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tunatumia wote I guess. Ndo yale mambo ya kugombania kioo na mtoto wa kiume.
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaa!!! Actually natumia vipodozi vya kawaida tu vya kiume na si kama mnavyotumia nyie wadada
   
Loading...