Jinsi ya kutoka nje ya mwili (Astral Projection)

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,461
2,000
ASTRAL PROJECTION/Mental Projection.

Ni Ule Uwezo Wa Mtu Kutengana Na Mwili Wake Ki Fikra Katika Imani Husemwa Kiroho.
au pale ambapo mwili unakuwa umetengana na fahamu zako.
Utokaji huu wa nje ya mwili upo wa aina mbili au tatu na wenyewe ni wa roughly watu wanafundisha kwa maelezo marefu na mapana hali ya kuwa ni kitu kifupi tu watu wanatakiwa kujua jinsi ya kutoka na mengine kujifunza huko huko.
images (2).jpg

FAIDA ZAKE:
1. Kujitambua kuwa wewe hufi na kuondoka moja kwa moja: Hili ni tukio litakalo kubadilishia maisha. Mamilioni ya watu wamekua wakithibitisha kuwa mtu akifa hapotei moja kwa moja bali kuna maisha mengine ambayo ataishi wale wasioamini life after dealth.

2. Kuongeza uwezo mzuri wa kulala:
Hii husaidia mtu kulala katika hali ya usalama na kupata nguvu inayozungumziwa baada ya kulala na kujua ni ipi sababu kubwa ya kulala tunalala ili miili yetu ipumzike roho zetu zianze kuishi.

3. Kuongeza nguvu ya majariwa:
Hii inaongeza kipawa cha unabii na uwezo mkubwa wa kumsoma mtu akili hufahamika kama kama mind reading au telepathy, kasimama hapo wewe unaongea na roho yake.

4. Kujiendeleza Kimaisha:
Ukiwa nje ya mwili inakuthibitishia kuwa wewe ni zaidi ya binadamu wa kawaida hivyo hukuongezea akili ya utendaji zaidi kwa kutumia maajabu na si nguvu tena.

5. Inakuongezea kukomaa kiroho:
Watu wengi wamekuwa na roho nzuri baada ya kuishi na kiumbe zaidi ya asiekuwa mwanadamu.

6. Inaongeza heshima ya maisha:
Hii hukufanya umuheshimu kila kiumbe na umuhurumie hata paka maana kule una uwezo wa kuongea hata na wanyama pia.

7. Inaongeza akili kumbukumbu na ubunifu:
kupitia ufahamu utakao kuwa nao kwa zoezi hili inaeleweka kwamba utakuwa umefungua sehemu za ubongo wako za fahamu zinazodeal na akili pamoja na kumbukumbu.

8. Kukuwezesha kupata majibu yako mwenyewe kwa spiritual guide:
kutoka nje ya mwili kutakujibia maswali mengi ambayo ulikua huwezi kuyajibu katika ulimwengu wako wa kiroho.

9. Kuondoa woga wa kufa:
kuhofia kifo ni kuhofia jambo usilolijua.utakapotoka utaona kwamba kumbe nina uwezo wa kuishi maisha ya pili hata nikifa.

10. Kutambua na kuelewa mambo ya kale yaliyopita:
utajifunza jinsi ya kupanua ubongo wako haya kuzungumza na historia za kale ingawa unaweza kuona pia tukio lijalo ila hii ni kwa wenye power ya precognition na retrocognitions.

11. Kupaa na kufurahi:
Ulimwengu wa roho hata anga sio mpaka. unaweza kupaa nyuma ya mawingu. na ukapaa kama puto. unataka kuwa na macho ya ndege mjini? la shaka! au unataka kupaa na kuogelea kama samaki dolphin na hata kuruka kama ndege, au kudumbukia ndani na kuogelea kama samaki!

ukitaka unaweza hata kufika kwenye sayari za juu na zile ambazo bado hazijawa discovered wazungu walifanya zamani sana hii na kwenda huko kabla hata ya kurusha ndege, unaweza kwenda popote duniani na nje ya dunia hata kuwatembelea marafiki kila corner ya ulikmwengu

12. Kuthibitisha kwamba mwili wako utakufa ila akili au nafsi yako itabaki tu

13. utayaona mengi maisha yako yaliopita na kuyachezea na utakuwa na nafasi ya kuona kila kitu ambacho unatakiwa kufanya ufanikiwe:
Pia hii yaweza kuwa tiba kubwa kwa magonjwa yasiyotibika kwa maana unaingia hata sehemu ambazo zimefichwa hasa na waweza kula dawa yeyote.

14. Kukutana Na Malaika wako wawili
Utawaona hawa hatua ya kwanza kutoka na kukuongoza kwa mengi ukitaka kuwaona.
japokuwa hawaonekani moja kwa moja ila kama vivuli

15. Kuongeza Nguvu ya miujiza
Kutoka huku kutakufanya uongeze nguvu zako za miujiza kama vile
kuona vitu visivyoonekana kwenye real world, kuskia sauti za mawazo ya mtu, kujua kinachotokea dk kadhaa zijazo, kumlazimisha mtu kufanya utakacho (mind control), kuhisi jambo fulani linatokea, nguvu ya unabii,

16. Kuona aura ya kila kitu na nguvu zingine nyingi tu. haya yote yatakutokea kwa maana umezidi mpaka wa ubongo wako hapa ndio tunaanza kuona more than a normal brain function(waweza kuwa genius pia ukitumia vizuri, anyway usitumie manguvu yote hovyo utaanza kuhisi kuchanganyikiwa fuata hatua kwa hatua.

17. kujaza busara akilini.
hii hukufanya uzidishe busara katika akili yako na amani kuu katika roho yako

18. Kuongeza tamaa ya kupata majibu
Kutoka nje ya mwili kutakufanya kujibu maswali na kujua zaidi kwamba wewe ni nani? upo wapi? na unafanya nini? na unaenda wapi? ukijua hayo hutabadilika mfumo wako wa maisha?

19. Kuwaona waliokufa
Hapa utakutana na ndugu zako uliokuwa ukiwapenda waliotangulia mbele za haki. Kukutana nao huku kutakusaidia sana kuwasaidia kama kuwalipia madeni na kukuonyesha mali walizoficha kama walikua wanakupenda.

20. Kujiongezea maajabu ya maisha
hapa utajifunza mengi kuona kila kiumbe kisichoonekana kupajua sehemu watu na nyumba kabla hujaenda

21. Kupona
Ukitoka nje ya mwili unakuwa umejitibu hapa utaweza kujitibu mwenyewe na wengine na wanyama pia.

Na Hizo bado ni baadhi tu:
astral-travel-compressed.jpg

Ni Aina Ya Nguvu Ambayo Huwa Nayo Watu Wote Isipokuwa Katika 100%

65% Ni Watu Wasioijua

25% Ni Watu Wanaoijua

10% Ni Watu Wanaoitumia

Hatua za kufuata ili uweze kutoka nje ya mwili

Kuna Njia Mbili Za Kutoka Nje Ya Mwili Hapa Nitaielezea Moja.

Njia Hizo Ni:

1; Kutoka nje wewe binafsi

2: Kutoka nje ya mwili kwa msaada wa mlio(Binaural beats)
astral-projection.jpg


HATUA ZA KUFUATA KWA NJIA YA KWANZA:

NI RAHISI TU.!
Ukiwa katika hali ya utulivu na utayari na amani na pia kujiamini kuwa leo nitaweza kutoka kwa mara ya kwanza,

HATUA ZA KUFUATA:
1; Oga Na Vaa Nguo Safi Zisizo Bana yaweza kuwa hata night dress ambayo ni laini au nguo yoyote itakayokufanya uwe vema na huru katika kufanya jambo hili,

2: Lala Chali Mgongo Ukiwa Umenyooka Vema huku umefumba macho, hakikisha hukazi mwili wala kufanya focus yoyote katika mwili wako ili uweze kufanya vema na kwa usawa na utulivu,
images (4).jpg

3: wakati ukiendelea kuutafuta utulivu utapata vishawishi vya kujigeuza au kujitingisha usiweke mawazo yako huko usiweke wazo moja wala usilenge wazo sehemu moja wala usitengeneze picha yoyote akilini wewe tulia tu. Kumbuka ili kufanikisha zoezi lolote la kiroho UTULIVU,UTULIVU,UTULIVU pekee ndio jambo au kitendo au maamuzi pekee ya kukufanikishia jambo la kiroho, usijishike wala kujitingisha wewe tulia tu UTULIVU ndio kitu kiwe kinachozunguka kwenye akili yako na mwili wako na pumzi yako TULIA. utaanza kuhisi uzito kwenye viungo mbali mbali vya mwili wako hasa kichwa.

4: Usitingishe Macho Wala Kuchezesha Mwili Wako. tulizana usiogope wala usihofu kwa maana hakuna cha kukuogopesha kwa wakati huo zaidi ya mwili wako ni sawa na mtu aliyelala usingizi.

5: Subiri Na utulizane Kwenye Pumzi yako ( Hapa unakuwa unaupa taarifa ubongo wako kuwa mwili wote umeshalala au upo kwenye state ya ndoto)

6: ukiweza kujizuia Kujigeuza Geuza Au Kujikuna Ubongo Utajua Umelala Na Utaruhusu Mwili Kuachia Kinga Ya Paralysis Au Ganzi Salama Ya Mwili Mzima.
Ambayo Huwa Inakinga Miili Yetu Kutokujiumiza Wakati wa Kuota Mfano: sleep walking(unaota huku unatembea) au wakati unapigana ndotoni usiweze kupiga au kujiumiza.

7: Wakati Hali Hii Inatokea Hapo Ndipo Unaweza Kujitenga na mwili wako ambao umepata ganzi.
tatizo hapa huwa lipo katika kujua ni upi mwili sahihi maana bado miili miwili inakuwa imeshikana
ukiamka na mwili wako wa ganzi kila kitu utakuwa umevuruga na utaamka kwenye mwili wenye ganzi (hii mimi ninauzoefu nayo pia unajiona upo macho lakini mwili hauamki wala kucheza unaganda ni kawaida ila huwa ni inashtusha kidogo. haichukui muda ni kama sekunde 10 ukianza kujishtua au kujitingisha ila inashangaza kidogo na kukutisha kama ni mwoga kwa maana unaweza hisi utakuwa hivyo moja kwa moja.

Sasa Je Utajua Vipi Kati Ya Miili Hii Upi Ni Sahihi?

Mbinu Rahisi Ipo Hivi Ukifikia Kwenye Hatua Hiyo Ya Kutoka. tengeneza picha Kwamba Una Mikono Mipya Na Miguu Mipya..
na ukishaingia kwenye hali hiyo hutokea set ya mingine na ndio unaweza kutumia kwa kutoka.

Lakini kwa wengine hii huwa ngumu sasa hapo unatakiwa uangalie dali na kuhisi ikiwa ni pamoja na mbinu kuwa kamba inashuka na kukukuta unaishika kisha unahisi inakuvuta na kukufanya uelee

9: Baada Ya Hapo Inuka Katika Mwili Wako huo na Sogea Mbele Hatua Tano Geuka Nyuma na Uangalie Mwili Wako Uliouacha.

10: Hongera Umeweza Fanya Chochote Unachojiskia Hakina Madhara Kwenye Real World....
lakini vipo ambavyo vinaonekana in real world play safe there.
Lakini pia kwa wanaoanza ni bora asiende mbali aishie karibu na nyumbani kisha azunguke zunguke ili azoee mazingira ya mwili huo na hali hiyo.


ANGALIZO:
3638238241_527c68904b_z.jpg

Wakati Unautizama Mwili Wako Uliouacha Kuna Kitu Kina Kuwa Kimekuunga Na Ule Mwili Kama Silver cold Hivi Nyeupe Ya Kama Wingu Hiyo Ndio Hukusaidia Kurudi Hata Kama Umepotea Njia.....
download.jpg


kama una swali ambalo ni personal na upo nje ya forum:

Wasiliana nami kupitia email hii:

Rakimsspiritual@gmail.com

au namba hii ya mtu aliye karibu nami

+255626085437

Kwa haya na mengineyo pia tembelea
Rakims Spiritual

Rakims
 

Attachments

Last edited by a moderator:

Masanva Aya

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
425
1,000
Mkuu Rakims na MziziMkavu, naombeni sana wakati mnatoa hili somo, pia muwape angalizo hao wanafunzi wenu, kuwa mchezo huu pia ni sawa na kuijaribu sumu kwa kuilamba!. Wapeni kabisa masharti ya kuzingatia, wakikosea ndio safari jumla!, asubuhi unakutwa ulitangulia ukiwa usingizini!.

Masharti ni haya.
  1. Fanya hivyo ukiwa umelala peke yako chumbani, na kabla hujaanza ujinga huo, hakikisha umefunga mlango kwa funguo, kwa sababu akitokea mtu akakuamsha kwa kukutingisha kwa nguvu na kuchange ile position yako hata ya milimita moja, ile cord ni kama utando wa buibui, inakatika, wewe unakuwa ndio basi tena!.
  2. Unaweza kukutana na "the under world" ukaona maisha hayo ya astra plane ndio bora zaidi kuliko real world, hivyo cord ikakatika, huku unakutwa ndio basi tena!, wewe ni safari jumla!.
  3. Hizi ni highest stages za meditation ambazo haziruhusiwi kufanywa na beginners, na hazifanywi un supervised vinginevyo ni safari jumla!.
  4. Yote utakayoyashuhudia kwenye astra body, unaweza kuyafanya by simply opening up the "third eye!"
  5. Hizi ndizo the first stages za wachawi!.
Wito wangu mimi wa wafuatiliaji wa haya makitu, kama hujui unataka nini, au utoke out of body ili kuachieve nini, please don't do it!. Mtu asikudanganye kuwa its very fun to go out of body, is not fun!. Too much knowledge on anything is harmful, please don't try unless you are sure what you are trying to do!.

Paskali
Aise, kuna watu wanakipaji cha kupinga matarajio ya Mungu kwa binadamu?
Harafu binadamu kama P anapinga. Kipaji cha mtu mmoja si cha kila mmoja. Kama wewe huna hicho kipaji kaa kimya, si kupinga pinga kila kitu.
PASCAL HESHIMU, mawazo na vipaji vingine kwa liojariwa.
Unamsifia yule pale magogoni, ni kipaji chako kufanya afanyavyo, hivyo usiwe mpigaji kwakuwa tu huna hicho kipaji.

Kwani utapata malaria ukikaa tu kimya sometimes..
 

nabiidaniel

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
763
1,000
Kuna uchawi wa aina mbili (au zaidi), kuna white witch na dark witch, dark witch ndio hip ya matunguli hirizi n.k, white witch ndio hio inayofundishwa na akina Rakhim.

Ukweli ni kuwa huu ni uchawi, mwili bila roho umekufa, kinachofanya roho itoke na mwili ubaki hai ni pepo linaloingia ndani ya ule mwili ili kuufanya hai, na roho yako itazurura kwa msaada wa mapepo ambayo huyaoni, ( Rakhim anasema ni malaika walinzi wawili unaoona vivuli vyao!!!)

Mwisho wa Siku utalazimika kwenda kusujudu kwa Mkuu wa wachawi, malkia wa mapango, Mwenye pembe mbili kama mbuzi, Utalazimika kumkufuru Mungu na kudanganywa kua ukifa utaendelea kuelea hivo hivo au utaenda ujinini!!! UWONGO MTUPU

Shetani atakuficha hutaona kuzimu ya kweli ya waliokufa na dhambi na mateso wanayopata, atakupeleka kuzimu ya wachawi (ujinini) kwenye maghorofa na starehe kumbe....
 

Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,177
2,000
Eti pepo anakufanya huwe hai. Ivi muandishi sizani kama unajua ulicho andika
Kuna uchawi wa aina mbili (au zaidi), kuna white witch na dark witch, dark witch ndio hip ya matunguli hirizi n.k, white witch ndio hio inayofundishwa na akina Rakhim.

Ukweli ni kuwa huu ni uchawi, mwili bila roho umekufa, kinachofanya roho itoke na mwili ubaki hai ni pepo linaloingia ndani ya ule mwili ili kuufanya hai, na roho yako itazurura kwa msaada wa mapepo ambayo huyaoni, ( Rakhim anasema ni malaika walinzi wawili unaoona vivuli vyao!!!)

Mwisho wa Siku utalazimika kwenda kusujudu kwa Mkuu wa wachawi, malkia wa mapango, Mwenye pembe mbili kama mbuzi, Utalazimika kumkufuru Mungu na kudanganywa kua ukifa utaendelea kuelea hivo hivo au utaenda ujinini!!! UWONGO MTUPU

Shetani atakuficha hutaona kuzimu ya kweli ya waliokufa na dhambi na mateso wanayopata, atakupeleka kuzimu ya wachawi (ujinini) kwenye maghorofa na starehe kumbe....
 

nabiidaniel

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
763
1,000
Eti pepo anakufanya huwe hai. Ivi muandishi sizani kama unajua ulicho andika
Lugha ipi nzuri kwako pepo au jini? Unajua wanaochukuliwa misukule roho zao zinachukuliwa mda mrefu kabla ya kifo cha "kutengenezwa", nini kinafanya miili iwe hai wakati roho imechukuliwa?...jini (pepo), umewahi kusikia habari za kuchukuliwa kivuli? Ulidhani ni shadow...pole
 

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,461
2,000
Upuuzi mtupu.

Ukitulia kama hivyo unavyoelekeza kitakachotokea ni utasinzia tu.

"Astral Projection" pekee utakayoiona ni ndoto zako kama kawaida ya ukilala.

Kutoka nje ya uhai wako ni kitu kisichowezekana. Ndo maana hata kwenye ndoto zote ukiota unataka kufa lazima ushtuke usingizini. Kanuni haziruhusu kukuvusha ulimwengu wa pili kwa maono tu. Ukivuka ni umevuka kimoja.

Sema hii ni elimu nzuri kwa kutapelia watu. Maana binadamu wana shauku sana ya kutaka superpowers na kuona kesho ikoje.
Mkuu it normal kwa watu wasiokuwa na elimu na kitu kusema kama hayo unayosema
 

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,461
2,000
Kuna uchawi wa aina mbili (au zaidi), kuna white witch na dark witch, dark witch ndio hip ya matunguli hirizi n.k, white witch ndio hio inayofundishwa na akina Rakhim.

Ukweli ni kuwa huu ni uchawi, mwili bila roho umekufa, kinachofanya roho itoke na mwili ubaki hai ni pepo linaloingia ndani ya ule mwili ili kuufanya hai, na roho yako itazurura kwa msaada wa mapepo ambayo huyaoni, ( Rakhim anasema ni malaika walinzi wawili unaoona vivuli vyao!!!)

Mwisho wa Siku utalazimika kwenda kusujudu kwa Mkuu wa wachawi, malkia wa mapango, Mwenye pembe mbili kama mbuzi, Utalazimika kumkufuru Mungu na kudanganywa kua ukifa utaendelea kuelea hivo hivo au utaenda ujinini!!! UWONGO MTUPU

Shetani atakuficha hutaona kuzimu ya kweli ya waliokufa na dhambi na mateso wanayopata, atakupeleka kuzimu ya wachawi (ujinini) kwenye maghorofa na starehe kumbe....
Hapana mkuu endelea kutafuta elimu utajua ninachozungumzia hapa
 

Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,177
2,000
Ujue mwil na roho mpaka ziachane completely ni lazima spiritual golden rop ikatwe au iachane ungekuwa mwil umekufa, Ata ufanye dawa gani hawez rudi lakin kama iyo rop haijaachana anaweza kurudi. Je ujawahi sikia flan msukule umemshidwa au mtu kakohoa na kuwa mzima wakati doctor wako alisibitisha amekufa. Kurudi kuna mazingira yake labda marehem sadikika aliwekewa kinga. Au individual ability kama gift alio zaliwa nayo maaana kuna watu hawalogeki na hana kinga ya mahalifa ya mtu, na hajaokoka kwa ndugu zangu wakristo, pia pitia na enock
Lugha ipi nzuri kwako pepo au jini? Unajua wanaochukuliwa misukule roho zao zinachukuliwa mda mrefu kabla ya kifo cha "kutengenezwa", nini kinafanya miili iwe hai wakati roho imechukuliwa?...jini (pepo), umewahi kusikia habari za kuchukuliwa kivuli? Ulidhani ni shadow...pole
 

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,144
2,000
NB: Kurudi Kwenye Mwili Wako Ukitaka Unarudi Tu Bila Tatizo Wala Kuukosa Hakuna Tatizo... Waweza Hata Kufumba Macho Ukataka Ukifumbua Uamke Kwenye Mwili Wako Unaamka au unagonga kidole au unajiambia ni muda wa kuamka

unaamka binafsi huwa narudi zangu kwenye mwili wangu nikiusogelea karibu zaidi au kutaka kuugusa naamka


Rakims
Nazidi kupata Darasa.......Kuna siku nilikuwa kwenye shughuli ya kifamilia na baada ya pilika nyingi watu wengi walilala ikafika mida ya Maakuli ikabidi tuwaamushe waliolala kwa kuwatikisa Mzee mmoja akagomba eti tusiwaamshe kwa njia hiyo na baadala yake Tuwaamshe kwa Kuwangonga gonga KIDOLE GUMBA cha miguuni.......!!! Sikujua maana Yake...... Sasa nimeelewa....

Rakims endelea Mkuu..........
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,348
2,000
Mimi sleep paralysis hunitokea, yaani mwili unakufa ganzi ila nakua alert na kuskia kila kinachotendeka karibu yangu, mwanzoni nilikua naogopa sana, nilikua nadhani ni majini yamenigandisha.
Lakini siku hizi huwa natulia na kusklizia tu hadi raha.
 

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Feb 15, 2018
565
1,000
Nilijaribu kutoka nje ya mwili ilinipa shida sana,siku hiyo ilikua alufajiri kama saa 11 hivi nikaamka nikabafu nikajifuta maji kama kawaida,nikajilaxa kwa utulivu nikaachia mwili nikaulegeza nikavuta hisiakali,theni nikahisi mwili unakakamaa kabisa dheni nikajikuta natoka kitandani nakaa pembeni halafu nauna mwili umejilaza ghafla najikuta najikuta natetemeka kwenye njozi kubwa.sijui ilikuaje lakini haifai kufanya hivyo.nilijikuta namuna mama yangu alie fariki miaka mingi iliyo pita nikaongea nae then akatoweka,ghafla nazinduka najikuta machozi yanatoka tena kwa hisia kali.nainuka naenda bafuni kuoga wakati naogo bado hisia zinakuja namaswali mengi najiuliza ivi kimetokea nini vile?sirudii tena
 
Top Bottom