Jinsi ya kutengeneza Chicken Sandwich

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Mahitaji
Mahitaji ya kuku wa sandwich

  • 1 kilo ya kifua cha kuku au miguu ya kuku toa ngozi ili kukwepa mafuta.
  • 1 tangawizi kubwa
  • 3 mbegu za pili pili manga
  • Chumvi kulingana na ladha unayotaka

Chemsha mchangayiko huo wote pamoja na kuku mpaka kuku iive vizuri na iwe laini kabisa kisha toa katika jiko na uache upoe.

Mahitaji kwajili ya sandwich

  • 1 loaf of wholemeal bread or French wholemeal loaf (sliced)
  • 1 pili pili hoho iliyokatwa saizi ndogo ndogo
  • 1 kitunguu kilichokatwa saizi ndogondogo
  • 3 au 4 mayonaisi kijikokikubwa cha chakula
  • 3 nyanya nyekundu kata mviringo nyembamba (sliced)
  • 1 tango zuri kata mviringo nyembamba (sliced)
  • 1 lettuce salad nzuri ya kijani

Jinsi ya kuandaa
Chukua kuku aliepoa nyofoa nyofoa nyama ya kuku weka mifupa pembeni kisha weka ile nyama katika bakuli changanya na mayonaise, chumvi, kitunguu, pili pli hoho na pili pili manga ya unga.

Kama mchanganyiko wako ni mkavu ongeza mayonaise na lemon juice kidogo kuongeza ladha zaidi.

Chukua mchanganyiko wako wa kuku weka juu ya jani la salad panga vizuri usijaze sana ili uweze kufunika na kipande kingine cha mkate kilichobaki kisha weka slice ya tango na ya nyanya juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mayonise.

Chukua kipande kingine cha mkate kilichobaki na funika kwa juu unaweza kula tayari au kama unapenda kau kau unaweza weka mkate wako huo kwenye toaster mashine na kuukausha kwa muda mapaka ukapata rangi ya kahawia na kua na ladha tofauti na ukala sandwich ya moto.

ChickenSalad-main_Full.jpg

Muonekano wa chicken salady baada ya kuikata

Chicken_Mayo_01.JPG

Muonekano wa mchanganyiko halisi wa chicken mayonise ukiwa juu ya jani la salady

croppedimage460460-egg-mayonaisse.jpg

Muonekano halisi wa sandwitch iliyokatwa tayari kwa kula

Recipe hii nimeiandaa special kwa ajili ya Bibie Kongosho na Kipipi Nimeanzisha rasmi darasa la mapishi kwa ajili yenu. Nataka muwe wapishi wazuri more than I. I hope you will like this recipe.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom