Jinsi ya kutambua processor ya simu na kuijua simu ghushi(AndroidOS)

Jinsi ya kutambua processor ya simu na kuijua simu ghushi(AndroidOS)

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,063
Reaction score
43,492
Processor katika simu ni kifaa ambacho huchukua maelezo kutoka kwenye software na kufanya kazi za kimahesabu na kimantiki pamoja na kutoa na kuingiza vitu ili simu yako ifanye kazi kwa ufanisi. unapo peruzi internet au kuangalia video na picha basi processor inakuwezesha. tunaweza kusema ni moja kati ya vitu muhimu kwenye simu na processor ikiwa nzuri na simu itakua nzuri pia.

Karibia simu zote zinatumia processor za arm ambazo zimetengenezwa huko uingereza. makampuni kama qualcom, samsung na apple hutumia chip za arm na kudesign wanavyotaka wao na leo hii unakuta soc kama exynos, tegra na snapdragon.

Aina za processor
Hawa arm wana series yao ya processor inayoitwa A series ambayo ndio sana inatumika kwenye simu na inajumuisha processor hizi.
-cortex A5
-cortex A6
-cortex A7
-cortex A8
-cortex A9
-cortex A12
-cortex A15

Processor hizi ndio kama unavyosema intel i3, i5 au i7. kama nilivyozipanga hapo juu cortex A5 ndio ndogo na cortex A15 ni kubwa. hivyo unapochagua proccessor za simu usiangalie clock speed kwanza mpaka uangalie aina ya processor. mfano processor ya 1.2ghz quadcore cortex A7 imepitwa nguvu na 1ghz dualcore cortexA15.

Jinsi ya kutambua simu yako inatumia processor ipi
Kuna njia mbili hapa za kujua.
1. Kuangalia specs online. hapa unaweza kwenda website kama gsmarena halafu ukachagua simu yako na kuangalia specification
2. Kwa kuinstall app halafu kujua specs za simu kutumia hio app mfano cpu-z

Jinsi ya kutambua simu fake
combination ya njia zote mbili hapo juu itakufanya ujue simu zote fake na original.

Mfano hapa nita assume mtu ameniletea samsung galaxy s3 ili niitambue kama ni fake au original. kwanza nitaenda gsmarena na kuangalia specs zake,
image.png

Hapo utaona s3 ina chip inaitwa exynos na processor yake ni cortex A9 quadcore 1.4ghz

Halafu nitainstall cpu-z kwenye hio simu na kukagua specs zake.
aWD3msh.png

Hivyo hapo juu utaona kuwa specs za gsmarena na cpu-z zimefanana na kuonesha simu ni original. Zingekua tofauti hapo unajua simu sio umepigwa changa la macho. nafkiri hii itasaidia wale wote wanaotaka kujua simu fake na original
 
Mkuu hivi ile namba *#*#4636#*#* inayoleta test information/Hidden menu ambayo unaweza kuset ishu za networks vp?, maana from my Xperience nimeona inakubali katika almost all OG android devices lakini inakataa kwenye feki
 
kaka sijathibitisha hilo. ila kama watu wanachange imei je watashindwa clone hio namba?
 
Mkuu Mediatek imekaaje?
Hii maneno inanichanganya kidogo
Mfano Tecno Phantom A+
Capture.PNG
 
Kaka kama unataka kununua simu mpya dukani, je muuzaji ataruhusu u_perform hizo test?

Dukani jaribu hyo namba aisee, za feki huwa hazirespond na nyingine ukitaka kumalizia tu hiyo namba, simu yenyewe automatically inafunga dial panel

Note: this is not for all android devices, nyengine manufacturers hawaweki hii kitu... So the best way, is of chief-mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hivi ile namba *#*#4636#*#* inayoleta test information/Hidden menu ambayo unaweza kuset ishu za networks vp?, maana from my Xperience nimeona inakubali katika almost all OG android devices lakini inakataa kwenye feki

Nilikuwa siijui mkuu wickerman , nimejaribu imekubali. Inaleta "Testing". Shukrani kwa kuniongezea ujuzi.
 
Kaka kama unataka kununua simu mpya dukani, je muuzaji ataruhusu u_perform hizo test?

Kama ni duka la samsung haiwez kuwa simu fake ...kama ni maduka ya kawaida cha kufanya nchakufanya muulize mara mbili mwenye duka akithibitisha mpe hela...baada ya kukupa simu weka line au weka wi fi hotspot afu download cpu-z ni just kb kidogo tu...run ikupe specs ikienda kinyume mwambie akupe hela yako fasta
N.b ni muhimu kufanyia humo humo dukani
 
Vp si na antutu benchmark inaweza kukuonesha phone specification

antutu inaonesha ila watu wanaichakachua sana. mfano clone zinatumia mediatek cortex A7 au A9 hawana high end processor lakini kwenye antutu inascore 20,000+ score ambayo hata nusu yake haifikii.

sasa hivi kuna scandal manufacture wote wa android wanazitengeneza simu ili zicheat kwenye benchmark hadi kina samsung, htc na lg wanafanya.

anandtech ndio kazi yake ya benchmark msome hapa kafanya analysis nzuri
AnandTech | They're (Almost) All Dirty: The State of Cheating in Android Benchmarks
 
Mkuu hivi ile namba *#*#4636#*#* inayoleta test information/Hidden menu ambayo unaweza kuset ishu za networks vp?, maana from my Xperience nimeona inakubali katika almost all OG android devices lakini inakataa kwenye feki

Kaka Hiyo Namba Ukishaingiza Una Dial Au Yenyewe 2 Inasense?
 
si anakupa warranty? chukua kama ni fake unamrudishia. akikataa unamshtaki maana ushahidi upo
Mkuu samahani kwa kuuliza swali la nje ya mada. Hivi Ukitumia betri ya simu ambayo uwezo wake ( i mean mAh) sio kama inavyooneshwa kwenye phone specification kuna madhara? Mfano kama phone specification inaonesha betri ya simu ni 2500mAh lakini nikatumia betri yenye 3100mAh, kuna effect yoyote kwenye uhai wa simu? Thanx
 
Back
Top Bottom