Leo nimevutiwa kuanzisha mada yenye utofauti kidogo, mada hii imepata msukumo wa kuwa na mada nyingi zinazofanana ambazo hazikuwa na haja ya kurudiwa. Mfano kuna baadhi tunaanzisha mada mpya wakati hoja/tatizo limeshajibiwa vizuri sana katika mada zilizopita, pengine mada ulioanzisha isipate mrejesho/majibu mazuri kuliko iliyopita na mifano mizuri ya mada hizi zipo JF doctor. Kuanzishwa mada za habari mpasuko, mtu anaweza kuanzisha hata siku baada ya tukio husika kuwekwa JF kutokana na kuchelewa kuipata na kutojua kama jamvi tayari inayo na muhusika anaweza kupokea kejeli ya kuleta 'zilipendwa'.
Kutokana na kujaribu kuifupisha mada yetu ili isichoshe na kuepuka tatizo tulilonalo la kutosoma vitu virefu, itakuwa katika sehemu nne fupi fupi. Inawezekana hutaelewa sehemu au una uelewa zaidi ya hapa ama una njia rahisi zaidi kueleza, uwanja ni wako.
Sehemu ya kwanza
View attachment 280594
Njia ya kwanza na rahisi kuliko zote ni kuingiza maneno muhimu(keywords) kwenye search box na kutafuta, njia hii itakuwa na manufaa kama ungependa kujua kitu kwa ujumla wake, itakuletea kila kinachohusiana na hiko kitu bila kujali ni cha muda gani na kinahusiana kwa kiwango gani.
Mapungufu ya njia hii itakuletea taarifa nyingi sana na nyingine zisiwe na mahusiano ya karibu na unachotafuta hivyo kukupa kazi tena ya kuanza kuchambua mchele na chuya na kutumia muda wako.
Sehemu ya pili
Advanced(Search mulitiple content)

Njia hii ina vitu kadhaa vimeongezeka, kufika hapa unabofya search bila kuandika kitu. Rangi zilizotumika zinawakilisha sehemu husika. Mfano

- Unataka kuangalia kama habari imeshaweka JF na ni tukio la siku husika basi unaweza kuchagua ilete taarifa za kuanzia jana na leo, itakupunguzia majibu mengi sana yasiyo husika na muda huo ulioanisha. Pia kama unataka matukio ya zamani na mada za sasa zisiwepo unachagua neno 'and older' badala ya 'and newer'. Mfano mada za kuanzia mwaka jana kurudi nyuma, hii ina manufaa endapo unataka kuoanisha tukio la zamani na tukio la sasa sababu ukitafuta pekee yatakayokuja ni matukio ya karibuni.
- Unataka kumtafuta mwanachama(member) sehemu rahisi ya kuanzia ni hapa kwa kuandika jina la member pekee kwenye 'username' na kutafuta, pia unaweza kuandika unachotafuta na kuandika jina la mwanachama alieweka/changia unachotafuta ili vihusiane. Hii pia husaidia kujua mwanachama ameanzisha mada gani na michango yake katika mada nyingine kwani huanzia hapa pia.