Jinsi ya kusoma vipimo kutoka kwenye Ramani

Ok ni hivi, kwenye ardhi hapo TUMIA Milimita 2900 hizo ambazo kiuhalisia ni MITA 2 na CM 90.
 
Ni muhimu kwanza kufahamu scale ni nini:

Scale ni uwiano wa kitu kati ya model(mfano ) na actual( halisi au kama kilivyo).

Kwa nini tunatumia scale - tunatumia scale kudogosha au kukuza kitu kwenye mchoro, kwa mfano wa nyumba huwezi kuichora nyumba kama ilivyo inabidi uidogoshe ili uweze kuichora kwenye karatasi kwa sababu kuichora kama ilivyo hakuna karatasi yenye saizi kama ya nyumba na haiwezekani.

Sasa unaposema scale 1:75 ni kwamba iyo nyumba yako imefanywa ndogo mara 75 katika mchoro, kwa hiyo meter au cm au mm moja kwenye mchoro ni sawa na meter, cm au mm 75 kwenye ardhi au kiwanja.

Sasa kama imeandikwa kwenye mchoro 2950, kwanza cheki kwenye huo mchoro kipimo gani wametumia ( mm, cm, m), kama ni mm kwa hiyo 2950 ni 2950mm ni sawa na 2.95m, kama ni cm itakuwa 29.5m na kama ni meter itakuwa 2950meter au 2.95 kilometer.

Kama scale ni 1:1 maana yake ni kwamba size ya kitu kwenye mchoro na kitu chenyewe viko sawa hapakufanyika kudogosha au kukuza kati ya mchoro na kitu halisi.
 
Back
Top Bottom