Jinsi ya kuroot simu za Android

Jinsi ya kuroot simu za Android

Mm nataka ku root samasung A7 2016 marshmalow, kuna mtu aliniambie et kwa samsung mashmalow bado haiwezekan, naweza harb simu ,je kuna ukweli hapo
ungemuuliza kwa uzur Kama alishawah kuua cm
 
Msaada niliroot TECNO Y3 asa nikafuta zile system app.
Nilifuta na dialer nimedownload dialer ingine inazngua haionyeshi incomming call wala outgoing call msaada mazee
ulitumia app gan kipind unaroot
 
mkuu tuma information za cm mfano version etc
nimetumia sana hizi rooting apps kama vile kingroot e.t.c kuroot Nokia 1 lakini wapi...nisaidieni mlifanikiwa mlitumia app ipi kuroot Nokia 1?
 
Nipe msaada imefika 97%
System auto purify

Inahitaji ku download file lenye 3.5mb
Nikijaribu kupakua inagoma
 
Wadau wa JF kama uzi unavyooleza hapo juu, naomba tufahamishane ni namna gani tunaweza kuroot simu zetu zile za matoleo ya juu kuanzia 6.0 - 9.0.

Pia faida zake na hasara zake, lakini pia tricks mbali mbali tunazoweza fanya baada ya kuroot simu zetu.

Ahsanteni.

Tukutane chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia hii mara nyingi uweza kufanya kazi kwenye simu zenye uwezo wa Android 2.1 hadi simu zenye Android 6.0 na baadhi ya simu zenye Android 7.0. Ili kuweza kuelewa zaidi njia hizi zimegawanyika kwenye makundi mawili yaani kundi la simu za makampuni ya Samsung, LG, HTC na Motorola pamoja na kundi la simu za Huawei, Tecno pamoja na simu nyingine kama iTel na nyingine.

Kuroot simu ni nini na kuna faida gani?
Kabla ya kuanza ni vyema ukajua kidogo kuhusu kuroot simu, kama umesikia neno hilo mara nyingi na hujui lina maana gani basi ningependa nikujuze kuwa kuroot simu ni kitendo cha kuondoa mipaka kwenye mfumo wa uendeshaji (Android System Files) na kuruhusu baadhi ya programu kwenye simu yako kuweza kufanya mambo ya ziada ambayo awali yalikuwa yamezuiwa na watengenezaji wa simu yako (simu janja).

Faida na hasara za kuroot simu

Kuna faida na hasara mbalimbali za kuroot simu yako na hii mara nyingi inategemena ni kitu gani unataka kufanya kwenye simu yako, moja kati ya faida za kuroot simu hizi hutokana na kama unataka kuinstall programu ambazo zinaweza kukupa uwezo wa kufanya vitu vya ziada kwenye simu yako.

Hasara kubwa za kuroot simu ni kuharibu simu yako na hii maranyingi inatokea kama hatua za kuroot simu yako zimekosewa. Pia unaweza kupoteza Warranty ya simu yako hivyo ni vyema kuwa makini kabla ya kufanya hatua hizi.

Jinsi ya Kuroot simu za Samsung, LG, HTC na Motorola (kuwa makini hatuta husika ukiharibu simu yako)

Kwa kuanza hakikisha unatumia simu hizo hapa juu na hakikisha toleo lako la Android ni kuanzia Android 2.1 hadi toleo la Android 7.0, Vilevile hakikisha kuwa simu yako ina chaji angalau asilimia hamsini.

Pia hakikisha simu yako ina internet kwani tutaenda kutumia programu ambayo ni lazima kudownload kwenye simu yako. Kama unayo mambo yote basi fuata hatua zifuatazo.

1. Fungua kisakuzi cha simu yako kisha bofya hapa > Kingo Root

2. Download na install App hiyo kwenye simu yako

3. Fungua App hiyo kisha utaletewa ukurasa unao kuitaji kuwasha App hiyo kwenye sehemu ya Accessibility, bofya OK kisha shuka chini kidogo mpaka sehemu ya Kingo Optimization kisha bofya ON.

4. Subiri kwa muda inaweza kuchukua muda kama wa dakika moja au zaidi inategemeana na simu yako,

5. Baada ya hapo utona maneno Root succeeded hii ikiwa na maana umefanikiwa ku-root simu yako. (kama utona roote failed zima simu yako alafu washa kisha anza tena hatua hizi).

Njia za kuroot simu za tecno, Huawei na iTel ni tofauti na njia ya kuroot Samsung, unaweza kujaribu kutumia programu ya Kingo Root kwenye simu hizi lakini kama programu hizi zitakataa basi unaweza kufuata hatua hizi zifuatazo.

1. Download programu ya Framaroot hapa > Frama Root

2. Install programu hiyo vizuri kwenye simu yako

3. Washa programu ya Frama Root kisha chagua kati ya Superuser au SuperSU (unaweza kuchagua hii baada ya sehemu moja kushindwa) Kumbaka kuwa makini na simu yako.

4. Kisha kwa chini yake chagua Boromir au option nyingine.

5. Baada ya kuchagua sehemu hiyo utaona simu yako ikianza kuroot

6. Baada ya hapo zima na washa simu yako, itakuwa tayari imekuwa rooted

7. Kama hatua hizo zimekataa rudia hatua ya 3 kwa kuchagua option nyingine pia rudia hatua ya 4 kwa kuchagua option nyingine.

8. Kujua zaidi kuhusu kuroot simu za Tecno soma HAPA

Mpaka hapo utakuwa umefanikisha kuweza kuroot simu yako ya Android bila kuwa na kompyuta, kumbuka njia hizi kwa namna moja ama nyingine zinaweza zisifanye kazi kwenye simu yako na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na sababu kubwa ya aina ya toleo la Android.

Kama una maswali au kuna mahali umekwama usiache ku-uliza hapo chini kwenye sehemu ya maoni nasi tutakuwa na furaha kujibu maswali yenu yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiroot simu huwezi kupokea update labda uiunroot tena, Huawei au Honor simu zao kama zimerootiwa siku hizi, unaicontrol unavyotaka ww, yaani inakupa uhuru afadhali tofauti na cm nyengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia magisk root iko poa sana...yenyew inakuja na feature ya magisk hide,,yani sim inakua rooted lakin apps zinazokataa root ,mfano mpesa au app za kibank basi haziwez detect hiyo root access

Faida nyingi sana...

Zile youtube adds za kuskip utaziskia kwa watu tu

Utaweza weka custom rom

Utapata sound mods za kutosha

Utaenjoy module kibao kutoka exposed framework

Inshort faida ni kibao tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa android zenye kutumia mfumo wa marshmallow, nougat (nadroid) na oreg kuroot kwa apps sim nyingi znagoma hivyo njia rahisi ni kutumia pc.. Kuna maelezo kidogo lkn hadi uwe na ujuzi wa kutumia pc au kama huez ukienda kwa mafundi cm wa kuflash sm kwa pc wengi huwa pia wanafanya rooting... Ila cha kuzingatia unaporoot cm chonde chonde usije badilisha imei number... Ni hatari kubwa sana TCRA wakikudaka hawatakuonea huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa android zenye kutumia mfumo wa marshmallow, nougat (nadroid) na oreg kuroot kwa apps sim nyingi znagoma hivyo njia rahisi ni kutumia pc.. Kuna maelezo kidogo lkn hadi uwe na ujuzi wa kutumia pc au kama huez ukienda kwa mafundi cm wa kuflash sm kwa pc wengi huwa pia wanafanya rooting... Ila cha kuzingatia unaporoot cm chonde chonde usije badilisha imei number... Ni hatari kubwa sana TCRA wakikudaka hawatakuonea huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
Aaaiseeee. Asante kwa wangalizo kiongozi.

Ila nikibadilisha Imei kwani nitakuwa nimefanya Nini au naweza kufanya nini Cha hatari kiasi nisionewe huruma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Program hipi nzuri ya root infinix hot 8, KingRoot imekataa. Inabakia 1% for long time over 2 hours

Sent using Jamii Forums mobile app
KingRoot imefall
Screenshot_20191211-133107.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom