Jinsi ya kupika mabumunda

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
MABUNDA ni aina ya chakula cha asili cha Afrika ambacho ni rahisi kukiandaa. Pia kinajulikana kama MKATE WA NDIZI Kwa lugha nyingine.Ni chakula kilicho katika mfumo wa mkate ila hiki upikwa na ndizi na unga wa mahindi.

MAHITAJI
> Ndizi mbivu zilizoiva vizuri au hata kukaribia kurojeka.

> Unga wa mahindi ila nzuri zaidi kama utatumia unga wa dona.

> Jani la mgomba.

JINSI YA KUPIKA
Menya ndizi zako na uziweke katika kinu kidogo kisha ziponde hadi zilainike na kuwa uji uji. Baada ya hapo, zitoe ktk kinu na weka katika bakuli kisha changanya unga wa mahindi hadi mchanganyiko wako ukolee.

Osha jani la mgomba vizuri na ulipitishe ndani ya moto ili lilainike.Kisha kata jani la mgomba vipande na chukua ule mchanganyiko wako wa unga na ndizi na uuweke katika jani la mgomba vizuri kisha ulisokote.

Weka katika sufuria au chungu na ubandike jikoni katika moto mkubwa kiasi.Funika na mfuniko wa chuma na juu paria moto kama unavyopika waki.

Subiri kwa dakika kumi au kumi na tano na ugeuze bumunda lako. Baada ya kuiva litakuwa gumu,hivyo tegua na ondoa mabaki ya majani ya mgomba na uache bumunda lako lipoe.

FAIDA ZAKE
> Ni chakula kinachodumu kwa muda mrefu bila kuharibika (kuchacha).

> Hakina madhara ya kemikali kama mikate ya viwandani.

Unaweza kula wakati wowote, waweza kunywa na chai au hata uji, pia usisahau juice.

"Onyesha ufahari kwa kula vyakula kwa kula vyakula vyenye asili ya mtanzania"

Maswali na ushauri vinaruhusiwa
 
Asante sana ndugu yangu umenikumbusha mbali sana enzi hizo za utoto,ila nilikuwa sikumbuki namna ya kupika. Chakula safi sana hii.

Naomba unieleweshe Hapo kwenye majani ya mgomba unamimina mchanganyiko wote au? Na sufuria unaipaka mafuta au unafanyaje? Na je naweza kutumia oven?
 
Hapana sufuria huipaki mafuta,unaiacha hivyo hivyo.Kwa upande wa oven sijawahi kujaribu nikaona inatokeaje.Kuhusu jani la mgomba,ni kwamba utaliosha halafu utalipitisha katika moto ili lilainike.

Utaligawa vipande kulinga na size ya bumunda unalopika,utachukua mchanganyiko kidogo na kuuweka katika jani la mgomba na ukunje kimakini ili mchanganyiko wako usimwagike.

everlenk ,pia waweza kufanya utafiti mwenyewe kwa kutumia jiko la oven,halaf uje kutuambia imefanikiwa kwa kiasi gani
 
Mi nilifikiri mabumunda ya kwetu Tanga, yale ya sukari, popcorn na sukari ya kuchanganywa. Anyway thanks kwa upushi huu umenikumbusha wakati nipo mdogo
 
hapana sufuria huipaki mafuta,unaiacha hivyo hivyo.
Kwa upande wa oven sijawahi kujaribu nikaona inatokeaje.
Kuhusu jani la mgomba,ni kwamba utaliosha halafu utalipitisha katika moto ili lilainike.
Utaligawa vipande kulinga na size ya bumunda unalopika,utachukua mchanganyiko kidogo na kuuweka katika jani la mgomba na ukunje kimakini ili mchanganyiko wako usimwagike.
everlenk ,pia waweza kufanya utafiti mwenyewe kwa kutumia jiko la oven,halaf uje kutuambia imefanikiwa kwa kiasi gani

Asante sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu, Katika mahitaji hujatuambia kiwango chake - unga kiasi gani kwa ndizi ngapi???

anhaaa sawa kabisa.
Unachotakiwa kufanya ni uhakikishe kiwango cha uji wa ndizi kinakua juu zaidi ya unga ili kuzuia bumunda lako kupukutika.
Pia kumbuka ni chakula cha asili kwa hiyo hata wakati bibi zetu wakitufundisha hawakutupa kiwango maalumu kati ya ndizi na unga,ila muhimu ni unga uwe pungufu kidogo ,hii pia itasaidia kupata ile sukari ya asili kutoka katika ndizi.
 
MABUNDA ni aina ya chakula cha asili cha Afrika ambacho ni rahisi kukiandaa. Pia kinajulikana kama MKATE WA NDIZI Kwa lugha nyingine.Ni chakula kilicho katika mfumo wa mkate ila hiki upikwa na ndizi na unga wa mahindi.

MAHITAJI
Ndizi mbivu zilizoiva vizuri au hata kukaribia kurojeka.

Unga wa mahindi ila nzuri zaidi kama utatumia unga wa dona.

Jani la mgomba.

JINSI YA KUPIKA
Menya ndizi zako na uziweke katika kinu kidogo kisha ziponde hadi zilainike na kuwa uji uji. Baada ya hapo, zitoe ktk kinu na weka katika bakuli kisha changanya unga wa mahindi hadi mchanganyiko wako ukolee.

Osha jani la mgomba vizuri na ulipitishe ndani ya moto ili lilainike.Kisha kata jani la mgomba vipande na chukua ule mchanganyiko wako wa unga na ndizi na uuweke katika jani la mgomba vizuri kisha ulisokote.

Weka katika sufuria au chungu na ubandike jikoni katika moto mkubwa kiasi.Funika na mfuniko wa chuma na juu paria moto kama unavyopika waki.

Subiri kwa dakika kumi au kumi na tano na ugeuze bumunda lako. Baada ya kuiva litakuwa gumu,hivyo tegua na ondoa mabaki ya majani ya mgomba na uache bumunda lako lipoe.

FAIDA ZAKE
Ni chakula kinachodumu kwa muda mrefu bila kuharibika (kuchacha).

Hakina madhara ya kemikali kama mikate ya viwandani.

Unaweza kula wakati wowote, waweza kunywa na chai au hata uji, pia usisahau juice.

"Onyesha ufahari kwa kula vyakula kwa kula vyakula vyenye asili ya mtanzania"

Maswali na ushauri vinaruhusiwa
Asante kwa elimu hii mujarabu mkuu. Sijawahi kula wala kuona bumunda zaidi ya kusoma tu kwenye vitabu vya zamani (1980's).
 
Vijana wamegeuza jina la chakula maridhawa cha asili kuwa kiungo cha mwili wa mwanamke.

Bumunda kwa lugha ya mtaani, ni uke uliojaziana na kuumuka vema. Kwa jina la wahuni wa Kizungu wanaita 'Camel toe'..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom