Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Vipimo

Unga wa ngano mweupe ................... 1 Kilo
Samli .............................................. 150gm
Chumvi ............................................3 vya chai
Maji ya moto yasichemke lakini ........... Kiasi
Mafuta Ya Zaituni (olive oil) ................ 4 vijiko vya supu
Samli tena ....................................... 200 gms
Iliki iliyosagwa ...................................1 kijiko cha chai

Namna ya Kutayarisha na kupika

1.Tia unga kwenye sinia au bakuli kubwa lililo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.

2.Unga uwe mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 20 30 ukiwa umeufinika ili unga ulainike.

3.Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa dakika 15 ukiwa umefunika bila ya kuingia upepo ndani.

4.Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.

5. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.

6. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.

7. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.

8. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kinamajimaji kidogo.

9. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote

10. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi.

11. Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.

Pika chapati kwenye frying pan, moto uwe wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati.

Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha chakula cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo.

Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifungue vizuri.

Zipange kwenye sahani huku unazifunika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.

========


Mahitaji:
  • Unga wa ngano nusu kilo.
  • Siagi vijiko 2.
  • Yai moja.
  • Chumvi kiasi.
  • Hiliki kama unapenda maana wapo ambao hawapendi.
  • Maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kukandia.
  • Mafuta ya kupikia.
Jinsi ya kuandaa

Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.

Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri weka yale maji ya uvuguvugu kidogo kidogo huku ukikanda, ukande mpaka uhakikishe haunati ila umekuwa laini.

Kukanda huko kutumie kama dakika 15 hivi ndiyo utalainika vizuri, ukimaliza katakata madonge kulingana na chapati unazotaka, hakikisha saizi inakuwa sawa kwa yote.

Ukimaliza, sukuma donge moja baada ya jingine. Ukishasukuma paka mafuta kisha weka donge pembeni mafuta yale yape nafasi ya kuingia ili kuifanya chapati iwe laini zaidi.

Ukishamaliza madonge yote chukua la kwanza sukuma anza kupika, pika chapati zako kulingana na jinsi ulivyokuwa ukizipaka mafuta moja baada ya nyingine.

Michango ya wadau
----
----
-----
 
jamaniii napenda chapatiiiii ziwe za kusukumaa.....au kumimina......wallah zinashuka vizuri mauongoni....ladha yake murua mdomoni....cant wait chai time! Thanks to mpishi kwa kunitengenezea appetite:A S 465:
 
Tatizo la chapati zinakula mafuta mengi sana....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…