Jinsi ya kupata mpenzi wa kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kupata mpenzi wa kweli

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 15, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Usiipe nafasi hofu
  [​IMG]
  Nyote mnapaswa kuwa na hisia zenye afya ili kujenga uhusiano wenye mafanikio. Kwa mfano, siyo dalili nzuri kama unakuwa kwenye uhusiano kwa sababu tu unahofu kuwa mpweke.
  Ni vibaya pia kwa mwanaume wako kusema anaupenda mchezo fulani kama anavyokupenda! Au ukiwa na msongo wa mawazo, usinase kwenye mtego wa mapenzi kwa kudhani unaweza kuwa tiba. Ni vizuri zaidi kutafuta mwanaume ambaye hahitaji utabibu.

  Chunga mwendo wako
  Jihadhari na chunga mwenendo wako kwani wanaume huwa makini na hushangazwa zaidi wakati wapenzi wao wanapokuwa wanafanya mambo ya ajabu. Unapozungumza naye muangalie usoni siyo sakafuni. Usimuulize maswali mengi kuhusu kazi yake, ingawa ni muhimu kujua anafanya kazi gani, kwani anaweza kuwa jambazi ati! Anaweza kudhani unataka kumchuna tu. Kama utashindwa kuchunga tabia yako, usishangae kama kukutana kwenu siku ya kwanza kunakuwa ndio mwisho wenu na usipojiangalia utajikuta tayari umemfunulia!

  Kufanana huleta mafanikio
  Hii haimaanishi unapaswa kuolewa na ndugu au mzazi wako, la hasha! Lakini unapoanza uhusiano na mtu, hakikisha unamfahamu kwanza kwa undani na jiulize mara mbili kama kuna vitu ambavyo mnalingana. Fikiria kuhusu uhangaikaji wake katika maisha (hata kama hana uwezo mkubwa kifedha, je, anajuhudi za kuzisaka hizo fedha ama la?), ujuzi na hata mapenzi ya dhati.
  Na fikiria sana kama malengo katika maisha yenu yanarandana. Nyote mnapaswa kukubaliana kuhusu athari pia za ndoa na kukabiliana nazo kama kuwa na watoto, kuishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa au hekalu. Vipo vitu unavyoweza kuvitambua kwa kukutana kwenu mara moja au mara mbili, na nyote mnapaswa kuwa wazi.

  Toa upinzani
  Mfanyie kila uwezalo mpenzi wako ili atambue kwamba unampenda, lakini usitake kuchukulia dalili zake za kuridhika na wewe mapema ndizo zikupumbaze na kumganda. Hapa sizungumziii kanuni – usisite kuijibu simu yake atakapokupigia au kwenda kukutana naye atakapokuita, hata hivyo, epuka kukutana naye sehemu ya uficho kama chumbani, lakini usijenge maisha yako kumzunguka yeye na wala usimlazimishe akakuelezea hisia zake.Hakikisha kwamba yeye ni nyongeza katika maisha yako na siyo muhimili wa maisha yako.

  Usiwe domokaya
  Najua wengi wenu mna mambo mengi ambayo mnaweza kuyazungumza, lakini yahifadhi mengine kwa ajili ya siku nyingine. Wanaume hupenda kusikia habari mpya kila mnapokutana.
  Wanawake wanapaswa kufikiria kuhusu hadithi mbili au tatu kali ambazo wanaweza kuzungumza wanapokuwa kwenye miadi, lakini wasivuke mpaka na kuanza kuzungumza mambo yanayowahusu wenyewe!

  Usinune
  ​[​IMG]
  Wanaume wengi huwa wanalalamika kwamba hupata wakati mgumu zaidi wanapokuwa na wapenzi wao, hasa katika siku ya kwanza ambapo hushindwa hata kuwabusu, kama huyo uliyenaye ndiye chaguo lako, basi usiwe mgumu, tabasamu na kama atakubusu usikwepeshe uso wako.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  sina la kuongeza, nawatakieni muwapate wa kufanana na nyie
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,658
  Trophy Points: 280
  Sasa hii ni namna ya kuishi na mpenzi au namna ya kumpata?
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hakuna formula bhanaa
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mapenzi hayana formula::::
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ahsante mkuu!
   
 7. O

  Obinna Senior Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha habari na yaliyoko ndani hayafanani!
   
 8. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si kwa mwanaume tu
  wanawake wenyewe mwanaume domokaya hatumtaki.
   
 9. PROF. ENG

  PROF. ENG Senior Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapateni sasa!!!
   
 10. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Tafuteni mtapata
  bisheni hodi mtafunguliwa
   
 11. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si kwa mwanaume tu
  wanawake wenyewe mwanaume domokaya hatumtaki.
   
Loading...