Jinsi ya Kuongeza Mtaji wa Kampuni Yako

Jinsi ya Kuongeza Mtaji wa Kampuni Yako

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
126
Reaction score
194
Umefungua Kampuni kwa mtaji wa 10M kama share capital mfano, baada ya kufanya biashara kwa muda Fulani unataka kuongeza Mtaji ufike 50M.

Hizi ni hatua za kisheria za kufuata.

1. Kikao Cha wakurugenzi (directors)
Wakurugenzi watakaa na kupitisha ajenda ya kuongeza Mtaji wa Kampuni.

2. Notice kwa wanahisa wote
Wanahisa wote watapewa taarifa juu ya mkutano na ajenda husika ya mkutano.
Notice iwe na reasonable time mfano siku 21 n.k

3. Kikao Cha wanahisa
Wanahisa watakutana na kupitisha special resolution ya kuongeza share capital
Hapa wataweka wazi kiwango Cha ongezeko na masharti ya kutolewa kwa hisa Mpya.

4. Marekebisho ya katiba ya Kampuni.
Katiba ni lazima ibadilishwe haswa kipengele Cha Nominal capital clause ili kuruhusu kiwango kipya Cha mtaji kionekane.

5. Kuwasilisha documents BRELA
Documents zote lazima ziwasilishwe Brela ndani ya siku 30.

Documents zitawasilishwa kupitia Brela ORS na Kisha utalipia Ada.

6. Kupewa cheti
Brela itatoa certificate on increase of share capital kama uthibitisho rasmi kwamba mtaji umeongezwa.

I hope this helps

Hey, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara, Kampuni na leseni.

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu kuongeza Mtaji wa Kampuni yako, unaweza kunitumia ujumbe WhatsApp kupitia namba hizi

0678131068
Your Favorite Lawyer.
 
Back
Top Bottom