Jinsi ya kumzunguka Dalali

Jinsi ya kumzunguka Dalali

Yaani kwa kifupi siwapendi hawa jamaa. Ni sawa na mpiga debe. Daladala kwa maandishi makubwa na Rangi juu limeandikwa Posta. Wewe na mibangi yako unakuja pigia watu kele Eti Posta hiyooooo kutwa nzima hiyo nayo kazi? Ujinga mtupu. Wanaowaendekeza ndio wajinga zaidi.
 
Kiukweli hawa jamaa wababoa na kila kukicha wanazidi kuongezeka na kujikita kila mahali. Hata sokoni ukienda mkulima/mfanya biashara hana nafasi ya kuamua bei bali madalali.

Siwapendi na nikishajua na deal na dalali siendelei tena na hiyo biashara.
Najua hata humu wapo, hapo juu nimewasoma na nitaendelea kuwasoma lakini siwapendi. Jitu zima linakaa mjini halifanyi kazi unasubiri mtu ahame uanze kudalalia chumba. Jenga yako.

Na sk hz tra inawatambua
 
Nakwambia akikukuta umemzunguka unalo.wengi ni wagomvi balaa.walishajichokea maisha.hata kuua wengine wanaweza.
 
Ujinga tu nyumba au kiwanja changu nikitaka kupangisha au kuuza naweka no zangu hazarani kwishakazi....


dalalai atakupigia simu atakuuliza unauza sh. ngapi ukisema milioni tano anakuambia nakuletea mteja wa milioni 10 kesho mimi yangu mbili na hatanii anakuletea kweli! ..dalali usimchukulie poa ndugu!
 
Labda kama hicho kiwanja hakijakamatwa na dalali mzoefu. Dalali mzoefu huwezi kumzunguuka kitoto hivyo!..yeye ndio anamiliki kiwanja na mwenye mali anamsikikiza yeye!..mikataba yote anatengeneza dalali na mwenye mali anasikiliza tu! Wewe umekutana na dalali underground

Nilisha fanikiwa kwa kutumia njia hiyo MWongozo kigamboni, dalali alinipeleka k wenye kiwanja na kunambia bei ya mwisho ni 16m baada ya kesho yake ku mafuta mwenye kiwanja tukamaliza biashara kwa 10m. Tangu siku hiyo dalali hanisalimii!
 
Mleta mada umeleta jambo zuri ...Ingawa kuna mapungufu makubwa juu ya ushauri wako wa kumzunguka aliyekusaidia kutatua maswaibu uliyonayo ...Njia ya kuzungukana inaudhi na inaamsha hisia za kumdharau na kumkejeli aliyepoteza muda wake kwa matumaini anafanya jambo likalomwezesha mwisho wa siku akapata chochote , kumbe wewe unamtumia kupata malengo yako kwa khadaa..una mawazo mabaya na hayana tija kwa maendeleo.,nimesema jambo ulilolianzisha ni zuri kwa maana ya kuwa madalali wanamchango mkubwa katika maendeleo na shughuli za kila siku za wanadamu...ndio maana kwenye biashara za kimataifa bila dalali huwezi kufanya biashara ,dalali ana uwezo wa kufanikisha biashara au kuihujumu...iwe hata ndogo kiasi gani...,,..kwa mantiki hiyo ingependeza basi serikali ingelifanyia kazi kwa kuwapa elimu stahiki ya udalali wahusika, na kuweka sheria kwa kuziboresha zilizoko pia wawe na ofisi maalum zitakazokuwa sehemu husika kwa malengo ya kuwatambua madalali halali, kwa mfano kama ni biashara za mboga mboga n.k sokoni kariakoo..au kama ni mahindi, tandale soko la mahindi n.k aliradi kunawekwa mpango mzima wa kuboresha mahitaji baina ya muuzaji na mnunuzi,kumbuka udalali ni AJIRA kamili.. Kazi za udalali zinapaswa kuboreshwa ili kuondoa na hata kuzuia utapeli usiwepo baina ya muuzaji na mnunuzi...

mchango wako nimeukubali lkn kiukweli kwa upande wangu mi siwapendi kbs hawa madalali ata kama wana mchango mkubwa ktk maendeleo na shughuli za kla cku za binadamu (kama ulivyonena) lkn kumbuka pia kuwa sometime wao ndio waangamizaji wa maendeleo ya mtu mungine, kwa mfano mdogo tu, umeuziwa kiwanja ml 20 alafu the end of day unackia mmiliki halali wa hicho kiwanja kapewa au alkuwa anauza ml 8 tu, c lazima utajickia kudhulumiwa hapa, wakati huohuo iyo ml 12 iliyoenda kwa dalali hakuna hata cent moja iliyoenda TRA au kulipiwa vat angali hii ni biashara kama biashara zingine, so nakuunga mkono kuwa imefika wkt madalali watambuliwe na walipe kodi km wafanyabiashara wengine? na watozwe vat kwenye zile asilia ( genji) zinazobaki kwao-
naunga mkono hoja
 
sema hiyo ni kesi broo akijua hyo dalali coz lazima ulipie nauli ya kukuonyesha eneo
 
Madalali wengi wanacheza na mazingira, ,,Huwezi kumzunguka kama wameshapewa kazi ya kuuza nyumba,na
mwenye nyumba vinginevyo itatengeneza maadui .!!

Niliwahi kusimuliwa dalali aliyepewa kazi n mzee mmoja amleteteea mteja wa milioni 30

Itakayozidi ya kwake.

Akanmleta wa.mill 40.. wakati wanaganwana mhindi i.akatoa mill 10 ya dalali
Mama mwenye nyumba akasema kwa kazi gani dalali apewe 10 ,mil wakati alijenga kwa mbinde .akakataa na mchezo ukaishiA haupo,,

Cha kushangaza hajawahi kuiuza mpaka leo
kila


Mnunuzi anayekuja wanaishia milion 5 tu,
Nyumba inanuka,,

Baadhi yao wanatumia nguvu za giza. ,ukiwakorofisha
 
Ukitaka kuwakwepa ni rahisi. Unamsomesha mwenye nyumba muelewane nyie wawili tu.
 
Ukitaka amani tafuta hicho kiwanja bila kumhusisha dalali. Ukimwingiza kwenye dili then utafute kumzunguka unalitafuta balaa mjini. Labda awe dalali learner

Madalali wapo kila mahali duniani. Labda useme tu wa hapa wengine wao ni wababaishaji tu ila hiyo ni kazi kama zingine. Kutafuta mteja wa kununua mali yako ni shughuli pia.
 
Madalali wengi wakibahatika wanatengeneza supper profity,yupo dalali alipewa dill na mwenye kiwanja katikati ya mji,makubaliano amletee mteja kwa m90,dalali akamwambia mwenye kiwanja waandikishane kwa wakili,na baadaye akamleta mtu aliyekubali kulipa m220,mwenye nyumba alitaka kuhamaki lakini akalegea kwa mkataba walowekeana,huwezi mpiga chenga dalali mjanja
 
Habari ya asubuhi wana jamvi, yaani mimi nawapenda sana na nina wa wahitaji sana kama kuna madalali hum u jamvini wa nyumb arusha anI pm nimpe kazi arusha nina . Karibuni madalali niwape kazi usa river na sakina
 
Tatizo sio madalali, tatizo linaanzia kweli sisi wamiliki wa bidhaa/vitu. Hata kama ni simu ya mkononi.

Mfano: unahitaji kuuza mali yako kwa sh. 200,000/= ukatangaza offer hiyo, then dalali akakwambia nipe dk. 2 nakupa sh. 220,000/= je utakataa??? Sasa uliza kauza hiyo mali sh.ngapi?? Unaweza kufa kwa pressure, kauza zaidi hata sh. 300,000/= lakini wewe tafuta mteja wa sh. 200,000/= humpati ng'o hata mwezi mzima.

Biashara zimeshaharibiwa na madalali, saiv mpaka maofisini kuna madalali. Huduma pia zina madalali.

"Madalali ni unkwepable" utakutana nao tu hata uwakwepe kiasi gani. Ila nawachukia saaaanaaa!!!
 
ilinitokea kama hii, nimepatania bei ya kununua gari kwa ajili ya biashara, wakati wa kukabidhiana documenti za gari na kuhamisha umiliki, kumbe jamaa ni dalali na mwenye gari ni mshikaji wangu sana,dalali alipiga cha juu milioni 2 na nusu.
 
Back
Top Bottom