Jinsi ya kumrudisha mtu aliyeuliwa na wachawi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Wachawi sio watu wa kuwachekea hata kidogo Unapoipata dawa yake wakomeshe kisawa sawa kama wao wanavyotukomeshaga sisi.

JINSI INAVYOKUWA...

Wachawi wanapomuua mtu huwa wanakuwaga na kahofu fulani na wao msidhanie kwamba ndo wanajifanyaga makonk sana. Aaah waapi ni waoga kama kunguru hao.
Wanapomuua mtu huwa wanasikilizia kwanza ili wajue. Je? Tunafuatiliwa au hatufuatiliwi?

Ndio maana wanapomuua mtu huwa wanamuweka kwanza kwa siku saba bila kumdhuru au kumfanya chochote. Siku saba zikipita kimya Hapo sasa ndo wanaanza kuwa na imani kwamba hakuna mtu wa kutufuatilia. Ndipo wanapoanza kumchokonoa chokonoa jinsi wanavyotaka huyo mateka wao.

Kwanza wataanza kumkata ulimi ili asiweze kuongea chochote tena. Na wakishamkata ulimi wanamuhifadhi kwanza kama aliuliwa kwa ajili ya kuliwa watasubiria Ifike siku ya arobaini. Nyie huku mnafanya atobaini ya marehemu wao huko wanamla nyama huyo marehemu.

Lakini kama watakuwa walimuua kwa ajili ya kumtumia tu huwa wanamfanyisha kazi mbali mbali nyepesi na ngumu zooote unazozijua wewe. Hao ndo wachawi na tabia zao chafu

SASA MWANZO NI HUU...

Ile siku ya msiba wachawi huwa wanamficha marehemu nyuma ya Mlango mkubwa wa kutokea balazani.
Yaani yule mtu mwenyewe hasa wa kwelikweli ndio wanamfichaga huko nyuma ya mlango. Nyie huku mnalizana na kuililia maiti iliyoko chumbani. Kumbe mnaulilia mgomba tu. Mtu mwenyewe Original yupo nyuma ya mlango. Mzimaaa wa afya tele hajachubuka popote. Anashangaa tu watu mnavyolizana ovyo na kumtaja taja tena anawaona anatamani kutoka pale na kusema ila anashindwa anakuwa chini ya ulinzi mkali sana.

Mwenye uwezo wa kumuona pale ni mtoto mdogo asiyeweza kuongea na mtu yeyote mwenye kuchanjia dawa za kuona wachawi basi. Lakini nyie wengine hamuoni chochote mnafikiria ni msiba wa kweli kumbe ni mazingaombwe matupu. Mnapita mlangoni ndugu yenu anawaita mje kumsaidia lakini hamsikii.. Sasa leo nitaitaja dawa nyepesi na ya haraka ya kumrudisha huyo ndugu yenu aliyeuliwa kichawi.

VIFAA VINAVYOTAKIWA...

*Chungu kimoja cheusi. Vile vyungu vya kupikia mboga.

*Maji safi ya kutosha kujaa kwenye chungu hicho. ( Hapa kwenye maji safi tuelewane kidogo. Ninaposema maji safi sio yale ya chupa ya dukani. Hapana mimi namaanisha maji haya haya tunayoyatumiaga kila siku ila yawe masafi tu).

TUENDELEE...

Mkishaandaa chungu chenu cheusi na maji yenu. Tulieni acheni papara na fungeni midomo yenu musitangaze, tangaze kwa kila mtu kuwa mnataka kufanya jambo. Mtashtukia chungu kimevunjika ghafla na maji yamemwagika alovunja na alomwaga musimjue. Tulieni tuliiii nyie endeleeni kuomboleza msiba tu.

Kumbe mna lenu moyoni Muda wa mazishi ukifika nendeni mkazike. Mkishamaliza kuzika mkarudi nyumbani tu hapo sasa ndo kwenye kazi.

KAZI INAANZIA HAPA...

Inatakiwa muuvae moyo wa ujasiri ikiwezekana muwaambie watu live bila kupepesa macho kwamba matanga hamna kila mmoja arudi kwao. Ili nyie mfanye mambo yenu. Watu wakishaondoka zao mkabakia wenyewe hapo sasa. Kama kuna watoto wadogo ndani tafuteni pa kuwapeleka kwanza wakakae kwa muda wa siku tatu tu. Hapo mbakie watu wazima wenye akili zenu vichwani. Maana mtajua kwamba wazo lenu ni moja.

Kwasababu mtakapoanza kufanya dawa haitakiwi kelele yoyote ndani. Yaani haitakiwa kuongeleshana. Inabidi mchuniane kwa muda wa siku tatu hakuna cha salamu wala kujuliana hali. Kila mtu alale akiamka aendelee na ishu zake. Lakini kusemeshana marufuku. Mwenye kwenda kazini aende, wa shuleni aende, wa kwenye biashara aende na wa nyumbani ashinde tu lakini kusemeshana hata kwa salamu ndani ya nyumba hiyo marufuku kabisa. Ndio maana nikasema watoto wahamishwe na kama mnakaa na chizi basi nae mumtafutie makazi ya muda. Haitakiwi heka heka kabisa humo ndani.

JINSI YA KUFANYA DAWA...

Jazeni maji katika chungu cheusi na mkiweke nyuma ya Mlango mkubwa wa kutokea balazani.
Mkishamaliza kukiweka tu kila mmoja akaendelee na shughuli zake. Hapo mwendo ni ule ule marufuku kuongea chochote hata kujichekesha chekesha marufuku Mnacheka nini wakati mwenzenu anateseka inabidi mumkomboe, sasa kinachokupa wewe furaha kitu gani na kuanza kujichekesha ovyo kama chizi si mtavunja masharti ya dawa sasa.

Hamna kucheka mtu fungeni midomo yenu. Kama unajiona utacheka toka ndani kakae mbali kabisa huko usubirie usiku uingie kulala tu.

MATOKEO...

Mtaacha chungu hicho kikae siku tatu huko nyuma ya Mlango. Ikitimia siku ya tatu muende nyuma ya Mlango mkatazame. Mtashangaa kumkuta mtu aliyekufa mukamzika kwa mikono yenu. Yupo mzimaaaa wa afya...

HIYO NDIO DAWA NYEPESI NA RAHISI SANA INARUDISHA MTU KWA SIKU TATU TU. ILA UGUMU WAKE NDO HUO WA KUISHI NDANI MKIWA KAMA MABUBU KWA MUDA WA SIKU TATU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom