Jinsi ya kumpata mpenzi wako wa zamani

Fernando sucre

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
293
345
Wakuu kipindi cha nyuma niliwahi pata binti wa Mbeya nikaishi naye huku nikiwa sijui ndugu yake yoyote.

Kuna kipindi akawa na kama kiburi ukimsemesha anaweza jibu ama la, nikavumilia siku moja asubuhi akakusanya vitu vyake huyo akasepa.

Bila kujua mimi siku hiyo nilipanga nihame hapo.mpango wa kuhama nilishindwa kumwambia coz alishaanza kiburi.

Kumbe jioni alirudi pale akakuta nimehama akanipigia na kuniambia ni mjamzito nikamwambia poa ila kwakua alishabadilika sikutaka kumuambia nilipohamia.

Akawa anapiga akijichekesha ili nimrudie wapi,baada ya miezi kadhaa akaniomba nauli arudi kwao Mbeya nikamtumia.

Akiwa Mbeya akasema kajifungua mtoto anaitwa Bahati wa kike.nikachangia mwanzoni matunzo ya mtoto kule,nikaja kusafiri kwenda nje nikakaa miaka 3 kurudi tigo washauza line yangu,

Nikasajili line nyingine kwa kuwa namba ya mama watoto nilikuwa nayo kichwani nikapiga anapokea mtu mwingine,anasema kauziwa na tigo kucheki jina tpesa kweli jina si la mama watoto.

Sasa kwao sipajui huko mbeya na hata yoyote wa kumpata.nisaidieni mawazo wakuu.
 
Angekuwepo ningemuuliza dada
Inawezekana hata hicho kiburi kilikuwa kinatokana na mimba...Hapo ulipokuwa unaishi naye kabla ya kuhama hakuwa na rafiki au mtu aliyemzoea sana? Kama yupo nenda kwa huyo huenda akakusaidia.
 
Weka majina yake kamili, mara kwa mara anzisha uzi maana leo mtu anaweza asione next time akauona, na hongera sana kukumbuka damu yako, tia nia utampata, ikibidi kaweke na matangazo radio zinazosikilizwa sana zamani radio one walikuwa na kipindi cha kutafutana sijui bado kipo?
 
Wakuu kipindi cha nyuma niliwahi pata binti Wa mbeya nikaishi naye huku nikiwa sijui ndugu yake yoyote.kuna kipindi akawa na kama kiburi ukimsemesha anaweza jibu ama LA.nikavumilia siku moja asubuhi akakusanya vitu vyake huyo akasepa.bila kujua mm siku hio nilipanga nihame hapo.mpango Wa kuhama nilishindwa kumwambia coz alishaanza kiburi.kumbe jioni alirudi pale akakuta nimehama akanipigia na kuniambia ni mjamzito nikamwambia poa ila kwakua alishabadilika sikutaka kumuambia nilipohamia.akawa anapiga akijichekesha ili nimrudie wapi,baada ya miezi kadhaa akaniomba nauli arudi kwao mbeya nikamtumia.akiwa mbeya akasema kajifungua motto anaitwa bahati Wa kike.nikachangia mwanzoni matunzo ya mtoto kule,nikaja kusafiri kwenda nje nikakaa miaka 3 kurudi tigo washauza line yangu,nikasajili line ingine kwakuwa namba ya mama watoto nilikuwa nayo kichwani nikapiga anapokea MTU mwingine,anasema kauziwa na tigo kucheki jina tpesa kweli jina si LA mama watoto.ss kwao sipajui huko mbeya na hata yoyote Wa kumpata.nisaidieni mawazo wakuu
Kwahyo saivi unamtaka mke au mtot wako!? Mana kama ni mtot Damu ako haiwez kupotea japokua itakawia.
 
Inawezekana hata hicho kiburi kilikuwa kinatokana na mimba...Hapo ulipokuwa unaishi naye kabla ya kuhama hakuwa na rafiki au mtu aliyemzoea sana? Kama yupo nenda kwa huyo huenda akakusaidia.
Kumbe ujawepesi husababisha kibri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom