Jinsi ya kumfunza mtoto mdogo kuongea vizuri

Navojua watoto wa kiume wanachelewa kuongea kdogo kuliko wa kike,sidhani kama ni tatzo kw umri alonao,ataongea tu with time,
 
Itabidi nami wa kwangu akifikisha umri huo baby class ihusike...
Ila vipi siku za kwanza kwanza uliwezaje kupata amani..
Si unajua mtoto wa kwanza mzazi unavyokua na uoga uoga

Mpaka leo hii sina amani mkuu lazima nipige simu mara kwa mara nijue anaendeleaje maana ni mtundu sana kama alivyo wako ila ananipa faraja sana ndo mtoto wangu wa kwanza...hahaha kama jamaa alivyosema nilikuwa nna hamu sana aanze shule ili nilipe ada
 
Come on mod...huu uzi hujautendea haki huwezi kuuleta huku MMU...
At least upeleka JF doctor ila huku kwenye mapenzi ebu review hii move.
Mbeky
 
Mpaka leo hii sina amani mkuu lazima nipige simu mara kwa mara nijue anaendeleaje maana ni mtundu sana kama alivyo wako ila ananipa faraja sana ndo mtoto wangu wa kwanza...hahaha kama jamaa alivyosema nilikuwa nna hamu sana aanze shule ili nilipe ada

I can't wait ikifika wakati wangu
 
Kama una mashaka mpeleke kwa doctor wa watoto.

Kuna taizo la ulimi kuungana na mdomo; kuna mtoto wa ndugu yangu alikuwa na hilo tatizo hosp wakamkata. Ulimi unakuwa hauwezi kuzunguka.

Otherwise watoto utofautiana; kuna wanaowahi kila kitu na kuna wanaochelewa.
 
Leo ndio mara ya kwanza nasikia mtu ana hamu ya kulipa ada...te te te..kweli mtoto ana raha yake....

Mpaka leo hii sina amani mkuu lazima nipige simu mara kwa mara nijue anaendeleaje maana ni mtundu sana kama alivyo wako ila ananipa faraja sana ndo mtoto wangu wa kwanza...hahaha kama jamaa alivyosema nilikuwa nna hamu sana aanze shule ili nilipe ada
 
Mbeky

Binafsi siamini kabisa dhana ya "mtoto wa kiume anachelewa kutembea, mtoto wa kiume ana ulimi mzito" n.k

Uchangamfu na wepesi wa mtoto unategemeana sana na afya yake kiakili, kimwili pamoja na mazingira unayomlelea. Mtoto ambae yupo mwenyewe mwenyewe na wazazi ambao sio active anakuwa slow naturally kwasababu hakuna kinachomsukuma kutaka kujua zaidi.

1. Akili.
Akili ya mtoto inapokuwa imara na inafanya kazi ipasavyo (kuendana na umri wake) anakua na hamu ya kujifunza na kufanya zaidi wakati wote.

Hapa maziwa ya mama yanahusika sana kuimarisha ukuaji wa ubongo wa mtoto. Nimeshuhudia kwamba wadada/mama wengi walioajiriwa hawawezi kunyonyesha 'EXCLUSIVELY'kwa miezi sita kwasababu baada ya miezi mitatu wanarudi makazini mtoto anaanza kulishwa vitu vingine. Wengine hata sio waajiriwa ila mtoto wa miezi 2-3 tayari ataanza kupewa uji kwa kisingizio cha kutoshiba/mama kutokuwa na maziwa ya kutosha. Kunywa wewe huo uji, mtoto aupate kwenye maziwa.

2. Kimwili.
Hapa tunarudi tena kwenye afya ya mtoto. Mtoto mwenye afya nzuri mwili wake unakuwa imara na anakuwa mwepesi kupiga hatua kwenye ukuaji wake tofauti na mtoto mwenye afya dhaifu. Again, maziwa ya mama ndio chakula chenye ubora zaidi kwa mtoto chini ya miezi sita. Ukijitahidi utaona maendeleo ya mtoto yanavyokuwa mazuri.

3. Mazingira.
Mtoto hawezi kuwa 'ACTIVE' kama hamna watoto wengine wa kumchangamsha na wazazi sio active. Unamuacha mtoto na dada wa kazi, ye kazi yake kumuweka mtoto mgongoni muda mwingi ili asimsumbue, kucheza nae ni kwa bahati sana. Mzazi nae akirudi amechoka sana sana atakaa amembeba mwanae basi amemaliza.

Ukimuongelesha ni kidogo, na unamuongelesha kitoto.

4.Kudanganyika na ujuaji.
"Kwanini unamkalisha mtoto bado mdogo hivyo, anaumia kiuno.Kwanini humvalishi mtoto nguo, watoto hawasikiagi joto ati." Mtoto analilia kukalishwa tangu mdogo (miezi 3-4) humkalishi unangan'ania kumpakata.

Badala ya kumsaidia mtoto hayo yote yanamlemaza na kumfanya atulie kwenye 'stage' moja kwa muda mrefu kuliko anavyotakiwa au hata kurudi nyuma.

Kwa uzoefu wangu hamna ajabu yoyote kwa mtoto wa kiume kutembea kabisa akiwa na miezi 10-11, ama kuongea na kuelewa maneno madogo madogo(mama, baba, lete, asante, poa) kuelewa ukimtuma ama ukimkataza kitu kuanzia miezi 11 na kuendelea.

Ongeza bidii ya kumchezesha chezesha na kumsemesha uone tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Kama una mashaka mpeleke kwa doctor wa watoto.

Kuna taizo la ulimi kuungana na mdomo; kuna mtoto wa ndugu yangu alikuwa na hilo tatizo hosp wakamkata. Ulimi unakuwa hauwezi kuzunguka.

Otherwise watoto utofautiana; kuna wanaowahi kila kitu na kuna wanaochelewa.

Mkuu sina shaka na uwezo wake wa kuongea sema nilikua natafuta mbinu ya kumfundisha aweze kuongea vzr..
 
[MENTION=147984]

Kwa uzoefu wangu hamna ajabu yoyote kwa mtoto wa kiume kutembea kabisa akiwa na miezi 10-11, ama kuongea na kuelewa maneno madogo madogo(mama, baba, lete, asante, poa) kuelewa ukimtuma ama ukimkataza kitu kuanzia miezi 11 na kuendelea.
Lizzy hili hata mimi nakubalina nalo mwanangu kaanza kukaa akiwa na miezi 3 watu wakesema ataumia cause mtoto wa kiume kukaa ni mpaka miezi 5
alianza kuonesha dalili za kuanza kutembea akiwa na miezi 9..
 
Last edited by a moderator:
Umri bado! ila ni vzr aanze cheza na watoto wenzie hasa wanaoweza ongea! 6month utamkimbia kila kitu anajua
 
Asanteni kwa uzoefu wenu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom