Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

MFALME WETU

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
4,735
Reaction score
11,343
Huyu jamaa ananitia hasira sana jamani nais ntamfanya kitu kibaya.

Kuna siku nilipost nauza simu yangu [Samsung Note 10+] kule kwenye jukwaa la matangazo maana nilikua siitumii sasa kwenye harakati za kutafuta mteja nikaamua kumshirikisha huyu rafiki yangu akadai nimuuzie.

Nikasema fresh haina shida ila nikampa condition aje na pesa yote cash maana masuala ya kudaiana hela siyawezi akasema sawa.

siku anakuja kuchukua simu ilikua tarehe 18 December 2022 nakumbuka alinipigia simu kuniuliza nilipo nikamwambia nipo Oysterbay bar xxxxxx akanambia anatokea kuja kuchukua simu kama tulivokubaliana nikamwambia sawa ila sipo nayo apa ipo nyumbani.

Ikabidi nimuunganishe na dogo langu pale home ampe jamaa simu mi nikaendelea kumwagilia moyo.


To cut the long story short

Mshikaji alienda akalipa hela nusu ya tuliokua tumekubaliana 250k/500k.. kwa kuwa dogo anamjua jamaa ni rafiki yangu hakuona haja ya kunijulisha jinsi transaction ilivoenda akampa jamaa simu akaishia zake.

Sasa kesho yake dogo ananikabidhi pesa ndo nagundua jamaa kanifanyia uhuni contrary na makubaliano yetu akanipiga sound kuwa atanilipa hela iliyobakia before 25th December 2022, nikamwambia fresh ila nikamsisitiza anilipe iyo hela maana kashaenda kinyume na makubaliano akasema sawa nisiwaze.

Ilivofika tarehe 25 sikumcheki maana mambo yalikua mengi ukizingatia ni sikukuu nikajua atajiongeza lakini wapi. Nikamcheki tarehe 27 akanambia hajapata hela nimsikilizie akisain boom atanilipa hela yangu yote nikasema fresh..kasain boom tarehe 09 January kumcheki akawa hajibu text wala kupokea simu. Akaja kunijibu kesho yake kuwa hela ya boom yote kalipa kodi ya nyumba hela imeisha akaniahidi nimvumilie aombe hela nyumbani anilipe.

Baada ya apo napigishwa sound kama mtoto tena mjinga nisiejielewa, sijalipwa ata mia na nikimpigia simu hapokei na akipokea anajibu kwa kujihami sana plus text zenyewe ndo anajibu kama hivi jamani pesa yangu mwenyewe inanitesa

Watu kama hawa tunadeal nao vp au nivae roho ya unyama nikodi polisi nimuibukie anapokaa nichukue simu yangu then nivunje urafiki.

Kinachoniuma ananijibu kwa dharau sana na anajibu au kupokea simu kwa kujiskia na hajanilipa hata mia kwenye hio hela iliyobakia

Nina muda mrefu sana sijawa na stress kias hiki.

Ingekua mchana ndo kanijibu hivi huyu dogo leo angejuta ashukuru Mungu ntaamka hasira zikiwa zimeisha.

Naombeni ushauri na mbinu za kuweza kupata hii hela au simu kutoka kwa huyu rafiki yangu

Mnisamehe kwa uandishi wangu mbovu maana huyu jamaa kanivuruga sana
Screenshot_20230205-201850.jpg
 
Kesi iyo..

Mi nishaachana na madogo wapumbavu kama hao wengine eti anakuzungusha ikipita mwaka anahisi umesahau anakuja Tena kwa shida ..Hivi karibu jamaa jirani nimempa 30k achukue ishu fulani maana anauza chips aliniambia trh 20 December atanipa ila mpaka leo hajanilipa na Yale mawasiliano ya awali kakata ..

Dunia Ina tatizo hili la kutokuwa muaminifu sijui kwa nn..
 
Aloooh!! Ama kweli hakuna anayezaliwa na roho mbaya ila binadamu tunafundishana.
Bora ingekua ata nimemwazima maana mi rafiki zangu huwa siwakopeshi huwa nawasaidia tu wakikwama nahesabu kama nmetoa sadaka suala la kurudisha au kutorudisha huwa nawaachia wenyewe nikiamini namimi ipo siku ntakwama wakanisaidia.

Lakini hadi kwenye business tena jamani ndo tufanyiane hivi
 
Chukua ubani Mashtakhaa
choma unuie " Kama mimi Ditto nguku bendu wa zabanga hii simu Samsung Note 10 niliinunua kwa jasho langu na nmedhurumiwa, ikiwa ni haki yangu ntaipata kama sio haki Inshaallah"

afu potezea
mshukuru Mwenyezi Mungu Allah subhanah wa Taala
 
Huyu jamaa ananitia hasira sana jamani nais ntamfanya kitu kibaya.

Kuna siku nilipost nauza simu yangu [Samsung Note 10+] kule kwenye jukwaa la matangazo maana nilikua siitumii sasa

Mnisamehe kwa uandishi wangu mbovu maana huyu jamaa kanivuruga sana View attachment 2507621
Simple mbona report police wizi wa kuaminiwa
 
Halafu kanaandika kipumbavu sana
Chukua hatua kali. Mletee noma, unakuaje na urafiki na mtu anaandika sms namna hiyo? Hiyo ni indication tosha kuwa ni kamtu kapumbavu.
Mtoto mdogo anakusuambaje?
Na wewe zembe..nakupa za uso.
Mkuu kumdai mtu hela ni kazi sana kwa kweli ngoja tu nakubali kuwa mimi ni dhaifu ukizingatia alikua rafiki yangu pete na kidole. Najuta
 
Chukua ubani Mashtakhaa
choma unuie " Kama mimi Ditto nguku bendu wa zabanga hii simu Samsung Note 10 niliinunua kwa jasho langu na nmedhurumiwa, ikiwa ni haki yangu ntaipata kama sio haki Inshaallah"

afu potezea
mshukuru Mwenyezi Mungu Allah subhanah wa Taala
Mimi ni mkristo.. vp hii inaweza fanya kazi niitumie kesho
 
Back
Top Bottom