Kuna njia tatu.
1. Kusoma label
2. Kujaza maji mwenyewe kwa vipimo kama ndoo au dumu ambalo unajua ujazo wake.
3. Kwa njia ya mahesabu kwa maana kupima urefu, upana na kina. Mfano
Ujazo (litres) = Urefu (cm) × Upana (cm) × Kina (cm) gawanya kwa 1000
👉 Kwa mfano:
Urefu = 80 cm
Upana = 60 cm
Kina = 50 cm
80 × 60 × 50 = 240,000 cm3
Chukua 240,000 gawanya kwa 1000 = 240 litres.
Kwa freezer hili litakua na ujazo wa lita 240.