Jinsi ya Kujua anae Angalia sana Akaunti yako ya Facebook

Amanijoseph86

Member
Jun 18, 2015
13
18
Habari wana JF leo ningependa kushare nanyi makala kutoka katika tovuti ya Tanzania Tech, Njia hii inaonekana kuwa bora na ya haraka kwa kila mtu mwenye kompyuta.

Kwa kuanza basi kumbuka ni lazima uwe wewe ndio mwenye akaunti hiyo ya Facebook kwani bila hivyo hutoweza kufanikisha hatua hizi, kwa maneno mengine ni kwamba ni lazima uwe umeingia (ume-login) kwenye akaunti yako hiyo unayotaka kujua nani amekua akitembelea mara kwa mara. Pia ni muhimu kujua kuwa ili uweze kufanya hatua hizi unatakiwa uwe umeingia (ume-login) kwenye akaunti yako hiyo kwa kutumia kompyuta iwe ni laptop au desktop.

Baada ya kuhakikisha hayo yote hapo juu basi twende moja kwa moja tukaangale jinsi ya kuangalia nani anae angalia sana akaunti yako ya facebook. Kwa kuanza ingia kwenye akaunti yako ya facebook kisha bofya kwenye profile yako au page au group unalotaka kujua nani amekua anatembelea sana, baada ya hapo hakikisha page hiyo au akaunti yako imemaliza kusoma (kuload) vizuri kisha futa hatua hizo hapo chini.

Kwenye Keyboard ya kompyuta yako (laptop au desktop) bofya vibonyezo Ctrl pamoja na U kwa pamoja yaani (Ctrl+U) au unaweza kutumia Mouse ya kompyuta yako kwa kubofya kibonyezo cha Mouse cha upande wa kulia (Right Click) kisha chagua sehemu iliyoandikwa view page source hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye page yenye code za akaunti yako. Subiri page hiyo imalize kusoma (ku-load) kisha bofya tena kwenye keyboard yako Ctrl pamoja na F (Ctrl+F) ukiwa kwenye page hiyo yenye code za akaunti yako.

Baada ya hapo utaona kwenye kioo chako box limefunguka upande wa kulia juu copy hizo code hapo chini (kucopy bofya view raw) kisha weka (paste) kwenye box hilo na bofya Enter kwenye keyboard yako.

InitialChatFriendsList

Baada ya hapo utaona namba nyingi zikianza mbele ya maneno hayo baada ya neno List, namba hizo zinakuwa na tarakimu 15 copy namba hizo kisha andika www.facebook.com/ kwenye sehemu ya kuandika link kwenye browser yako kisha weka namba hizo 15 mbele ya mkato yani www.facebook.com/123456789012345 kisha bofya Enter kwenye keyboard yako.

Baada ya hapo utaona (profile) akaunti ya mtu ambae ndio anatembelea sana profile page yako kwenye mtandao wa facebook, kumbuka namba ya kwanza ndio inayo wakilisha anaetembelea sana kama ukiangalia namba hizo ziko nyingi inamaanisha zimejipanga kwa mtu wa kwanza mpka wa mwisho, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kutembelea Tanzania Tech na kuangalia video ili kujifunza zaidi.
Ui
Natumaini imeweza kukusaidi...
 

Attachments

  • upload_2017-2-1_11-49-28.gif
    upload_2017-2-1_11-49-28.gif
    42 bytes · Views: 99
Alafu nikishajua'nini napata sasa!!!
Ben usifikirie hii kwa namna ya tofauti, hii inakusaidia kujua watu wanaokufuata kwenye mtandao wa kijamii ni wa aina gani, kwa njia hii kama wewe ni mfanya biashara au mtu flani mwenye nyazfa flani kwenye jamii itakusaidia kujua your number 1 fan ni nani. Ukweli ni kwamba nadhani kila mtu anapenda kujua hilo uwe ni mfanya biashara au mtu wa kawaida.
 
Ben usifikirie hii kwa namna ya tofauti, hii inakusaidia kujua watu wanaokufuata kwenye mtandao wa kijamii ni wa aina gani, kwa njia hii kama wewe ni mfanya biashara au mtu flani mwenye nyazfa flani kwenye jamii itakusaidia kujua your number 1 fan ni nani. Ukweli ni kwamba nadhani kila mtu anapenda kujua hilo uwe ni mfanya biashara au mtu wa kawaida.
Uko sahihi kwa ilo,ungeweka basi kama hitimisho
 
nlifungua vizur mpka kweny hzo code nikaziona..ila nlipobonyeza control F box juu likafunguka likiwa halina kitu....
 
baada ya hapo utaona kwenye kioo chako box limefunguka upande wa kulia juu copy hizo code hapo chini (kucopy bofya view raw) kisha weka (paste) kwenye box hilo na bofya Enter kwenye keyboard yako.

hii sentensi sijaielewa vizuri, naomba unifafanulie vizuri
 
K
baada ya hapo utaona kwenye kioo chako box limefunguka upande wa kulia juu copy hizo code hapo chini (kucopy bofya view raw) kisha weka (paste) kwenye box hilo na bofya Enter kwenye keyboard yako.

hii sentensi sijaielewa vizuri, naomba unifafanulie vizuri
kajojo copy code hizi ( InitialChatFriendsList ) kisha endelea kufuata maelekezo
 
hii ni ya kujua watu unaochati nao freequently sio wanaotembelea profile yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom