Jinsi ya Kujiokoa na Mlipuko wa Bomu la Nyuklia (nuclear blast/attack)

Msherwa

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
1,335
1,225
Amani katika uso wa dunia imeendelea kupungua huku maendeleo mapya ya binadamu miaka 65 tu iliyopita yamepelekea amani ya dunia kuwa katika kiwango cha INAYOWEZA KUTOWEKA MILELE.
Hali hii imetokana na mataifa yenye resource za kutosha kuamua kutumia nguvu zao zote kutafuta njia ya kuangamiza watu wengi zaidi kwa mara moja, hapo ndipo nuclear race ilipoanza na kutufikisha hapa tulipo leo, ambapo kwa hali ya mahusiano ya mataifa makubwa inayoendelea sasa, Dunia imeshapoteza amani na kinachosubiriwa ni button chache kubonyezwa na dunia ya amani ikabaki kwenye historia

Mataifa mengi yanayokua, hayajawa tayari au hata hayajawa na ushawishi wowote kuhusu mustakabali mzima wa amani duniani, Mataifa machache yenye nguvu yametumia mabavu na ushawishi kuwaaminisha binadamu kwamba wao wanaweza kuishika amani ya dunia na wakaitunza

Hilo liliendelea kuwa kanuni hadi kufika mwaka 2001 ambapo Dunia ilianza vita mpya dhidi ya ugaidi iliyotufikisha hapa ambapo hata ashuke nani duniani, uwezekano wa vita kubwa kuliko zote katika historia ni mkubwa kuliko hata uwezekano wa ugunduzi wowote mpya wenye faida

Ni vyema tukajipa elimu ndogo mapema ili kujiandaa kwani kama vitabu vya dini vinavyosema "itakuwa ni kama kuja kwa mwizi ndani ya nyumba" hakutakuwa na taarifa!!


Jinsi ya kujiokoa na bomu la Nyuklia. (endapo nafasi hiyo inakuwepo)

  1. Ifahamike kwamba, kwa yeyote ambaye atakuwa katika ground zero wakati detonation inatokea, hatokuwa na uwezekano wa kutumia hata moja ya njia hizi, Kwani ni hakika huwezi kusurvive nuclear attack ukiwa ground zero, labda kama uwe shielded KWELI!!. Sasa kwa yule ambaye atakuwa maili kadhaa toka ground zero, dalili za kwanza za attack ni mwanga mkali (flashligth) ambazo kwa kawaida hutembea kwa speed kali kuliko fallout (mabaki ya bomu na debris zingine)
  2. Kama umekwishajua uelekeo wa ground zero toka ulipo, USIJARIBU KUIFUATA shelter (eneo la kujikinga na mionzi) iliyopo karibu ya/ au katika mwelekeo ule, ina maana kwamba, toka mwanga unapoonekana hadi madhara kukufikia inachukua muda kidogo kulingana na mahali ulipo. Tumia muda huu ku-move haraka uwezavyo ukielekea upande wa mbali na ground zero.
  3. Fungua mdomo wako wazi (achama) wakati ukikimbia ili kuepusha ngoma za masikio (ear drums) kupasuka kwa sababu ya presha inayokuwepo wakati huo.
  4. Fallouts ndio kitu cha hatari zaidi wakati huu, na zinaweza kuendelea kuleta madhara makali kwa mwili wa mwanadamu hata baada ya siku 19 toka mlipuko. Hivyo ni vyema kuhakikisha vitu vinavyofanana na mchanga mwembamba angani visitue ardhini na kukukuta ukiwa un-shielded, kipimo pekee cha mwelekeo wa fallout ni upepo, kimbia kuelekea upepo unakoelekea hii inakuweka mbali na danger zone (hata kama ni mita 3 mbele, zaweza kuwa ndio msaada wako)
  5. Nuclear fallout huendelea kuwa na mionzi sumu (radioactive rays) kwa muda hata wa wiki mbili (2) toka zilipuke (hizi ni zile aggressive zaidi kwa mwili wako, ingawa mionzi huendelea kusambaa kwa muda mrefu zaidi ya huo huku ikizidi kupungua nguvu) hii ina maana kwamba kama utakuwa umejiokoa katika mlipuko, UNAHITAJI KUWA ULISHAJIPANGA KWA CHAKULA NA MAJI. Nafasi hiyo ipo sasa tu, kwani baada ya tragedy hii kuanza nafasi hiyo itakuwa haipo, na shughuli yoyote nje ya shelter itakuwa na madhara tu.
  6. Ardhi ndio ngome pekee ya asili dhidi ya nuclear attacks, Ni nyema tukaanza kufikiria upya uwezekano wa Watanzania kumiliki mahandaki makubwa kiasi yenye huduma za msingi kama njia pekee ya tahadhali. Ikiwa wewe unaweza sasa kutengeza shield hiyo, ANZA SASA, MUDA NI KAMA UMEWADIA
  7. Epuka nguo au mapambo ambayo yana tabia ya kushika moto kwa urahisi, Kwani msuguano (friction) wa hewa (upepo mkali) kati yako na mazingira wakati huo utakuwa mkubwa (over 600mph) kiasi cha kuweza hata kupelekea fire combustion, hii iwe tabia yako kwa wakati huu ambao weng hawajui kwamba ni kati ya nyakati critical sana kwa amani na uwepo wa dunia kwa ujumla.
La mwisho, Usiamini kwamba dunia ilijengwa kuwa na amani milele, Dunia ina amani ndani yake lakini waliokabidhiwa hawana matumizi yoyote na amani na wanatamani siku zote amani isiwepo!

Mtu yeyote anayeamini kwamba amani duniani itabaki hivi to the near future anatakiwa kuutazama tena mtazamo wake,
UKIONA BABA ANABEBA PANGA SHAMBANI, NAWE BEBA HATA KISU, YAWEZEKANA ANAYAJUA MENGI YA HUKO SHAMBANI. (Vladmir Putin)



Msherwa.


images (14).jpg
images (14).jpg
 
Mahandaki kwa Tanzania labda kwenye military base ama secure government offices lkn kwa watanzania wa kawaidaa sidhani kama wanaidea zozote yahio situation
 
Back
Top Bottom