Jinsi ya kuisikia Sauti ya Mungu

Jinsi ya kuisikia Sauti ya Mungu

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,601
Reaction score
7,216
Ndugu zangu, Mungu yupo na amekuwa akiongea na watu wake tangu zamani hadi leo. Katika maisha ya kila siku, Mungu anatumia njia mbalimbali kuwasiliana na sisi. Lakini mara nyingi tunakosa kuisikia sauti yake kwa sababu ya 'kelele' nyingi za ulimwengu huu au mioyo isiyotulia.

Katika kitabu cha Waebrania 3:7-8 tunaambiwa hivi:
“...mkisikia sauti yake leo, msiwe wakaidi kama wakati ule waliponiasi...kule jangwani."

Andiko hilo linatuhimiza kuwa watii haraka tunaposikia Mungu akinena nasi, ili tusikose neema yake na baraka zake kama Waisraeli walivyokosa kwa sababu waliacha kumtii Mungu walipokuwa jangwani.

Hebu basi leo tuangalie jinsi ya kuisikia sauti ya Mungu anaposema nasi. Mungu anaweza kusema nasi kwa njia zifuatazo:

1. Kupitia Neno lake (Biblia)
Mara kwa mara Mungu hunena nasi kwa njia ya Maandiko. Biblia ni sauti ya Mungu iliyoandikwa. Tukisoma Biblia kwa moyo wa maombi, Roho Mtakatifu hufanya Maandiko hayo yawe hai na kutuelekeza yatupasayo kufanya katika maisha yetu.

Timotheo aliambiwa hivi:
"Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha ya adili” (2 Timotheo 3:16).

Mtu aliye na huzuni au aliyechanganyikiwa, akisoma Zaburi au Mithali, ghafla ataona aya moja inamgusa, yaani inaelezea afanye nini katika hali hiyo aliyo nayo. Hapo ni Mungu anakuwa amesema naye.

2. Kwa njia ya Roho Mtakatifu ndani yetu
Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atatuongoza na kutufundisha yote. Roho huyu hukaa ndani ya waaminio na ananena kupitia dhamiri zetu, msukumo wa ndani, au amani isiyoelezeka.

Paulo alizuiwa na Roho Mtakatifu asiende kuhubiri Asia (Matendo 16:6-7) — sio kwa sauti kubwa, bali kwa mwongozo wa ndani. Vivyo hivyo kuna wakati mtu anapanga jambo fulani lakini moyoni anahisi "kukosa amani” kulifanya jambo hilo — hiyo mara nyingi ni sauti ya Mungu kupitia Roho wake.

3. Kwa njia ya maombi na utulivu wa moyo
Tunapomuomba Mungu, tunatakiwa sio tu kumwambia mahitaji yetu bali pia kutulia na kusikiliza anatuambia nini kuhusu mambo tuliyomuomba. Mungu anaweza kunena nasi ndani yetu kwa utulivu. Hivyo ni muhimu tujizoeze kutulia na kuisikiliza sauti yake baada ya maombi.

Nabii Eliya hakumsikia Mungu katika upepo mkali wala tetemeko la ardhi, bali katika “sauti ya upole mtulivu” (1 Wafalme 19:12).

Watu wengi hushuhudia kuwa walipotulia baada ya maombi, ghafla walipata wazo au msukumo fulani ulioleta suluhisho la matatizo yao.

4. Kwa njia ya ndoto na maono
Mungu anaweza kuongea na mtu kwa njia ya ndoto na maono hasa pale mtu anapokuwa tayari kupokea ufunuo wa kiroho. Hata hivyo sio kila ndoto inatoka kwa Mungu. Baadhi ya ndoto zinasababishwa na uchovu tu. Lakini kuna ndoto fulani huja na uzito wa kipekee kutoka kwa Mungu.

Yusufu, baba mlezi wa Yesu, alipokea maagizo kutoka kwa Mungu kwa njia ya ndoto (Mathayo 1:20; 2:13).

Kuna watu wengi pia wameshuhudia kwamba wameota ndoto zenye ujumbe wa kiroho.

5. Kupitia Watumishi wa Mungu na ndugu katika Kristo
Mungu anaweza kusema na sisi kupitia watumishi wake — yaani wahubiri, walimu wa Biblia, au hata ndugu wa kawaida kanisani.

Kwa mfano, Mungu alimtumia Eli kumpa ujumbe kijana Samweli(1 Samweli 3:9).

Kwa njia kama hiyo Mhubiri, Mwinjilisti au Mwalimu wa Biblia anaweza kuhubiri au kufundisha ujumbe unaogusa hali yako moja kwa moja — ukahisi kabisa Mungu amenena nawe kupitia mtu huyo.

Mpaka hapo naamini umeona sasa kuwa kuisikia sauti ya Mungu sio jambo la ajabu bali ni sehemu ya maisha ya kiroho kwa wote wanaomwamini Mungu. Kumbuka tu, ili uweze kuisikia sauti ya Mungu kinachohitajika ni moyo mnyenyekevu, usikivu wa kiroho, na utii; na kwamba mara nyingi Mungu hasemi kwa sauti kubwa bali kwa sauti ya utulivu inayosikiwa na moyo uliotulia. Hivyo kama umekuwa ukimuomba Mungu jambo fulani, tarajia kwamba Mungu anaweza kusema na wewe kuhusu jambo hilo ulilomuomba - kwa njia mojawapo katika hizo.
 
Mimi pia Mungu amekuwa akisema nami mara nyingi kwa njia hizo na kuniongoza yanipasayo kufanya. Kila ninapotii sauti yake inayonielekeza kufanya jambo fulani, nimekuwa nikiona mafanikio katika mambo ya elimu, katika kazi, biashara na maisha kwa ujumla.
 
Namkumbuka ndugu mmoja, alikuwa anatembea barabarani kisha akaona kifaa fulani mbele yake kimedondoshwa. Akasikia sauti inamuambia kwa upole akiokote kifaa hicho ni cha mama mmoja. Akapuuza sauti hiyo. Baadaye akakutana na mama huyo anahuzunika amepoteza kifaa hicho. Huyo ndugu akajilaumu kwanini hakutii na kuokota kile kifaa.
 
Kama hujaokoka, naamini Mungu amekuwa akisema na wewe kwa njia hizo kukutaka uokoke.

Naamini umekuwa ukisikia msukumo wa kutubu, au sauti inayokukumbusha kuacha dhambi ili uokoke. Kama hujasikia hivyo, basi Mungu anasema nawe sasa:

"Leo, umeisikia sauti yake, usifanye mgumu moyo wako..." (Waebrania 4:7)

Usiipuuze sauti hii inayokuambia uokoke. Usingoje kesho usiyoijua, kwa kuwa leo ndiyo siku ya wokovu. Narudia tena: Kama unaisikia sauti ndani yako inayokuita utubu, hiyo ni sauti ya Mungu. Usiizimishe. Fungua moyo wako sasa. Mwambie Bwana Yesu aingie ndani yako akuokoe na kukufanya kiumbe kipya. Anakupenda, ndio sababu anakuita sasa. Isikie sauti yake na kutii.

Kama uko tayari sasa kuokoka, omba(kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba:

Omba hivi:
"Ee Mungu Baba, nimeisikia sauti yako inayoniita niokoke. Nimeitii sauti hiyo, hivyo leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.

Mungu akutunze na akusaidie kuisikia sauti yake hata katika maeneo mengine ya maisha. Ubarikiwe sana. Amen.
 
Mungu huwa anasema na watu kwa sauti kubwa pia. Katika Biblia, kuna matukio maalum ambapo Mungu alinena kwa sauti kubwa, ya wazi, iliyosikika na wengi au na mtu mmoja binafsi.

Haya hapa baadhi ya matukio ambapo sauti ya Mungu ilisikika waziwazi.

1. Katika Yohana 12:28 Yesu aliomba hivi:
“Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, ikasema, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”

Watu waliokuwepo hapo waliisikia sauti hiyo — wengine walidhani ni radi, wengine malaika. Lakini ilikuwa sauti halisi ya Mungu.

2. Tukio jingine la sauti ya Mungu iliyosikika wazi tunaliona katika Matendo 9:4-7. Hapo Sauli wa Tarso (Paulo) alisikia sauti ikimwambia
“Sauli, Sauli! Mbona waniudhi?”

Wale waliokuwa pamoja na Sauli waliisikia sauti hiyo lakini hawakumuona mtu aliyeongea.
 
Mpaka hapo tumeona kuwa Mungu husema na wanadamu na tumeona jinsi ya kuisikia sauti ya Mungu. Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba Mungu hasemi kinyume na Maandiko. Kwa mfano, Mungu hawezi kukuambia nenda kamuue mtu fulani. Kuua ni kinyume na Neno la Mungu. Hivyo ukisikia sauti inayokuambia jambo lililo kinyume na mapenzi ya Mungu, ipinge sauti hiyo - sio ya Mungu. Usisahau pia kuwa sauti ya Mungu huambatana na amani ya rohoni na mara nyingine hujirudia kwa uthibitisho wa watu wa Mungu au hali.

Wakolosai 3:15
"amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu..."

2 Wakorintho 13:1
"...Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.”

Usikimbilie kutangaza kile ulichosikia; tafuta uthibitisho wa kiroho kwanza.
 
Kama hujaokoka, naamini Mungu amekuwa akisema na wewe kwa njia hizo kukutaka uokoke.

Naamini umekuwa ukisikia msukumo wa kutubu, au sauti inayokukumbusha kuacha dhambi ili uokoke. Kama hujasikia hivyo, basi Mungu anasema nawe sasa:

"Leo, umeisikia sauti yake, usifanye mgumu moyo wako..." (Waebrania 4:7)

Usiipuuze sauti hii inayokuambia uokoke. Usingoje kesho usiyoijua, kwa kuwa leo ndiyo siku ya wokovu. Narudia tena: Kama unaisikia sauti ndani yako inayokuita utubu, hiyo ni sauti ya Mungu. Usiizimishe. Fungua moyo wako sasa. Mwambie Bwana Yesu aingie ndani yako akuokoe na kukufanya kiumbe kipya. Anakupenda, ndio sababu anakuita sasa. Isikie sauti yake na kutii.

Kama uko tayari sasa kuokoka, omba(kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba:

Omba hivi:
"Ee Mungu Baba, nimeisikia sauti yako inayoniita niokoke. Nimeitii sauti hiyo, hivyo leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.

Mungu akutunze na akusaidie kuisikia sauti yake hata katika maeneo mengine ya maisha. Ubarikiwe sana. Amen.
Ushauri wa bure

"Mwambie Huyo mungu wako awache kujitekenya na kujichekesha mwenyewe"
 
Nimekaaa siti ya mbele nisikie maneno Yake wakati watu wako bize na mambo ya Dunia hii Yesu atakua kama mwizi iyo ni muhimu kusikia sauti yake wakati huu wa hatari ambayo sauti za uongo na nadharia ikipotosha ukweli wa Mungu, ubarikiwe kwa habari hii njema ya Injili
 
Ushauri wa bure

"Mwambie Huyo mungu wako awache kujitekenya na kujichekesha mwenyewe"
Chonde chonde ndugu yangu ManchoG
Usidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka (Wagalatia 6:7-9)
Hivyo jifunze kuuzuia ulimi wako usinene mabaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom