Jinsi ya kufanya vizuri kwenye kila interview utakayoitwa

Learn First

New Member
Joined
Aug 18, 2022
Posts
2
Reaction score
2
Habari zenu.

Natumaini kuwa hamjambo na gurudumu la elimu mnazidi kuliendesha vema.
Mimi pia sijambo. Namshukuru Mungu.

Moja kwa moja kwenye Mada.

Tanzania ni kati ya nchi za Africa zenye wasomi wengi wa vyuo vikuu ambao wako mtaani bila ajira. Tena wengi wao wana vigezo toshelevu vya kuwa kwenye ajira rasmi, za kudumu au hata za muda. Kwa bahati mbaya nafasi hiyo inakuwa ngumu kwao kuipata.

Wasomi hawa asilimia kubwa ni vijana wenye nguvu na stadi stahiki tena wenye sifa za ziada kuwa kwenye mifumo, ila kuna mambo machache yanayopelekea mifumo kuwakataa au kutokuwa kwenye nafasi ya kupata ajira.

Leo sitazungumzia chochote juu ya mchango wa serikali wala ubovu ama ubaya wa mitaala ya kielimu ya nchi yetu, ila nitazungumzia uhalisia katika upande ambao fursa zinazopatikana inashindikana kuangukia kwenye mikono ya vijana hawa wenye kuweza kuzitumikia ipasavyo.

Hapa nitazungumzia makosa ambayo vijana huyafanya pindi wakiitwa kwenye usaili wa nafasi za kazi mbalimbali . Mengi kati ya haya nayaeleza kutokana na uzoefu wangu baada ya kushuhudia interview nyingi (Mock & Real Interview)

1. CHANGAMOTO YA LUGHA

Kwa uzoefu, interview nyingi kwenye taasisi na makampuni binafsi hutumia lugha ya Kiingereza (English). Sitaki kuamini kuwa kiwango cha lugha msomi wa chuo kikuu alichonacho kinakuwa haba kutosheleza mahitaji ya maelezo kwenye usaili. Kila aliyesoma chuo, basi alisomea kazi, hakusoma maarifa tu ya jumla ya kumsaidia maisha yake ya kila siku. Kama umeisomea kazi basi kuna mambo ambayo kwa namna yoyote huwezi kushindwa kuyatetea ukiwa mbele ya msaili.

Kinachowashinda wengi sio uhaba wa msamiati wa lugha ya kiingereza, isipokuwa ni hofu, kutojiamini na uelewa hafifu juu ya kampuni au taasisi ambayo mtu anaomba kazi.

Lugha ya kiingereza sio lazima uongee ile misamiati migumu ya kufikirisha sana na ile itakayokushinda kutamka vizuri, isipokuwa jiamini na utumie lugha unayoimudu, msamiati unayoijua vema kujibu kwa usahihi ulichoulizwa.

Epuka kutumia lugha na misemo isiyokuwa rasmi kwenye interview. Mfano wa maneno ambayo nimekuwa nikikutana nayo kwenye interview nyingi ni "Guy/Guys" "oh shit I forgot" kumuita interviewer "bro/sister" na mambo yanayofanana na hayo.
 
mbona hujamalizia sasa mkuu
 
Malizia Mkuu
 
2. KUTOFANYA UTAFITI WA KUTOSHA JUU YA KAMPUNI, SHIRIKA AU TAASISI ILIYOKUITA KWENYE INTERVIEW

Kwenye kila interview lazima utaulizwa swali litakalotaka ueleze unachokijua kuhusu kazi unayoiomba au shughuli za zinazohusu brandi inayotarajia kukuajiri.

Swali hili kutokana na kutojibiwa vizuri msaili humuona msailiwa kama msanii tu anayejaribu kupata 'ana ana-do' ambapo atajenga imani kuwa kama msailiwa ameshindwa kufanya utafiti wa kutosha juu ya kampuni au shirika husika je, ataweza kuhangaika kutafuta utatuzi wa changamoto zinazodumu siku akiajiriwa?
Kujibu vizuri swali hili kunamuongezea kujiamini msailiwa na nafasi kubwa ya kupata kuajiriwa (ajira).

Aidha kabla ya kuhudhuria Interview yoyote hakikisha unapitia upya Tangazo la Kazi lililokufanya ukaomba kazi. Chunguza kwa makini majukumu yaliyoainishwa kwenye nafasi ya ajira uliyoiomba, zisome upya sifa za mtu waliyesema wanamhitaji na kisha kama Taasisi husika ina Tovuti (website) nenda katika kurasa zifuatazo.

i. Mission and Vision. Hapa utapata kwa kina kuhusu kampuni au taasisi husika. Hapo utatambua majukumu ya jumla ambayo kampuni, taasisi au shirika linajihusisha. Kuna wakati mwingine utapata hata historia fupi ya kuanzishwa kwake hapo.

ii. About Us
Karibu kila Website ina ukurasa huu. Hapa utapata kiundani juu ya brandi inayokwenda kukusaili, historia, umiliki na umri wa brand au taasisi husika. Vipengere muhimu zaidi ambavyo hutatakiwa kuvisahau ni Mwaka wa kuanzishwa kwake, mwanzilishi, sababu za kuanzishwa, mabadiliko yaliyopitiwa na malengo ya sasa ya kampuni au taasisi husika.

iii. Causes.
Siku hizi kuna mashirika, taasisi au kampuni zenye kipengele hiki. Hapa ni muhimu sana kupasoma kwa kuwa ndio Inapowekwa miradi na malengo mahsusi ya kampuni au shirika husika. Mara nyingi hii huwa katika Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs)

3. ANDAA MAJIBU YA MASWALIBYA LAZIMA KUONGEZA KUJIAMINI.

Kila usaili utakapoitwa lazima kuna maswali manne au zaidi ambayo kwa namna yoyote utayakuta. Si lazima yatajwe sawasawa na ulivozoea, ila itatumika mifumo mbali mbali ya kukuhitaji uyajibu. Yafuatayo ni maswali ambayo lazima utakutana nayo kwenye usaili.

i. Tell me about yourself /Give short description about yourself/ Who is (jina lako)/ What is your education background/May I know you? n.k

Swali hili linaweza pia kuja katika sura tofauti na hii ila majibu yake yanalenga uelezee kwa ufupi kuhusu wewe binafsi, majina matatu, historia fupi sana ya taaluma yako ukianzia sekondari mpaka na uzungumzie kidogo vitu vilivyokuhamasisha kusoma ulichokisoma huku ukihusisha na nafasi ya kazi unayoiomba.

ii. Why should I hire you / What qualities do you possess / Why do you think you are the perfect candidate for this post / Differentiate yourself from all other candidates. n.k

Swali hili linalenga kukupima 'confidence' uliyonayo. Sio nia ya msaili wewe kuwazungumzia vibaya wasailiwa wenzako isipokuwa anataka umshawishi kwa nini akuajiri.

Interview ni sawa na kampeni, au ni sawa na kutongoza msichana mzuri sana au ni sawa na kuchimba madini. Ina maana kuwa atakayefanikiwa haimaanishi anapaswa kujibu namna bora zaidi au kuwa hakuna jibu moja sahihi la kujibu swali hili. Unatakiwa uwe na stadi za ku-improvise mambo au majibu yako kichwani, uwe na uwezo mkubwa wa kuzungumza bila kutoka kwenye mada, uepuke kigugumizi na kufikiria zaidi wakati wa kutoa jibu la swali hili, eyes contact na interviewer iwepo, punguza "gap-fillers" zisizo za msingi zile za ...uuuum.... Aaah..... Well..... Eeeeh... Wakati unatafita cha kujibu. Hiyo inamuonesha msaili kuwa wewe binafsi hujiamini
 
Back
Top Bottom