Jinsi ya kuepuka malumbano kwenye mahusiano

hypothalamus

Senior Member
Feb 19, 2018
126
142
Moja ya changamoto kubwa kwenye mahusiano ni jinsi ya kukabiliaana na tofauti zetu.Mara nyingi wapenzi wanapotafautiana hali huwa inabadilika na kuwa malumbanao na pengine kuwa ugomvi kabisa.
Ghafla wanaacha kuongea kama wapenzi na kuanza kutupiana maneno yanayo muumiza kila mmoja.Kama ilivyo mawasiliano ndio nguzo kubwa ya ustawi wa mahusiano,malumbano ndio kiharibifu kikubwa Zaidi cha mahusiano.

Siri pekee ya kuepuka malumbano ni kuwasiliana kiupendo na kwa heshima.
Kutofautiana haipawsi kuwa chanzo cha malumbano,chanzo cha malumbano huwa ni jinsi tunavyowasiliana wakati wa ‘’kutofautiana’’.Mwanzo wapenzi huwa wana lumbana kuhusu tofauti iliyo jitokeza baada ya dakika tano wanaanza kulumbana kwa nini wanalumbana na sio ile tofauti yao tena
Pasipo kujua wanaanza kuumizana,utofauti uliotakiwa kumalizwa kwa makubaliano na kuelewa tofauti zetu unabadilika na kuwa ugomvi


Kwa nini kutofautiana huwa kunabadilika na kuwa malumbano yanayoumiza?

Kinachoumiza huwa sio walichokisema wapenzi wetu lakini kinacho umiza huwa ni jinsi gani wamekisema?
Mwanaume anapokuwa challenged,attention yake hubadilika na huanza kuforce kuwa sahihi na husahau kuwasiliana kiupendo.
Ghafla uwezo wake wa kuwasiliana kwa kunyenyekea na kwa heshima hupungua.Huwa hatambui kwa jinsi gani badiliko hili la haraka linavyo badilisha jinsi mpenzi wake anamchukulia kwa wakati huo.
Katika hali hii tofauti ndogo tu huwa mwanamke anaichukulia kama ameshambuliwa,ombi anaichukulia kama amri.
Kiasili mwanamke huwa anaanza kupinga hii hali hata kama anachoombwa kukifanya angekichukulia kiupendo nyakati ambazo sio za malumbano.
Mwanaume pasipo kujua anamuumiza mpenzi wake kwa jinsi anavyowasiliana kwa wakati huo huanza kufoka kwa nini mpenzi wake anampinga
Pasipo kujua anaanzisha ugomvi kwa kipindi hiki mwanaume anabase kwenye kujidefend kwa nini yupo sahihi huku mwanamke akijidefend kutoka katika aina ya mawasiliano yanayomuumiza yaliyoanzishwa na mpenzi wake.Si rahisi mwanaume kutambua kiasi gani maneno yake yanaumiza kwa kuwa kiuhalisia mwanaume haathiriwi na aina hiyo ya maneno.
Tofauti na mwanaume,mwanamke anapokuwa challenged uongeaji wake hubadilika na kuwa ya kutokuwa na imani na mpenzi wake na kukataa kila anachoambiwa.Uongeaji huu huwa unamuumiza sana mwanaume.
Mwanamke huanza kutupa maneno kwa kukumbushia negative feelings za mpenzi wake na kuanza kumpa ushauri ambao kwa mwanaume huuchukulia kama kumkosea heshima,ghafla mwanaume huanza kureact(baadhi kwa kupiga) kwa kuwa anajua hawezi kushindana kwa battle ya maneno na mwanamke.
Ili kuepuka malumbano inapaswa tujue kuwa tatizo huwa sio tofauti zetu lakini ni jinsi gani huwa tunaziwasiliana wakati wa utofauti huo
Jipe muda kidogo,acha kuongea kitu kwa muda na tafakari njia sahihi zaidi ya kuongea jambo ambalo mnatofautiana


Vitu vinne vya kuviepuka wakati wa malumbano ambavyo vinaweza kuharibu kabisa mahusiano

1.Kupigana
Hiki kitendo kwa asilimia kubwa huanzishwa na wanaume.Unaweza refer hapo juu kwa nini mwanaume huwa anafikia hatua hii.Wapenzi wanapopigana huwa wanapoteza uwezo wao wa mwanzo wa kuwa wawazi hatimae hupoteza nguvu ya upendo waliyokuwa nayo mwanzoni


2.Kujiepusha
Hiki kitendo pia huanzishwa na mwanaume.Ili kuepuka ugomvi mkubwa mwanaume hujiepusha kuongelea jambo linalo watatiza,ni kama huanzisha vita baridi.Kwa baadhi ya wanaume hali hii huwa mbaya zaidi kwa kumkomesha mwanamke kwa vitendo kama kuchelewa kurudi au kupunguza vitu vya kimapenzi ambavyo alikuw akimfanyia mpenzi wake.Hali hii huatarisha uhai wa mahusiano


3.Kufake
Hiki kitendo huanzishwa na mwanamke.Kuepuka ugomvi mwanamke hufake kama vile kila kitu kipo sawa kwa lugha rahisi tunasema huwa ana fake smile.Kadri hali inavyoendelea mwanamke huyu huumia ndani kwa ndanu kwa kuwa anatoa zaidi kumfurahisha mpenzi wake lakini yeye haridhiki na anachopata kwenye mahusiano.


4.Kukubali kubeba lawama
Hiki kitendo hufanywa na mwanamke.Ili kuepuka ugomvi,mwanamke hukubali kubeba kila lawama atakazopewa na mpenzi wake,hukubali kushuka katika kila ugomvi unaotokea.Mwanzoni huonekana kama mapenzi mazuri yasiyo na matatizo yoyote,lakini itafikia kipindi ambacho mwanamke ata fed up na anaweza kuchukua maamuzi ambayo hushangaza kwa kuwa mahusianoi haya yalikuwa hayaoneshi dalili yoyote ya kufa

Moja ya kosa kubwa ambalo mwanaume hulifanya ni kumuacha mwanamke aweke mambo yanayomuumiza ndani asipate nafasi ya kuyatoa.Hali hii ikiendelea kwa muda huatarisha uhai wa mahusiano.
 
Back
Top Bottom