Jinsi ya kudeal na mama mkwe mpiga mizinga

Jinsi ya kudeal na mama mkwe mpiga mizinga

kwahyo ma mkwe alizaa akiwa sweet 16 duh kaz ipo
 
she is desperate, i think she need a man,..suala sio kumpa hela, suala ni yeye kuwa ananiomba omba sana mimi hela, utafika wakati hata huyu wife wangu atashindwa kunielewa and all that.

Aisee.... kumbe tatizo ni kubwa kuliko nilivyodhani....
 
Dogo naona umesahau msemo usemao ukipenda boga penda na ......Afu naona kama umemdhalilisha mama mkwe wako sasa wewe unaombwa hela tu unatoa siri adhalani wengine tumejenga hadi ukweni na bado tunapeleka hela za matumizi..lakini tunachukuli easy tu acha kulialia..:baby:
 
Hawa watu wamependana acha wale maisha. Hata hivyo jamaa muungwana kuowa kabisa wakati sisi chapa ilale🙁
 
Nimefunga ndoa mwaka jana na mchumba wangu ambaye tulianzia kwenye urafiki wa muda mrefu, uchumba hatimaye ndoa. Msichana niliye muoa was just born in 1995. Baba yake alizaliwa mwaka 1970 na ni rafiki yangu mkubwa sana. Huyu msichana pamoja na wadogo zake wamelelewa na mama wa kambo, baba yao aliachana na mama yao tangu mwaka 2005 so sasa hivi mama yao anaishi home kwao hapa hapa mjini. Huyo mama mkwe amezaliwa mwaka 1977.

Tatizo la mama mkwe, anapiga sana mizinga. Nilijitambulisha kwake kwa njia ya simu mnamo mwaka jana. Mwezi mmoja kabla ya kwenda kutoa mahari ukweni.

Siku naongea nae tu kwenye simu, nikapigwa mzinga siku hiyo hiyo.

Hzikupita wiki mbili nikapigwa tena mzinga mwingine. Halafu kitu anacho nikera, akipiga mzinga ukamwambia siku fulani halafu hiyo siku ukapotezea basi ana fanya follow up, atapiga simu na kutuma meseji akiulizia kama umeshatuma mzigo au vipi.

Kila wiki lazima apige mzinga.

Hii kwangu ni kero kubwa sana na nadhani siwezi kuivumilia hata kidogo coz ninaishi kwa kufuata utaratibu ulio nyooka.

Nimejaribu kumchimba baba mkwe akaniambia u know she is so desperate and all that.

Kumwambia mama mkwe sipendi unavyo nipiga mizinga, siwezi coz najua kibongo bongo sio poa kivile.


Mama mkwe analipa kiukweli tena analipa sana. sana tu yani, tena sana, tena sana yani!

Kesho nyumbani kwangu, kutakuwa na sherehe ya kuzaliwa ya binti wangu wa kwanza. Mama mkwe atakuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa.

Jamani kama kuna bachelor yoyote humu ndani au mwanaume yoyote ambaye anajua anaweza kutunza mwanamke please naomba ani- pm, nitamkutanisha na mama mkwe , amkeep busy ili aache kunisumbua bana.


OKOA NDOA YANGU, OKOA NDOA YA MWANA-JF

pole mkuu kwa yaliyokukuta mkuu tafuta solution fasta.
 
Ha ha ha ndio maana wengine kabla ya kuoa tunaangalia na familia yenyewe, we unaoa kwao hakuna hela unategemea nini sasa? Au usikute unaletewa na wadogo za Mke wako uwalee mi hayo mambo sitaki hata kuyasikia.
 
she is desperate, i think she need a man,..suala sio kumpa hela, suala ni yeye kuwa ananiomba omba sana mimi hela, utafika wakati hata huyu wife wangu atashindwa kunielewa and all that.

Kumbe kama ni hivyo mshirikishe wife katika suala hilo. Usirudie kumtumia hela wewe mwenyewe akiomba mjulishe mkeo na umkabidhi yeye ndiye atume kama ataridhia. Atume asitume hayo wewe usiingilie. Ikiwa mama mkwe atakumbushia mwambie hela ulishamkabidhi mkeo amtumie kwa hiyo awasiliane naye mwenyewe. "Kwa nini umpe mkeo usinitumie moja kwa moja?" Mwambie niko bize kwa hiyo masuala yote yayohusu kutuma hela kwa ndugu na jamaa umemkabidhi mkeo, kwishney! Na uwe na msimamo thabiti katika hilo.
 
Ha ha ha ndio maana wengine kabla ya kuoa tunaangalia na familia yenyewe, we unaoa kwao hakuna hela unategemea nini sasa? Au usikute unaletewa na wadogo za Mke wako uwalee mi hayo mambo sitaki hata kuyasikia.

Mambo mengine yanajitokeza wakati pingu za maisha ziko mikononi, too late! Hali ya uchumi wakati mwingine sio kipimo kizuri. Unaweza kuoa kwenye familia yenye unafuu wa maisha ukasumbuliwa sana lakini mwingine akaoa familia ya kimaskini asisumbuliwe kihivyo labda mara chache kukiwa na mahitaji ya muhimu kama ada za shule, nk. Watu wengine wana tamaa tu ya hela, wanataka maisha ya juu kwa gharama za wengine hasa wakijua uko vizuri kiuchumi shida haziishi.
 
kwahyo ma mkwe alizaa akiwa sweet 16 duh kaz ipo
Mama mkwe alizaa akiwa na miaka 16 na mkeo sasa ana miaka 18 ulimuuoa akiwa miaka l7 na unasema ulianza naye uchumba siku nyingi.Kwa ufupi umeoa familia ya vicheche hawasomi pia hapo waweza kula kuku na mayai usipojiangalia umepotea njia mkuu
 
Amesema huyo ni mama wa kambo,soma habar vzur

Haapana amesema huyo binti amelelewa na mama wa kambo ila kwa sasa mama yake anaishi home kwao means mama mzazi labda afafanue vizuri huyo mama anayepiga nizinga ni wa kambo au mzazi
 
Sasa mzee mzima si ukaushe follow up zinakutisha nini...UKAUZU ZAIDI YA DAGAA UTAKUSAIDIA,ukikaa we ni kugawa hela daily maendeleo utafanya sa ngapi???
 
Haapana amesema huyo binti amelelewa na mama wa kambo ila kwa sasa mama yake anaishi home kwao means mama mzazi labda afafanue vizuri huyo mama anayepiga nizinga ni wa kambo au mzazi

Anaye piga mzinga ni mama ake mzazi..Kuna watu wameniambia, nimtongoze nimchape nao halafu niimwage, so urafiki ama ukaribu wetu uwe umefikia hapo, but to me that was a crazy idea
 
Dogo naona umesahau msemo usemao ukipenda boga penda na ......Afu naona kama umemdhalilisha mama mkwe wako sasa wewe unaombwa hela tu unatoa siri adhalani wengine tumejenga hadi ukweni na bado tunapeleka hela za matumizi..lakini tunachukuli easy tu acha kulialia..:baby:

Kaka umeshikwa pabaya
 
you are not systematically organized. mama mkwe inabidi awekewe kiwango fulani cha kuwa anasaidiwa regularly,

nadhani yeye mwenyewe keshatambua kuwa wewe hauko kimsaada kwake, naweza sema hivyo japo si responsibility ya wewe kumsaidia kila siku..

kuna mbinu za kumkwepa nyingi tu endapo utakuwa na roho ya paka.... kwani ukisema huna, atakunyang'anya mwanae?

kwani ukisema niwie radhi mama, kwa sasa siwezi kukusaidia, na wala siwezi ahidi lini, atakulaani?

hujiamini kijana... angalia usije ukawa yahaya.
 
Back
Top Bottom