Nimefunga ndoa mwaka jana na mchumba wangu ambaye tulianzia kwenye urafiki wa muda mrefu, uchumba hatimaye ndoa. Msichana niliye muoa was just born in 1995. Baba yake alizaliwa mwaka 1970 na ni rafiki yangu mkubwa sana. Huyu msichana pamoja na wadogo zake wamelelewa na mama wa kambo, baba yao aliachana na mama yao tangu mwaka 2005 so sasa hivi mama yao anaishi home kwao hapa hapa mjini. Huyo mama mkwe amezaliwa mwaka 1977.
Tatizo la mama mkwe, anapiga sana mizinga. Nilijitambulisha kwake kwa njia ya simu mnamo mwaka jana. Mwezi mmoja kabla ya kwenda kutoa mahari ukweni.
Siku naongea nae tu kwenye simu, nikapigwa mzinga siku hiyo hiyo.
Hzikupita wiki mbili nikapigwa tena mzinga mwingine. Halafu kitu anacho nikera, akipiga mzinga ukamwambia siku fulani halafu hiyo siku ukapotezea basi ana fanya follow up, atapiga simu na kutuma meseji akiulizia kama umeshatuma mzigo au vipi.
Kila wiki lazima apige mzinga.
Hii kwangu ni kero kubwa sana na nadhani siwezi kuivumilia hata kidogo coz ninaishi kwa kufuata utaratibu ulio nyooka.
Nimejaribu kumchimba baba mkwe akaniambia u know she is so desperate and all that.
Kumwambia mama mkwe sipendi unavyo nipiga mizinga, siwezi coz najua kibongo bongo sio poa kivile.
Mama mkwe analipa kiukweli tena analipa sana. sana tu yani, tena sana, tena sana yani!
Kesho nyumbani kwangu, kutakuwa na sherehe ya kuzaliwa ya binti wangu wa kwanza. Mama mkwe atakuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa.
Jamani kama kuna bachelor yoyote humu ndani au mwanaume yoyote ambaye anajua anaweza kutunza mwanamke please naomba ani- pm, nitamkutanisha na mama mkwe , amkeep busy ili aache kunisumbua bana.
OKOA NDOA YANGU, OKOA NDOA YA MWANA-JF