Jinsi ya kuanzisha day care

Jinsi ya kuanzisha day care

bless 2011

Member
Joined
Dec 20, 2021
Posts
19
Reaction score
17
Habari zenu, naomba mwenye idea ya Day care anisaidie ukitaka kufungua day care unatakiwa uwe na vigezo gani na nini kinahitajika ili umiliki Day care na unatakiwa kuanza na watoto wangapi?
 
Mtaji wa Day care Ni UAMINIFU kutoka kwa wazazi.

Wakikuamini unaweza kuanzia hata nyumbani kwenu.
 
Sehemu yenye fence itakayozuia watoto kutoka nje bila uwangalizi.

Sehemu ya michezo ya nje; mfano kucheza mpira au kucheza na baiskeli.

Sehemu ya michezo ya Ndani; mfano kusoma, kuchora nk, saa ya chakula unaweza kutumia meza hizo hizo kulia chakula.

Sehemu ya kupumzika; unafahamu watoto wanahitaji kulala kama sehemu ya kukua. Wakisha kula unaweza kuwatandikia mikeka wakalala.
Mvua ikiwa inanyesha na hawawezi kutoka nje, unaweza kutumia sehemu hii kuwaonyesha cartoons.

Jiko la kupikia uwe na mpishi. Vyakula vya watoto mara nyingi wanapenda wali maharage au wali kabichi. Wazazi warakueleza watoto wao wasicho kula.

Ukiwa na uwezo unaweka vyoo vya watoto, milango inakua nusu ili wakihitaji msaada waite mkubwa wa kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom