Jinsi ya kuandaa French Toast

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Mahitaji:

  • Mkate vipande vinne (uliokatwa vipande vikubwa ili usilowe sana)
  • Mayai 4
  • Maziwa nusu kikombe
  • Mdalasini (ama vanila) kijiko kimoja
  • Asali vijiko viwili ama Jam ya ladha yeyote unavyopenda
  • Mafuta ya alizeti ama mafuta mazito kama kimbo

breakfast-009.jpg

Jinsi ya kuandaa:
Changanya mayai, Maziwa, Mdalasini (ama vanila).Koroga mpka uone iko tayari.(unaweza kusaga kwa blender ama kupiga kawaida tu kwa mkono).

Chukua mikate yako iliyokatwa vipande vikubwa chovya kwenye mchanganyiko huo, gueza mkate halafu weka pemben kwa dakika 10 tu.

Chukua kikaango weka mafuta yaive kisha anza kukaanga mikate, panga mikate itoshe kwenye kikaango. hakikisha unagueza mikate inapokuwa ya hudhurungi(brown). Kuwa makini isiungue.

Chakula chako kipo tayari.. Panga kwenye sahani yako... mimina Asali kwa juu kisha pamba kwa vipande vya matunda upendayo.(ili iwe laini na nzuri ipashe asali yako kwenye microwave ama kwenye jiko lako)


E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Back
Top Bottom