Stanley Mims
Member
- Aug 29, 2020
- 47
- 86
1 Pet 3:7 SUV
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
........................................................................
Jumatano moja ya mwisho wa Mwaka 2023, yaani mwezi Disemba, saa 7:38 Asubuhi nilipokea simu kwa Mwanamume mmoja aliyejitambulisha kama James (Jina si halisi); aliniuliza kama namjua Agnes (Jina si halisi), nikamuuliza
"Agnes nani?" Niliuliza jina la pili ili kujua, ni yupi anamzungumzia kati ya Agnes ninao wajua. Nikamjibu "NDIO"
Akaniuliza tena mimi ni nani yake.
Kutoka hapo nikatambua tu kuna kitu hakipo sawa, Ila, ni Kaliba yangu kupokea taarifa za mitindo yote bila kutanguliza jazba.
Akaniambia yeye ni Mume wake; na akaanza kunipandishia sauti kuhusu mimi kuwasiliana na mke wake kwamba angenifanya chochote kile bila kumzuia na nikae mbali sana na mkewe; na kama namtaka yeye hana muda wa kumbembeleza Mwanamke, aende akadai talaka aje niishi nae, ila kama sivyo nimkome sana.
Ikabidi nishushe pumzi, nafsi yangu ikajaribu kuvaa kiatu chake, nilishindwa kwa kweli, nikaona ana kila sababu ya kuongea vile. Ila, nikajisemea moyoni "Amefanikiwa"; hapa sikumaanisha huyu ninayezungumza nae kwenye simu, bali Agnes.
Kisa kilianza hivi.
Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na huyu dada; miaka kadhaa ya nyuma, mpaka mwaka tuliomaliza chuo; nilimuacha, ni Mwanamke aliyeharakia maisha, alikuwa na hulka ya kulazimisha ndoa kwa maneno kwa upande wangu, ilifika mpaka wakati tunakwazana. Sikuwa na amani kwa wakati fulani, kwa sababu ndoa niliitaka, sidhani kama kuna Mwanamume kwenye dunia hii awe mjinga kiasi cha kutomuoa Mwanamke kama Aggy, ila purukushani zake zilinitia mashaka; mbaya zaidi kuna kisa kilitokea kikafanya tusiwe wapenzi tena.
Kutoka pale mwenzangu alikuwa na kinyongo na mimi, na kwa sababu ya upendo wake kwangu, kuna namna yoyote alifanya kupata Mawasiliano yangu.
Mwanzoni mwa Mwaka 2021, alinipigia kwa namba fulani ambayo ilikuwa ngeni kwangu, ni wakati ambao hata mimi ndio nilikuwa naanza kujitafuta kimaisha.
"Unaishi wapi siku hizi?" Aliniuliza, na zaidi akapenda kuniona; Unajua nini?
Wanawake walioachika (Kimahusiano) wana tabia ya kujua hali za maendeleo kimaisha za Ma Ex wao, lengo afahamu kama alikuwa akililia kufanya maisha na mtu ambaye angemfikisha sehemu fulani..........
Kwa bahati mbaya ama nzuri, niliitikia wito wake; nikafungua moyo, "Karibu, chukua magari ya Mbezi......." nikamuelekeza, na baada ya nusu saa akafika.
.................................................................................
Alifika kwangu; ila mimi sikuwa nakaa kinyonge kwa sababu tangu tuachane, sikuwahi kumuamini tena, ilikuwa kila muda nakaa kuangalia response yake kwa habari nilizompa, yeye alikuwa cheerful (Samahani kama ulikimbia umande).
Tukapiga story, na kucheki movie (sikupasha of course); baadae nikaenda kuoga.
Wakati ambao mimi naoga, yeye kumbe aliingia kwenye simu yangu ya button, akacheki mesej, akakuta Mwanamke ambaye mimi nilikuwa nachat nae; akachukua namba yake.
Badae nikamsindikiza stendi, akapanda gari na kusepa, ilipofika Miezi kadhaa badae, kumbe alinivutia muda wote huo ifike siku ya birthday yangu ani "suprise" na kweli alifanya hivyo, aka screenshot DP ya mpenzi wangu, kisha akanitumia kwa WhatsApp; for sure nilim mind sana, tuligombana kwa sababu ya ile Incident, ila kama kawaida yangu, siku panic sana; uzuri ni kuwa, hakuwahi kumtafuta, na kuna namna nilimpanga mpenzi wangu akabadili ile namba, na sasa ana nyingine.
Kutoka hapo hatukuwahi kuwasiliana tena; Aggy ameolewa Mwaka jana, baada ya kuolewa akanitafuta tena; sikumpokea vibaya, ila safari hii sikumpokea kama ex wangu kama ilivyo awali, nilimpokea kama mtu nayepaswa kuwa naye makini, nilijua kama ameolewa...... kama kawaida, aliniuliza kuhusu kazi yangu na mahala napoishi, bila hiyana nikamwambia, japo si kiufasaha.
Mimi ni Mwandishi wa Matangazo (Copies) lakini naandika na nyaraka nyingine kama CVs n.k. akaniomba nimuandikie CV na Resume kama alivotaka, anataka kuhama kituo cha kazi, nikaona hakuna baya, nikamwabia anitumie taarifa zake (japo nazijua)
Baada ya kazi, nikamtumia Lipa Namba, lakini hakuwahi kulipa; sikuitazama hii kama shida bali fursa, nilimtajia kiwango ambacho nilijua hawezi kunilipa, lengo ni yeye asinitafute kwa sabaabu nilikuwa namkumbushia deni, and this time hatukuwa na mawassiliano ya mara kwa mara.
Sasa basi, sijui kama wewe ni muumini wa Coincidence ila kuna siku nilikuwa naelekea sokoni, kubeba vikorokoro, huku si kule nilipokuwa naishi mwanzo, ni pengine.
Ghafla bin vu!! Nikamuona anapita kwenye boda, anaelekea upande wa Bar Maarufu ya Mbuzi Online (Utajua mwenyewe ya Wapi); of course tukashangaana sana, akanifanyia ishara ya kuwa atanicheki kupitia simu, nikamwambia poa
Mi nikaendelea na mizunguko yangu, nikabeba vitu kumpelekea babyto alifika ilu apike pike badae nirudi kupiga msosi, nikaenda kukaa kijiweni ghafla meseji ya Aggy inaingia...
NTAENDELEA....